Nina miaka 32, elimu bachelor of science economics population and development chuo mzumbe, kwenye uzi huu ntaelezea maono, mipango na sera niliyonayo juu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Watu wengi wananiuliza unawezaje kugombea na wakati una miaka 32 huku katiba ikitaka mtu awe na miaka 40, na wengine wanasema nina ndoto za alinacha, wengine una matatizo ya akili
Jibu ni kwamba hii movement ina-malengo ya mda mrefu nikimaanisha itachukua mda ili itimie sio jambo la leo au kesho na mimi sina uhusiano wowote na chama cha siasa
PROBLEM STATEMENT
Changamoto kubwa inayoikumba Tanzania na nchi nyingi za Afrika ni kama zifuatazo;-
i) Uwepo wa walipa kodi wachache sababu watu wengi wanajihusisha na informal sekta kwa hiyo wengi hawalipi income tax na kodi nyingine.
ii) Kwa sababu kuna walipakodi wachache imepelekea nchi nyingi kuongeza kodi kwenye vyanzo vilevile na hii imepelekea kuumiza wananchi wengi.
iii) Kiwango cha kodi kinachoongezeka hakiendani na ongezeko kubwa la watu na mahitaji yao hivyo kushindwa kwa serekali kupeleka huduma muhimu za kijamii.
iv) Kwa sababu wigo wa kodi ni mdogo imezilazimu nchi nyingi za africa ikiwemo Tanzania kukopa ili waweze ku-finance budget zao na kuleta changamoto nyingine ya ukuaji mkubwa wa madeni.
SULUHISHO
kujenga viwanda vingi
TANZANIA MODERN ECONOMY OUTLOOK
VISION
- To become the largest economy in Africa in term of industrial output, gdp, and ppp
MISSION
- To invest heavily on industrilization as a way of achieving economy supremacy
Kama kisemavyo kichwa cha habari nina nia ya kuwa Rais wa Tanzania, zifuatazo ni njia ntakazotumia kuongeza mapato kupitia viwanda na hatimaye kuondoa umaskini;-
i) Kuzalisha umeme wa megawatts 1,000,000 (gigawatts 1000)
Umeme wa uhakika na bei nafuu ni moja ya msingi muhimu sana wa viwanda, hizi zitachangia kushusha gharama za uzalishaji viwandani.
ii)Kwa miaka 10 serekali itajenga viwanda zaidi ya laki 1 ndio laki moja, na kila kimoja kitaajiri wafanyakazi kiwango cha chini wafanyakazi 500 (wa kiwandani na ofisini) na kuendelea
100,000*500= 50,000,000 (watu million hamsini)
Kutakua na zone saba nchi nzima ambazo zitakua ni kitovu cha viwanda ili kupeleka maendeleo kila mahali ni kama zifuatazo;-
a-Wilaya ya mpanda na uvinza viwanda zaidi ya 20,000
b-Wilaya ya muleba na karagwe viwanda zaidi ya 20,000
c-Wilaya ya kishapu na shinyanga vijijini viwanda zaidi ya 20,000
d-Wilaya ya itigi na manyoni viwanda zaidi ya 20,000
e-Wilaya ya ruangwa na lindi vijijini viwanda zaidi ya 20,000
f-Wilaya ya mwanga na moshi vijijini viwanda zaidi ya 20,000
g-Wilya ya kibaha, chalinze, bagamoyo na mkurunga viwanda zaidi ya 30,000
Kutakua na factories ambazo zinazalisha bidhaa from scratch na sio assembly na vitakuwa ni vya ku-export kwenye soko la dunia
Primary industries
- Steel
- Aluminium
- Leather
- Plastic
- Glass
- Copper cable
- Battery
Secondary industries
- Automobile
- Chipset
- Home appliances
- Smartphones
- Clothes and apparel
- Aeroplane
- Pharmaceutical
Minimum wages itakua sh 10,000 na kuendelea kwa mwezi
NINI KIFANYIKE ILI VIWANDA VIWEZE KUDUMU NA KUTEKA SOKO LA DUNIA
Ntaanzisha government agency itakayovipambania viwanda vilivyopo Tanzania ili viteke soko la dunia, na itakua inafanya kazi zifuatazo;-
- Kutafuta vyanzo vipya vya umeme na kuhakikisha umeme unakua mwingi sana na wa bei nafuu
- Kuhakikisha viwanda vinapata raw material hili jukumu hataachiwa mwenye kiwanda pekee yake
- Kuhakikisha viwanda vinapata machine zinazotumika viwandani hili jukumu hataachiwa mwenye kiwanda pekee yake
- Kuhakikisha viwanda vinapata skilled labour hili jukumu hataachiwa mwenye kiwanda pekee yake
- Kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa Tanzania zinakua na bei ndogo kwenye soko la dunia ili ziuzike
- Kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa Tanzania zinakua na ubora ili ziuzike kwenye soko la dunia
FAIDA ZA VIWANDA LAKI MOJA KWA NCHI YA TANZANIA
a) Serekali itakuwa na uwezo wa kukusanya moja kwa moja usd billion 100 (Tsh trillion 250,000,000,000,000) kutoka kwenye viwanda tu; hapo sijaongelea sektor nyingine ambazo kupitia multiplier zitaguswa na viwanda indirect na zitaongeza pato la nchi
b) Viwanda Vitakuwa vinamilikiwa na familia tofauti tofauti za wazawa (watanzania), kwa gharama kubwa sana serekali itawapigania kwa nguvu zote wazawa kumiliki viwanda lengo ni uchumi kumilikiwa na wazawa na sio wageni
c) Viwanda vitaondoa sekta ambazo sio rasmi (informal sector)kama wamachinga, wauza mitumba bodaboda n.k sababu wataajiriwa kwenye hivyo viwanda zaidi ya laki 1
Njia ya kuwaondoa wamachinga, wauza mitumba, bodaboda, wapiga debe ni kujenga viwanda vingi ili waajiriwe na wawe na uhakika wa pension wanapofikia miaka 60 na zaidi
Sasa hivi watu wanaojihusisha na sekta ambayo sio rasmi hawana pension au akiba yeyote itakayowasaidia pale watakapokua wazee
d) Nchi ikiwa na viwanda zaidi ya laki 1 hizi squatters na slum zitaondoka tu automatical sababu kutakua na hela ya kuziondoa na watu watakua na kazi za uhakika na hii itaenda sambamba na kupanga kisasa nchi nzima kisasa na nyumba na majengo yatakua na mfumo unao-fanana ili miji yetu ipendeze sio kila mtu anajenga jenga namna anavyotaka
e) Kutakua na wigo mkubwa wa walipa kodi sababu watu wengi watakua wanajihusisha na kazi rasmi
f) Miradi yote mikubwa ya ujenzi itajengwa na kampuni za wazawa; najua hawana uzoefu ila serekali itawawezesha wawe na uzoefu kikubwa ni ela kubakia hapa hapa nchini
g) Gharama za kujenga nyumba zitakua chini sana serekali kushirikiana, na sekta binafsi watajenga nyumba na kuwauzia watu wa hali ya chini na kipato cha kati- kipato cha juu watajenga wenyewe
Karibu tuandike historia mpya ya Tanzania nchi itakayokua na uchumi mkubwa Afrika nzima