Nina nia ya kuwa Rais wa Tanzania

una uhakika gani utawanyoosha, au wewe ndio watakunyoosha
 
mbona na vya watu binafsi vinakufa, lake soap na gardenia vilikufa, tanalec nacho kilikufa, swala, sahara foundry, vyote vilikufa, biashara ni suala mtambuka sio fallacial argumentum tu
 
hii dunia ina wenyewe, ukitaka kujua fuatilia habari za dangote refinary kule nigeria
 
Kamwe siwezi tumia njia za JPM nchi inatakiwa iwe na taasisi imara na sio strongman
 
mbona na vya watu binafsi vinakufa, lake soap na gardenia vilikufa, tanalec nacho kilikufa, swala, sahara foundry, vyote vilikufa, biashara ni suala mtambuka sio fallacial argumentum tu
Changamoto yako umejikita kwenye kukosoa anzisha uzi ili ueleze unachojua na misamamo yako
Usitafute upande mrahisi wa kukosoa
 
Kamwe siwezi tumia njia za JPM nchi inatakiwa iwe na taasisi imara na sio strongman
Ili ujenge taasisi imara inabidi wewe kwanza uwe imara hadi zisimame. Ni swala la muda na kuhakikisha mafisadi hawaziingilii. Mfano kujenga jeshi imara la polisi inabidi ufukuze mafisadi wote na kuweka watu wenye uadilifu na maadili. Pia inabidi uwalipe misharaha ya kutosha. Inabidi ufanye hivyo kwenye Taasisi nyingine kama Magereza, Salama, Takururu, Tamisemi ni kazi inayohitaji mkono wa chuma.
 
Huihitaji mkono wa chuma bali unahitaji taasisi imara na dhamira ya ukweli
 
Unazijengaje taasisi imara bila kuwa mtu imara usiyecheka na wapigaji wa mali za umma. You are a bit naive.
Unahitaji akili na sio nguvu ndo maana busara busara/hekima ina nguvu sana ukitumia nguvu au hisia utafeli
 
Unahitaji akili na sio nguvu ndo maana busara busara/hekima ina nguvu sana ukitumia nguvu au hisia utafeli
Una safari ndefu sana kujua jinsi taasisi imara, nchi imara zinavyoundwa. Fuatilia historia ya USA, Russia, China, Singapore, South Korea, Japan, UK, na nyingine nyingi nchi zlizoendelea, Taasisi zao zilijengwa na watu wa aina gani?
 
Una safari ndefu sana kujua jinsi taasisi imara, nchi imara zinavyoundwa. Fuatilia historia ya USA, Russia, China, Singapore, South Korea, Japan, UK, na nyingine nyingi nchi zlizoendelea, Taasisi zao zilijengwa na watu wa aina gani?
Ahsante kwa maoni yako
 
Dpp kuchaguliwa na wananchi na sio kuteuliwa na Rais hii itampa uhuru wa kufanya kazi zake bila kuingiliwa. Uchumi wa viwanda unahitaji umakini mkubwa sana., DCI, mkuu wa takukuru, kamishna wa kupambana na dawa za kulevya watakua chini ya ofisi ya DPP.
 
Ahsante kwa maoni yako
Wewe ni mchanga sana kwenye historiaya dunia.
Napoleon akikomesha utawala wa kifalme Ufaraansa. Abraham Lincoln alipambana kuondoa utumwa, Cromwell alipambana kuondoa ufalme usiojali wengine Uingereza. Nchi nyingine fanya research unahitaji dictator mzalendo kama JPM ili nchi ifanikiwe sio dicteta kama Samia kuuza nchi, hana uchungu na taifa la Tanzania.
 
Siamini kwenye udictactor naamini kwenye misingi ifuatayo
  • Rais kutokuchagua majaji wa mahakama kuu ili mahakama kuwa huru kumshughulikia yeyote yule atakayejaribu kukwamisha jitihada za viwanda na kuvunja sheria sahivi.
  • Dpp kuchaguliwa na wananchi na sio kuteuliwa na Rais hii itampa uhuru wa kufanya kazi zake bila kuingiliwa. DPP atachagua wasaidizi wake kwenye kila mkoa na wilaya ambao watakua ni DCI, mkuu wa takukuru, kamishna wa kupambana na dawa za kulevya watakua chini ya ofisi ya DPP., Uchumi wa viwanda unahitaji umakini mkubwa sana.
  • Msajili wa vyama vya siasa, mkuu wa tume ya uchaguzi kuchaguliwa na umoja wa vyama vya siasa na sio Rais hii itaepusha kuchaguliwa viongozi ambao wanauwezo mdogo na kuondoa hali ya tume ya uchaguzi kupendelea upande mmoja na hii itaepusha sana vurugu za uchaguzi
Ahsante kwa kushiriki
 
Kama umesoma na bado hujagundua elimu yetu ni fake,na ndio maana hujaiongelea hata kidogo,basi hufai hata kufikiriwa kuwa diwani.

Nchi hii inatakiwa kuwa na Rais atakayefikri tofauti sana na sio debate za form two unazotuletea.

Kwanza unatakiwa kuhakikisha kuna chakula cha kutosha,pili kuvunja kabisa mfumo wa elimu uliopo na kuanza mfumo mpya usiofanana kabisa na wa nchi za kimagharibi.

Tatu vijana wote wasio na ajira maalum au kujiajiri na kulipa kodi, wakamatwe wapelekwe mashambani wakalime.Kazi za uchawa marufuku.Vituo vya redio vinatakiwa viwe vichache na usipokuwa na div one form six au GPA ya 4 ya chuo huruhusiwi kutangaza.Wasanii wa muziki wote wapewe mashamba na hakuna kuimba matusi.
Lazima akili za watu zilishwe maneno bora sio ujinga ulio kwenye bongofleva
 
Mpaka leo unaamini kilimo ndo kitaitoa nchi hii unasafari ndefu sana kifikra
Modern agriculture hakihitaji group kubwa la watu kama unavyoamini
Ahsante kwa kushiriki
 
Unaongelea mihimili mitatu. Mahakama, Serikali, bunge. Unnaona zinafanya kazi?
 
Unaongelea mihimili mitatu. Mahakama, Serikali, bunge. Unnaona zinafanya kazi?
Hakuna dikteta anayeamin kwenye mihimili mitatu ya serekali
Madilteta wote wanaamini kwenye one man show
Wewe unaamini kwenye madikteta mimi naamini kwenye taasisi imara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…