Nina mtaji wa Milioni 35 nataka kufanya biashara Kariakoo

Nina mtaji wa Milioni 35 nataka kufanya biashara Kariakoo

Ni fremu iliyo tupu. Mfano mimi ndiye niliyekua nimeingia mkataba na mwenye nyumba na nataka kuachana na hiyo bishara sasa nataka niuze fremu ikiwa tupu. Yaan mzigo wangu na kila kitu changu nachukua. Nakuachia frem tupu. So kuhusu bei yake tunakubaliana mimi na wewe. Bado ya udalali. Na eneo linapokua potential zaidi ndo gharama inazidi kuwa juu
Hivi ukishatoa kilemba unampa na bei halisi ya kodi ya mwenye nyumba au ndio yale ya kujiongezea percent kwenye kodi halisi ya chumba cha biashara kama wale vijana wa Moshi stand pale?
 
Hana tofauti na mtu anaeuza fixed odds au mikeka. Unajiuliza kama wewe una fixed odds si ubeti sasa upige hizo odds 100! Kwanini umuuzie mtu mwengine 😂😂😂
Hahaha acha mbwembwe dogo.

Unamtoza mtu laki 8 kwa wazo LA biashara, wewe kwanini usiifanye hio biashara na uoneshe mfano kwamba umefanikiwa
 
Mkuu Njoo kanda ya Ziwa nkupeleke visiwani, mfano Ghana, Siza, Giziba, Izinga... Nunua mafuta ya jumla kwa iyoo helaa tumia milioni 20tu utapataa mpaka Lita elfu 12, milioni kumi iliyobaki ni kuandaa eneo la kuweka matenki jenereta na mashine za kupimia mafuta, milioni tano ubakize km backup....kwa msimu mmoja unaweza kuuza mpk lita 50k.....lita unaweza kuinunua tsh 1850 kule wanauza mpaka 2300..

Usisahau kutafuta Mganga huu ni ushauri ambao wengi awatakupa ila ni muhimu, pesa ulindwa na kudhibitiwa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera Sana Mkuu ,35m ni nyingi sana ,tafuta watu wenye vifremu vidogo vidogo wakupe ushauri,wale wenye fremu kubwa watakuzingua.
 
Hivi ukishatoa kilemba unampa na bei halisi ya kodi ya mwenye nyumba au ndio yale ya kujiongezea percent kwenye kodi halisi ya chumba cha biashara kama wale vijana wa Moshi stand pale?
Kwa moshi kwa kweli sina ujuzi nako. Kwa kkoo unaendelea kama kawaida na kodi aliyoiacha mpangaji aliyekuachia
 
Kwa moshi kwa kweli sina ujuzi nako. Kwa kkoo unaendelea kama kawaida na kodi aliyoiacha mpangaji aliyekuachia
Moshi ilibidi manispaa iingilie kati maana hali ilikuwa mbaya, Manispaa wanauza frame laki 2 mpangaji wa kwanza akiichukua anaongeza 2 na malipo unamlipa laki 4 yeye ndio anaenda kulipa manispaa maana ndio anatambulika. Akija mtu wa tatu anamlipa huyu wa pili laki 6 kwa mwezi 😁😁😁!!!

Mwisho Manispaa ikaja kuwatimua wote baada ya kugundua huo uhuni na bei ikapanda ikawa laki 4 na mmiliki haruhusiwi kumpangishia mtu mwengine.
 
Lazima ulipe Kilemba cha kumvua mtu fremu? 😂😂😂 Dah ila biashara za kibongo bwana jau kweli! Hapo Bado hujaanza kusumbuliwa na wazee wa Tai za rangi ya karoti wale 😂😂😂
Yani haikwepeki kuu maana hakuna fremu ambayo haina mtu kwenye zile centre za biashara

Hata wamiliki wakiwa wanajenga fremu mpya anachukua kilemba ndio akupe mlango
 
Moshi ilibidi manispaa iingilie kati maana hali ilikuwa mbaya, Manispaa wanauza frame laki 2 mpangaji wa kwanza akiichukua anaongeza 2 na malipo unamlipa laki 4 yeye ndio anaenda kulipa manispaa maana ndio anatambulika. Akija mtu wa tatu anamlipa huyu wa pili laki 6 kwa mwezi [emoji16][emoji16][emoji16]!!!

Mwisho Manispaa ikaja kuwatimua wote baada ya kugundua huo uhuni na bei ikapanda ikawa laki 4 na mmiliki haruhusiwi kumpangishia mtu mwengine.
Hahahi ila dar si za watu bunafsi?
 
Mkuu Njoo kanda ya Ziwa nkupeleke visiwani, mfano Ghana, Siza, Giziba, Izinga... Nunua mafuta ya jumla kwa iyoo helaa tumia milioni 20tu utapataa mpaka Lita elfu 12, milioni kumi iliyobaki ni kuandaa eneo la kuweka matenki jenereta na mashine za kupimia mafuta, milioni tano ubakize km backup....kwa msimu mmoja unaweza kuuza mpk lita 50k.....lita unaweza kuinunua tsh 1850 kule wanauza mpaka 2300..

Usisahau kutafuta Mganga huu ni ushauri ambao wengi awatakupa ila ni muhimu, pesa ulindwa na kudhibitiwa....

Sent using Jamii Forums mobile app
Kufanya biashara kanda ya ziwa inabd uwe mchawi Tu , watu ni arrogant Sana kule na ni washirikina to the maximum.... Hata jiwe naye ana mindset za hvyo hvyo , uganga na ushirikina ni first attempt katika kusolve matatizo.....na hii inatokana na poor education background
 
Hayo mambo ya kununua nafaka na kuzitunza store, yalishapitwa na wakati, utakuja kulia!! Siku hizi unakuta karibia kila mwaka kuna mvua za kutosha, hivyo mavuno ni mengi, usitegemee bei kupanda ki vile!! Msimu huu waliotunza mahindi wanalia, walinunua gunia kwa sh.50,000 leo hii mtu anataka alinunue kwa 40,000!!! Kwa hiyo pesa yako huku huku kwenye mazao unaweza pata net profit ya hadi milioni 3/ kwa wiki!! Ni kujua chanels tu. Hutajutia
Brother yaani umenisema mimi kabisa bila hata kubakiza neno moja. Nina mahindi gunia 445 nimenunua kwa bei ya 50,000/= na soko halipandi. Hapa najikaza kiutuzima
 
Brother yaani umenisema mimi kabisa bila hata kubakiza neno moja. Nina mahindi gunia 445 nimenunua kwa bei ya 50,000/= na soko halipandi. Hapa najikaza kiutuzima
Pole mkuu!!sisi wafanya biashara wa mazao, tunapata updates za masoko kila muda, kama rais anavyopata za usalama wa nchi!!hahaa, hiyo ipo mpanda watu wanalia huko balaa!!biashara za kuhifadhi mazao store siku hizi, ni nadra sana kupata faida kama ilivyokuwa zamani, kwanza soko la ndani tu liko hoi, kutokana na purchasing power kuwa kidogo, masoko ya nje yapo, lakini nayo ni changamoto, huyo anayejiita NFRA,

Ndio kabisa eti kilo moja anakopa kwa sh.500!!hapo anajisifia amekuja kumkomboa mkulima??bora ununue uuze hiyo 150-200, unayoipata hapo hapo ni bora kuliko kutaka kutafuta 350-400 ya kuomba mungu!!mwaka juzi ni kweli zali liliwaangukia baada ya miaka mingi sana kupata hasara!!na msimu huu tena unakuja na kulingana na halibya mvua hii, mavuno yatakuwa mazuri tena, hapo sasa!!na utunzaji mahindi ni gharama sana tofauti na mpunga.
 
Nauboresha huu ushauri...maana hapa nod kuna hela.

Mkuu kwa pesa yako hiyo fanya hivi.
[emoji117]Tafuta mji ambao ndo unaanza kukua au umekua ila huduma za afya bado hazijakua.
[emoji117]Tafuta nyumba kubwa tu kwa miji kama hiyo kodi unaweza kukuta kwa mwezi nyumba nzima haizidi laki 3.
[emoji117]Baada ya kulipa kodi labda ya mwaka mzima sawa labda na milioni 3.6(hapa lipa kishika uchumba kwanza labda laki 2 kabla ya kulipa kodi).
[emoji117]Nenda manispaa onana na DMO,afanya mpango akakague jengo na mazingira akipitisha.
[emoji117]Fanya ukarabati utakao ambiwa nafikiri kwa nyumba iliyokamilika hautamaliza 5M
[emoji117]Hakikisha mazingira yanavutia,nunua na vifaa sio lazima ununue vipya kuna used kibao vilivyo na hali nzuri kwa gharama nafuu..weka huduma ya dispensary yenye RCH ndani yake...huduma ziwe nzuri na bei ya kawaida...ukiwa na uwezo weka na meno na nunua Ultrasound ya bei poa hata ya milioni 10.
[emoji117]Tafuta wafanyakazi wachache wenye uzoefu kisha kaa mwenye golini wanapolipia ndani ya mwaka utakua mtu mwingine na huduma zikiwa bomba bro utapiga hela mpaka basi.

Mfano mdogo nakupa Dawa kama Doxcy boksi linauzwa 6400 ambao kila boksi linakaa na blister 10 na kila blister moja ina vidonge kumi sawa na vidonge 100.Kwahiyo kwenye boksi moja unatoa dozi 10 dispensary ninayofanya kazi dozi moja wanauza elfu 4 hivyo kwa kila boksi unatoa elfu 40.Drip unazoziona bei ya jumla unanunua 850-1000 ila mtu utamuwekea kwa elfu 10 hapo ukitoa giving set na scalp vein faida yako ni 8000.

Bado sikwambii kwenye kitengo cha Dental jino kung'oa ni elfu 10 ,mng'oaji anaweza chukua elfu 3 ,ukitoa gharama ya ganzi na syringe unakuta unabaki na faida ya elfu 6,,,bado kwemye ultrasound na RCH bado kuna kesi za Kusafisha ,kutahiri nk.

Bro biashara ya afya inalipa hasa ukiwa mjanja na akili nyingi inalipa sana.

Nb:ukishindwa Dispensary basi funguo maabara ya kisasa au pharmacy ule maisha.
Kwa mil 35? Sio rahisi kama unavyodhani nasema hivyo coz nipo katka hiyo kada .labda awe na mil 70 ndio anaweza fanya hivyo vitu,au afungue pharmacy
 
Mkuu usibishe...nina rafiki zangu wawili nimesoma nao Mmoja ameshafungua dispensary kwa bajeti ya 21M tu.
Kwa mil 35? Sio rahisi kama unavyodhani nasema hivyo coz nipo katka hiyo kada .labda awe na mil 70 ndio anaweza fanya hivyo vitu,au afungue pharmacy
 
Kama una hiyo hela njoo nikupe maelekezo.

Katika kufungua Dispensary ishu inakua tu DMO timu yake na wahusika wengine wapitishe jengo wakishapitisha basi swala haliwi gumu kama unavyodhani halafu si lazima kila kitu ununue kipya kuna vitu Used kibao(kama alivyofanya jamaa yangu). La msingi nyumba atakayopanga atafute ambayo haina marekebisho makubwa basi chap tu.
Kwa mil 35? Sio rahisi kama unavyodhani nasema hivyo coz nipo katka hiyo kada .labda awe na mil 70 ndio anaweza fanya hivyo vitu,au afungue pharmacy
 
Mkuu Njoo kanda ya Ziwa nkupeleke visiwani, mfano Ghana, Siza, Giziba, Izinga... Nunua mafuta ya jumla kwa iyoo helaa tumia milioni 20tu utapataa mpaka Lita elfu 12, milioni kumi iliyobaki ni kuandaa eneo la kuweka matenki jenereta na mashine za kupimia mafuta, milioni tano ubakize km backup....kwa msimu mmoja unaweza kuuza mpk lita 50k.....lita unaweza kuinunua tsh 1850 kule wanauza mpaka 2300..

Usisahau kutafuta Mganga huu ni ushauri ambao wengi awatakupa ila ni muhimu, pesa ulindwa na kudhibitiwa....

Sent using Jamii Forums mobile app

Mganga tena [emoji3][emoji3]
 
Kufanya biashara kanda ya ziwa inabd uwe mchawi Tu , watu ni arrogant Sana kule na ni washirikina to the maximum.... Hata jiwe naye ana mindset za hvyo hvyo , uganga na ushirikina ni first attempt katika kusolve matatizo.....na hii inatokana na poor education background
Brainwashed creature..uganga ndio asili ya mwafrika

#MaendeleoHayanaChama
 
Hela nyingi sana hio usikurupuke biashara usiyoijua iko kama biashara ya kuku..wakiamua kukuangusha ni dakika.
fanya utafiti wa biashara ambayo unauwezo wa kuiendesha.
 
Back
Top Bottom