###Huku nimechanganya kiswahili na kingereza ###
A- MAONO
Malengo yangu ni kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni lini sijui ila naamini ntakua Rais. Jina naitwa Dennis R Yesse miaka 32, elimu bachelor of science in economics chuo mzumbe, kwenye uzi huu kama Rais mtarajiwa ntaelezea maono, mipango na sera niliyonayo juu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
B- PROBLEM STATEMENT~
Changamoto kubwa inayoikumba Tanzania na nchi nyingi za Afrika ni kama zifuatazo;-
i) Uwepo wa walipa kodi wachache sababu watu wengi wanajihusisha na informal sekta kwa hiyo wengi hawalipi direct tax mfano hawalipi kabisa income tax.
ii) Kwa sababu kuna walipakodi wachache imepelekea nchi nyingi kuongeza kodi kwenye vyanzo vilevile na hii imepelekea kuumiza walipa kodi waliopo ambao tayari wanalipa kodi kubwa kumbuka watu wengi hawalipi kodi sababu hawafanyi kazi rasmi.
iii) Kiwango cha kodi kinachoongezeka hakiendani na ongezeko kubwa la watu na mahitaji yao hivyo kushindwa kwa serekali ku-finance huduma za maendeleo sababu sehemu kubwa inatumika kwenye recurrent expenditure na bado haitoshi.
iv) Kwa sababu wigo wa kodi ni mdogo imezilazimu nchi nyingi za africa kukopa ili waweze ku-finance budget zao na kuleta changamoto nyingine ya ukuaji mkubwa wa deni la taifa ambayo sehemu kubwa ya budget inatumika kulipa deni na wanajikuta wapo kwenye debt trap.
SWALI KWANINI NCHI NYINGI ZA AFRICA NI MASKINI
Vipaumbele vinavyochukua mda mrefu sana kurudisha fedha iliyowekezwa
Nchi nyingi za Afrika haziwekezi kwa watu bali kwenye miradi isiyokua na connection na kipato cha watu mfano kujenga miji mipya, kujenga treni, majengo marefu ambayo mengi hayajajaa na mbaya zaidi miradi hiyo inatumia hela za kukopa na inapelekea kuongeza deni la taifa, hii miradi inachukua mda mrefu sana kurudisha fedha iliyowekezwa. Nchi za africa zinatakiwa ziwekeze kwa watu kwanza na hiyo miradi mikubwa itajengwa tu bila kuumiza wananchi kwa sababu tabaka la walipa kodi litaongezeka.
Culture of impunity kupelekea kuwa na taasisi za serekali dhaifu
Afrika kuna watu wengi sana wanauhuru wa kufanya jinai yeyote ile na wanauhakika wakutokuchukuliwa hatua yeyote mfano kuna upotevu mkubwa sana wa fedha za umma ila hakuna hatua yeyote wanachukuliwa hii inarudisha nyuma jitihada za kuleta maendeleo.
C- VIWANDA
Uwekezaji wa viwanda unauhusiano mkubwa sana na kipato cha watu kupitiwa kuajiriwa moja kwa moja na kupitia multiplier effects ya viwanda ni kubwa sana. Kumekua na jitihada nyingi za kuanzisha viwanda kwa nchi nyingi za afrika bali zimefeli kwa sababu bado bidhaa nyingi zinakua imported. Viwanda vinahitaji miundombinu bila ya kuwa na miundombinu ya viwanda ni vigumu sana kwa nchi za afrika kuwa na viwanda, sababu hakuna miundombinu ya viwanda ambayo huvutia waekezaji.
C1- SEREKALI LAZIMA IJENGE MIUNDOMBINU YA VIWANDA HAKUNA NJIA YA MKATO
- Kosa kubwa sana kwa nchi za kiafrika ni kutokujenga na kumiliki miundombinu ya viwanda- ni hatari sana miundombinu ya viwanda kumilikiwa na wageni au waekezaji binafsi hawa ni rahisi sana kuihujumu.
- Si sawa kwa serekali kuandaa tu sera na kukaa ofisini huku wakisubiri waekezaji mambo sio marahisi hivyo muwekezaji unatakiwa umuelezee ni jinsi gani ni nafuu kuzalisha bidhaa Tanzania na sio nchi nyingine kimahesubu na sio kinadharia.
- Swala la viwanda afrika limekuwa ni kama slogan tu ya kisiasa wala hamna mikakati yeyote ile ya viwanda tunaamini tukitamka mara kwa mara viwanda basi vitaota kama uyoga
- Nchi za gulf zimefanikiwa sababu miundombinu ya viwanda ya kuzalisha mafuta wanamiliki serekali na sio wageni au watu binafsi.
- Nchi za western viwanda vinazidi kupungua kwa speed kubwa sababu miundombinu ya viwanda waliwaachia sekta binafsi na hata serekali zao zimejaribu kuwapa subsidy ila zimewafaidisha wamiliki wa stock wa hizo kampuni.
C2- TANZANIA INDUSTRIAL MODE-gharama ndogo sana za uzalishaji, ubora mkubwa na bei ndogo sokoni
Changamoto kubwa sana wanayoikumba nchi za magharibi ni model yao ya viwanda walioichagua zamani ya gharama kubwa ya uzalishaji na ubora mkubwa hii imewapa wakati mgumu kwenye soko la bidhaa kutoka mashariki ya mbali ambao gharama ndogo za uzalishaji ubora wa kawaida. Tanzania bidhaa za viwandani zitajikita kwenye kutumia gharama ndogo za uzalishaji, ubora mkubwa, na bei ndogo sokoni
C3- TRADITION INDUSTRIAL FOUNDATION
Tanzania hatukuwahi kuwa na tradition industries mfano aluminium, steel, copper na polymer kwa sababu kiwanda chochote lazima kitumie bidhaa mojawapo sasa kama una import gharama zitaongezeka.
Nikiwa Rais ntafanya mambo yafuatayo kama sehemu ya kujenga miundombinu ya viwanda- serekali itajenga viwanda vifuatavyo na kuvumiliki
- Kujenga kiwanda kikubwa cha kuchakata bauxite kutoka zambia na congo ambayo itatoa pure aluminium ya bei nafuu zaidi kwenye soko la dunia, watauziwa wawekezaji wa ndani bei yao itakua chini zaidi ya wale wa nje kwa ajili ya kutengeneza bidhaa mbalimbali za aluminium.
- Kujenga kiwanda kikubwa cha kuchakata raw copper kutoka zambia na congo na kuwa pure copper cathode za bei ya chini zaidi kwenye soko la dunia, watauziwa wawekezaji wa ndani bei yao itakua chini wa nje itakua juu kidogo kwa ajili ya kutengeneza bidhaa mbalimbali za copper.
- Kujenga kiwanda kikubwa cha kuchakata iron ore, cooking coal (coke) na limestone na kuwa pig iron za bei ya chini zaidi kwenye soko la dunia, watauziwa wawekezaji wa ndani bei yao itakua chini wa nje itakua juu kidogo kwa ajili ya kutengeneza bidhaa mbalimbali za steel.
- Kujenga kiwanda kikubwa cha kuchakata cotton, wool, na kuwa yarn zenye ubora na bei bei ya chini zaidi kwenye soko la dunia, watauziwa wawekezaji wa ndani bei yao itakua chini wa nje itakua juu kidogo kwa ajili ya kutengeneza fabrics za aina mbalimbali.
- Kujenga kiwanda kikubwa cha kutengeneza silicon wafer zenye ubora wa hali ya juu, na zitakua na bei ya chini zaidi kwenye soko la dunia, watauziwa wawekezaji wa ndani bei yao itakua chini, wa nje itakua juu kidogo kwa ajili ya kutengeneza chips na semiconductor mbalimbali.
- Kutengeneza oil refinery kubwa ya kuchakata crude oil ambayo itazalisha bidhaa mbalimbali watakaouziwa waekezaji kwa ajili ya kuzalisha bidhaa mbalimbali.
- Kutengeneza kiwanda cha kuchakata gold (smelting na refining) kwa bei nafuu sana, na gold yeyote inayozalishwa Tanzania haitashafirishwa kama malighafi tena nje ya nchi kwa ajili ya kufanyiwa smelting na refining.
- Kuwekeza kwenye vocational hasa tool engineering hii itasaidia kuzalisha bidhaa za bei ya chini na zenye ubora
Ukiwa na miundombinu hiyo saba ni rahisi sana kuvutia wawekezaji na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda
D- MIRADI ENDELEVU
- kuongeza megawatts za umeme maradufu na huu utakua mradi endelevu
- Kupima nchi nzima na kuhakikisha kila ujenzi unafuata mipango miji na majengo ya aina mbalimbali yatafuata uniformity ili miji na nchi ipendeze sio kama sahivi kila mtu anajijengea na kufuata ramani yake
E- KULINDA MIUNDOMBINU YA VIWANDA
Uchumi wa viwanda unahitaji uwepo wa mambo yafuatayo ili viweze kudumu.
- Kuwekeza haswa kwenye tafiti za kuongeza ubora na kupunguza gharama za uzalishaji bidhaa Tanzania
- Rais kutokuchagua majaji wa mahakama kuu ili mahakama kuwa huru kumshughulikia yeyote yule atakayejaribu kukwamisha jitihada za viwanda na kuvunja sheria sahivi.
- Dpp kuchaguliwa na wananchi na sio kuteuliwa na Rais hii itampa uhuru wa kufanya kazi zake bila kuingiliwa. DPP atachagua wasaidizi wake kwenye kila mkoa na wilaya ambao watakua ni DCI, mkuu wa takukuru, kamishna wa kupambana na dawa za kulevya watakua chini ya ofisi ya DPP., Uchumi wa viwanda unahitaji umakini mkubwa sana.
- Msajili wa vyama vya siasa, mkuu wa tume ya uchaguzi kuchaguliwa na umoja wa vyama vya siasa na sio Rais hii itaepusha kuchaguliwa viongozi ambao wanauwezo mdogo na kuondoa hali ya tume ya uchaguzi kupendelea upande mmoja na hii itaepusha sana vurugu za uchaguzi.
Michango yenu ni muhimu sana karibuni