Nina mwezi mmoja tu umebaki kabla ya kufunga ndoa. Ushauri wenu tafadhali

Ukishaoa:
1. Endelea kumfanyia 'mke' wako yale uliyokua unamfanyia mkiwa wachumba. Usichoke kisa na maana umeshamweka ndani.

2. Kuwa mume sio kua 'boss', saidia baadhi ya chores za nyumbani kama kujiandalia kahawa, kupiga nguo za familia mzima pasi, kupika kama unaweza.

3. Usitabirike muda wa kurudi nyumbani. Itakunyima uhuru. Leo Rudi saa kumi jioni, kesho saa nne usiku. Itapunguza usumbufu.

4. Usitake mawazo yako yakubalike always. Wala usilazimishe afuate usemacho. Wewe shauri yakiharibika atakuelewa siku nyingine.

5. Ukipata watoto hakikisha unatengeneza bond. Bond ya baba ni ya kutengenezwa ya mama ni asilia!

6. Mambo ya familia yako mf. Wazazi, dada, kaka na mandugu wengine mkeo asijue sana. Wanawake wana wivu!

7. Muhimu kuliko zote pesa za mkeo achana nazo kabisa. Akikupea mwenyewe sawa ila usizipangie budget.

8. Muhimu zaidi nyumba yako ikose vyote ila usishindwe kuprovide chakula. Ile basic ya mara tatu Kwa siku. Sio lazima mikuku ila msosi uwepo.

9. Mpende mkeo.

10. Sikiliza ushauri wa mawifi (dada zako) ila usiufuate. Nao wana wivu!
 
Endesha maisha yako unavyotaka...

Mtu asikutishe.

Ndoa tamu ukiwa na akili kichwani.
 
Ndoa ni kutafuta PESA+ kuzaliana+ kulea watoto wasio wako.

Hayo mengine yaache yajisumbukie ukiyasumbukia utajisumbua mwenyewe.
 
Mume ampende mke wake,na mke amuheshimu mume wake.
 
Mwanamume kamili lazima/sharti upite jandoni.
 
Exactly
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…