Nina nia ya kuwa Rais wa Tanzania

Nakuelewa kiasi nikupongeze kwa masomo yako ,kwa umri wako haipaswi kuwa na masomo tena bali uifanye iwe mipango iweke kwenye maandishi isomeke, anza maandalizi kuwa mwanachama wa chama cha siasa kumbuka viongozi wote wa kisiasa ni zao la vyama vya siasa. Hatahivyo napingana na wewe kwenye idadi ya wafanyakazi kwenye kiwanda kimoja idadi hiyo ni kubwa mno kwenye dunia ya sayansi na teknolojia, je umefikiria kuhusu AI? au nafasi ya Robot? ,mengine yote uko vizuri ila nazidi kusisitiza "maono waachie kanisani".
 
Hiyo idadi sio kubwa hata kidogo ni ya kawaida
Kuna factory zina wanafanyakazi elfu 1000 na zaidi

Na kwenye kiwanda kuna wafanyakazi wa kiwandani, wa ofisini, madereva, wafanyausafi, wapishi n.k
 
Kitu ambacho hujui ndani ya vyama vya siasa kuna udikteta huwezi kuwa huru kusema mawazo yako mfano ndani ya ccm hakuna anayethubutu kutangaza nia waziwazi sababu utaonekana unampinga Rais aliyepo

Kwa lugha nyingine mfumo wa vyama vya siasa unaua watu wengi sana wenye ndoto kubwa ndo maana wagombea binafsi wanatakiwa kurusiwa
 
Tanzania itakua na uwezo wa kuzalisha megawatts 1,000,000 (gigawatts 1000) za umeme ambao utatumika viwandani na hii itapelekea Tanzania kzalisha bidhaa nyingi za viwandani kwa bei nafuu
 
Huo umeme wa GW 1000 ndio umeme ambao US anazalisha sasa Kwa mwaka, Tanzania hatuna hata GW 2 kwenye gridi ya Taifa,Kwa nchi kama TZ siku ukisikia tuna GW 10 kwenye gridi ya Taifa ujue tumetoka kundi la third word countries, hauko serious wewe
Kama jambo kwako haliwezekani ni kwako kwangu mimi linawezekana
Nigeria ina GW 22+ na bado ni nchi maskini
 
Doh! Kuanza kuchukua hatua ni kukatishwa tamaa ?

Nadhani kuna tatizo sehemu hasa kwenye uelewa wako, Sasa ndugu unakatishwaje tamaa kirahisi namna hii utaweza kusimama kweli kuwa raisi ?
Kusema kuna watu wanajaribu kunikatisha umeme ndo ukweli wenyewe na haina maana kwamba ntakata tamaa wazo la kiwa Rais hakuna aliyenishauri bali ni uamuzi nilioamua pekee yangu na nina matumaini yatatimia
 
Hakuna mtu asieutamani U Rais, but changamoto ni namna ya kufika pale na kukikalia kile kiti safari ni ngumu na mitihani mingi

Ni Sawa na safari ya Wana Israel jangwani kuitafuta nchi ya ahadi
 
Hakuna mtu asieutamani U Rais, but changamoto ni namna ya kufika pale na kukikalia kile kiti safari ni ngumu na mitihani mingi

Ni Sawa na safari ya Wana Israel jangwani kuitafuta nchi ya ahadi
Mimi siutamani urais bali sipendi tu kuona umaskini uliotamalaki sehemu kubwa ya nchi na naona wanaoongoza wanakosa maono ya kututoa kwenye huu umaskini

Kunautofauti mkubwa sana kati anayetaka kutumikia wananchi na anayetamani uongozi
 
WAMACHINGA
Ni-ukweli usiopingika serekali inawachukulia wamachinga kama mzigo na wasiokua na faida sababu;-
  • hawalipi kodi ya moja kwa moja (direct tax)
  • hawamiliki mashine za EFD
  • hawana leseni za biashara
  • wanapanga biashara mbele za maduka ambayo wanalipa kodi
  • wengine wanapanga barabarani na wengine wanatumika na wafanyabiashara kukwepa kodi
  • Wengi sana ni vijana kwahiyo hii nguvu kazi serekali haifaidiki nayo
  • Hawaweki akiba ya uzeeni kupitia mifuko ya akiba na hatari kama hii itapelekea kua na taifa la wazee wengi maskini

Suluhisho sio kuwafukuza kwa kutumia nguvu bali kuwatafutia kazi za uhakika mbadala., Msimamo wangu kuhusu wamachinga ni kama ufuatao;-
  • wasihamishwe maeneo waliyopo kwa kupelekwa huku au kule au kwenye maeneo mapya wabaki maeneo yale yale waliyopo
  • wafuate taratibu zilizowekwa na uongozi wa wamachinga wa eneo husika, na wafuate sheria ndogo ndogo walizojitungia ili usiwe uwanja wa fujo
  • serekali itapambana kujenga viwanda ambavyo vitawaajiri wamachinga na kuwaondoa katika maeneo waliyopo sasa
 
Hongera kwa kuwa na maono hayo, ingawa ni maono madogo sana kwa nafasi ya Urais. Chukua ushauri wa wadau ili uanzia level za chini upate uzoefu. Rais ni taasisi sio mtu so uzoefu unahitajika sana kwani chanamoto wewe umeona moja tu, kiasi kidogo cha kodi na walipaji wachache wa kodi.
 
Mimi siutamani urais bali sipendi tu kuona umaskini uliotamalaki sehemu kubwa ya nchi na naona wanaoongoza wanakosa maono ya kututoa kwenye huu umaskini

Kunautofauti mkubwa sana kati anayetaka kutumikia wananchi na anayetamani uongozi
Kama hutamani urais, ana na vijana wachache wasaidie kwa ujuzi ulionao ili wajikwamue kiuchumi. Pia Famila, Ukoo, Kijiji/Mtaa, Kata, Tarafa n.k
 
Unachekesha mkuu
 

Minimum wages itakua sh 2300 (0.90usd) kwa saa na kuendelea kwa wafanyakazi wa viwandani

 
Oyaa ukipata usinisahau nafiti wizara yeyote au hata ukinieka office ya rais fresh tuh
 
Kama jambo kwako haliwezekani ni kwako kwangu mimi linawezekana
Nigeria ina GW 22+ na bado ni nchi maskini
Hata GW 1 ya uhakika huna then unaongelea 1000 ambayo ni equivalent na capacity ya richest country in the world today, ndoto nzuri lakini be realistic kidogo, na Nigeria with 22GW ndio richest country in Africa, idea nzuri lakini sounds all talk
 
Hata GW 1 ya uhakika huna then unaongelea 1000 ambayo ni equivalent na capacity ya richest country in the world today, ndoto nzuri lakini be realistic kidogo, na Nigeria with 22GW ndio richest country in Africa, idea nzuri lakini sounds all talk
Kama kuna nchi ina GW 1000 kwanini sisi tushindwe
Mkuu usiyaogope sana maisha as long unachowaza hakijavunja sheria yeyote

Wazungu walichofanikiwa ni kuhakikisha wanatuwekea mipaka mingi sana kwenye fikra zetu mara hiki huwezi, kile huwezi., hapana sisi wafrika tunatakiwa tuwe na guts za kusema tunaweza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…