Nina mtoto ila nataka kuingia kwenye mahusiano yatayopelekea ndoa. Naeleza vipi kwa mwenza wangu huyu?

Nina mtoto ila nataka kuingia kwenye mahusiano yatayopelekea ndoa. Naeleza vipi kwa mwenza wangu huyu?

Kila mwanaume timamu aliyesoma kichwa cha uzi alizani uzi unamuhusu mwanamke nachomaanisha huu uzi ilibidi umuhusu mwanamke sio mwanaume, umedharirisha wanaume tuombe msamaha.

MWANAUME hawazi, hatakiwi kuwaza wala kuwa na wazo la kuwaza kuhusu suala la yeye kuwa na mtoto anapotaka kuoa na wala halijawai kuwa tatizo toka Dunia iumbe.

Kwa mada hii jamaa yako hana tofauti na Single Mother mpaka pale atapotambua yeye ni mwanaume.
 
Mwanaume hakuna haha ya kujieleza sana!

Oa halafu mtoto atakuja nyumbani baadae!!

Unajieleza Nini hasa!!?

Kwani mtoto Kwa mwanaume anasumbua nani!!?

Oa tu!!
 
Nimesoma comment ila, swali limelenga, mtu mwenye situation hiyo anafanya vipi, kuwa mwanaume sio tatizo. Mwanamke pia ni kiumbe ,hofu ipo kwa mtu yyte yule.
SABABU ZA kutokuwa na mama watoto wake zinawezekana zikawa nyingi sana, ila sisi tuachane na upande huo, tustick hali hiyo wewe kama mwanaume unafanyaje?
Na kama mwwanamke situation hiyo unaipokeaje. Achana na jamaa sijui apigwe viboko, sijui sio mwanaume.
 
Kwa Nini usimfundishe ajiunge jamii forum kama wewe umeshindwa kumshauri!?atakutuma mara ngapi? ,,, Tena mwambie asikuzoee, haiwezekani member mwenzetu anatumika kama jini,kutumwatumwa tuuu bila mpango
 
Habari za jioni wana JF. A true story inayohitaji msaada kutoka kwa rafiki yangu wa karibu, Yeye tayari ana mtoto wa miaka miwili lakini hayupo pamoja na Mama mtoto wake. Sasa yupo kwenye mahusiano ambayo conclusion yake ni Ndoa na ni ndani ya mwaka huu 2024.

Naomba tumshauri, anatakiwa afanye nini kumueleza huyu Mwanamke kwamba tayari yeye ana mtoto wa miaka miwili, ili isilete shida. Huwa inakuaje? Kwa wazoefu.
Ningetamani mawazo ya pande zoote mbili. Na kataa ndoa tutulie.
Usifikirie mengine bali mwambie ukweli ili aamue kuwa nawe au kusitisha mahusiano ya ndoa na wewe. Ni bora ajue kabla kuliko akajua tayari akiwa ndani ya ndoa mkuu, makovu yake ni makubwa na hatakuamini tena.
 
Huo ni uanaume gani sasa hadi kushindwa jambo dogo kama hilo? P.....umbavu zake!
 
Habari za jioni wana JF. A true story inayohitaji msaada kutoka kwa rafiki yangu wa karibu, Yeye tayari ana mtoto wa miaka miwili lakini hayupo pamoja na Mama mtoto wake. Sasa yupo kwenye mahusiano ambayo conclusion yake ni Ndoa na ni ndani ya mwaka huu 2024.

Naomba tumshauri, anatakiwa afanye nini kumueleza huyu Mwanamke kwamba tayari yeye ana mtoto wa miaka miwili, ili isilete shida. Huwa inakuaje? Kwa wazoefu.
Ningetamani mawazo ya pande zoote mbili. Na kataa ndoa tutulie.
Usioe. Mkuuu
 
Back
Top Bottom