Nina mtaji wa Milioni 35 nataka kufanya biashara Kariakoo

Uzi mzuri ila haya mambo ya vilemba bwana🤣🤣
Nilichogundua kilemba ndio changamoto inayofanya biashara iwe ya faida nyingi maana haiwi na watu wengi sana watakaoshusha bei ya bidhaa,inavyoonekana ukitoboa kwenye kilemba basi umeshatoboa kibiashara.😃
 
Kingine ni vile watu hawana uaminifu vinginevyo mnaungana wawili au watatu, mnakuza mtaji mwisho wa siku kila mtu anaweza kuwa na fremu yake.
 
Kyusa street karibu na madogo wanachoma kuku wa kienyeji jioni!!? Nitakuja kukuungisha nikija pande hizo.
 
Tafuta kiwanja jenga vyumba vya kupanga. Hapo utakuwa umelinda hela yako na kisha kusanya unayopata fanyia unachotaka.
 
Hiyo hela yako utaipoteza mkuu ukienda Kkoo. Licha ya kwamba biashara si nzuri hapo lakini huo mtaji utaenda kuchoma. Kwanza kilemba tu hata hiyo 35 yako itapotea. Me nadhan nenda mkoa unaoanza kuchipukia. Ama fanya biashara ingine mtaani
Mkuu kilemba ndo nini?
 
hahahahahah yaani akabet
 
Mkuu nimepitia mawazo ya watu wengi sana hapa ni mazuri, ila wakati mwingine kila mtu anaiona biashara kulingana na upande aliosimama mfano pharmacist kukushauri ufungue pharmacy ni rahisi sanaa ila unaweza kukuta wewe na pharmacy ni giza ( simaanishi kuwa haiwezekani).Ushauri wangu kwako kwanza angalia kile kitu ambacho wew kwa mazingira yako unaweza kukifanya vizuri kabisa then chukua hatua tafuta ''mentor'' mtu atakayekushauri kuhusu hicho unachotaka kufanya halafu usiogope kupoteza muda chukua hata miezi sita ili kujua kwa usahihi unachotaka kufanya, kariakoo sio lazima sana uanze na fremu kubwa kuna vigoli pia laikin hakikisha lazima umpate mentor kabla ya kufanya chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…