Malengo yangu ni kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni lini sijui ila naamini ntakua Rais. Jina naitwa Dennis R Yesse miaka 32, elimu bachelor of science in economics chuo mzumbe, kwenye uzi huu kama Rais mtarajiwa ntaelezea maono, mipango na sera niliyonayo juu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
PROBLEM STATEMENT
Changamoto kubwa inayoikumba Tanzania na nchi nyingi za Afrika ni kama zifuatazo;-
i) Uwepo wa walipa kodi wachache sababu watu wengi wanajihusisha na informal sekta kwa hiyo wengi hawalipi income tax na kodi nyingine.
ii) Kwa sababu kuna walipakodi wachache imepelekea nchi nyingi kuongeza kodi kwenye vyanzo vilevile na hii imepelekea kuumiza wananchi wengi.
iii) Kiwango cha kodi kinachoongezeka hakiendani na ongezeko kubwa la watu na mahitaji yao hivyo kushindwa kwa serekali kupeleka huduma muhimu za kijamii.
iv) Kwa sababu wigo wa kodi ni mdogo imezilazimu nchi nyingi za africa ikiwemo Tanzania kukopa ili waweze ku-finance budget zao na kuleta changamoto nyingine ya ukuaji mkubwa wa madeni.
SULUHISHO
- kujenga viwanda zaidi ya 151,000+.
Viwanda vinahitaji miundombinu bila ya kuwa na miundombinu ya viwanda ni vigumu sana kwa nchi za afrika kuwa na viwanda sababu hakuna miundombinu ya viwanda ambayo huvutia waekezaji.
SEREKALI LAZIMA IJENGE MIUNDOMBINU YA VIWANDA HAKUNA NJIA YA MKATO
- Kosa kubwa sana kwa nchi za kiafrika ni kutokujenga na kumiliki miundombinu ya viwanda- ni hatari sana miundombinu ya viwanda kumilikiwa na wageni au waekezaji binafsi hawa ni rahisi sana kuihujumu.
- Si sawa kwa serekali kuandaa tu sera na kukaa ofisini huku wakisubiri waekezaji mambo sio marahisi hivyo muwekezaji unatakiwa umuelezee ni jinsi gani ni nafuu kuzalisha bidhaa Tanzania na sio nchi nyingine kimahesubu na sio kinadharia.
- Nchi za gulf zimefanikiwa sababu miundombinu ya viwanda ya kuzalisha mafuta wanamiliki serekali na sio wageni au watu binafsi.
- Nchi za western viwanda vinazidi kupungua kwa speed kubwa sababu miundombinu ya viwanda waliwaachia sekta binafsi na hata serekali zao zimejaribu kuwapa subsidy ila zimewafaidisha wamiliki wa stock wa hizo kampuni.
Nikiwa rais ntafanya mambo yafuatayo kama sehemu ya kujenga miundombinu ya viwanda- serekali itajenga viwanda vifuatavyo na kuvumiliki
- Kujenga kiwanda kikubwa cha kuchakata bauxite kutoka zambia na congo ambayo itatoa pure aluminium ya bei nafuu zaidi kwenye soko la dunia, watauziwa wawekezaji wa ndani bei yao itakua chini zaidi ya wale wa nje kwa ajili ya kutengeneza bidhaa mbalimbali za aluminium.
- Kujenga kiwanda kikubwa cha kuchakata raw copper kutoka zambia na congo na kuwa pure copper cathode za bei ya chini zaidi kwenye soko la dunia, watauziwa wawekezaji wa ndani bei yao itakua chini wa nje itakua juu kidogo kwa ajili ya kutengeneza bidhaa mbalimbali za copper.
- Kujenga kiwanda kikubwa cha kuchakata iron ore, cooking coal (coke) na limestone na kuwa pig iron za bei ya chini zaidi kwenye soko la dunia, watauziwa wawekezaji wa ndani bei yao itakua chini wa nje itakua juu kidogo kwa ajili ya kutengeneza bidhaa mbalimbali za steel.
- Kujenga kiwanda kikubwa cha kuchakata cotton, wool, na kuwa yarn zenye ubora na bei bei ya chini zaidi kwenye soko la dunia, watauziwa wawekezaji wa ndani bei yao itakua chini wa nje itakua juu kidogo kwa ajili ya kutengeneza fabrics za aina mbalimbali.
- Kujenga kiwanda kikubwa cha kutengeneza silicon wafer zenye ubora wa hali ya juu, na zitakua na bei ya chini zaidi kwenye soko la dunia, watauziwa wawekezaji wa ndani bei yao itakua chini, wa nje itakua juu kidogo kwa ajili ya kutengeneza chips na semiconductor mbalimbali.
- Kutengeneza oil refinery kubwa ya kuchakata crude oil ambayo itazalisha bidhaa mbalimbali watakaouziwa waekezaji kwa ajili ya kuzalisha bidhaa mbalimbali.
- Kutengeneza kiwanda cha kuchakata gold (smelting na refining) kwa bei nafuu sana, na gold yeyote inayozalishwa Tanzania haitashafirishwa kama malighafi tena nje ya nchi kwa ajili ya kufanyiwa smelting na refining.
Ukiwa na miundombinu hiyo saba ni rahisi sana kuvutia wawekezaji na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda
MIRADI ENDELEVU
- kuongeza megawatts za umeme maradufu na huu utakua mradi endelevu
KULINDA MIUNDOMBINU YA VIWANDA
Ni ukweli usipopingika Tanzania na nchi nyingi za kiafrika rushwa ni tatizo kubwa sana na ndo moja ya sababu kubwa sana kwa kuwa maskini mfano kuna nchi yenye mafuta mengi Afrika ila refinery zao zote za oil hazifanyi kazi mpaka anakuja mwekezaji binafsi anajenga refinery na bado wanataka tena kumfanyia fitna
Ntafanya mambo yafuatayo kama jitihada za kulinda msingi wa viwanda Tanzania
- Kuwekeza haswa kwenye tafiti za kuongeza ubora na kupunguza gharama za uzalishaji bidhaa Tanzania
- Rais kutokuchagua majaji wa mahakama kuu ili mahakama kuwa huru kumshughulikia yeyote yule atakayejaribu kukwamisha jitihada za viwanda na kuvunja sheria sahivi.
- Dpp kuchaguliwa na wananchi na sio kuteuliwa na Rais hii itampa uhuru wa kufanya kazi zake bila kuingiliwa. Uchumi wa viwanda unahitaji umakini mkubwa sana., DCI, mkuu wa takukuru, kamishna wa kupambana na dawa za kulevya watakua chini ya ofisi ya DPP.
- Msajili wa vyama vya siasa, mkuu wa tume ya uchaguzi kuchaguliwa na umoja wa vyama vya siasa na sio Rais hii itaepusha kuchaguliwa viongozi ambao wanauwezo mdogo na kuondoa hali ya tume ya uchaguzi kupendelea upande mmoja na hii itaepusha sana vurugu za uchaguzi.