Nina safari nje ya Dar kwa siku tatu, ningependa kupark gari JNIA ili nikirudi niichukue


Na riba yake pia unalipa sio?
 
Oysterbay Police Pana jengo jipya na la kisasa na parking nzuri nenda kaongee na Mkuu wa pale uone itakaaje kaaje Maana usalama upo wa kutosha ,
Note ukikutana na kamanda Kingai mkwepe ana njaa za Hapa na pale ataanza kukudalalia Ili utoe Cha juu na mjua yule mpuuzie
(Joke Kwa Kingai)
Ila ndio hivyo Mkuu!
 
PUMA ENERGY.
 
Hela yako tu..
Lakini kwann usiliache kwako?
 
Ingawa mi Naona rahis ni kuipeleka Kwa ndugu, jamaa au Rafik na uipaki hapo kisha ukimuachia hata Elf 10 ya wese, parking au ya dharura. Kama una taka akufate siku ya kurudi pia anaweza kukufata airport na kukupeleka hom.
 
Benki wanachukuaga gari au kadi?
 
Shida yake apaki karibu na airport, asafiri, ili akirudi asipate tabu ya usafiri.

Siyo gari hana pakuiacha, kwa dar yote.
 
Nenda TAMESA pale jirani na Mkuki House kama unawnda Coca cola ya zamani, ulinzi ni 💯 na Bei ni Tsh 5,000/ per day, unaandikisha unaacha funguo, kurudi kuja kuchukua wanakupa Gate pass ya kutoke,
 
Tafuta mwanaume mmoja wa dar..mpe apigie misele mwambie akupe 50000 kwa siku..×3=150000 .

Mafuta juu yake...

ila akisepa nalo mazima au akilibomoa usiseme mimi ndo nimekushauri
Huu ushauri mbona kama wa kiboya sana?
 
Habari wakuu, kuna yeyote anayefahamu utaratibu na gharama za kufuata ili kupata long term parking katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Nina safari nje ya Dar kwa siku tatu, na ningependa kupark gari pale ili nikirudi niichukue.
Mkuu pale kawaida ni 2k per hour.
Hvyo kwa siku ni 2000 × 24 = 48k
Kwa hizo siku 3 ni 48,000 × 3

But huwa wanatoa discount sijajua wanaangalia vigezo gani maana November mwaka jana nliondoka asubuhi saa10 nikapark gari pale, na nikarudi saa1 usiku lakini nlilipia 15k labda ufanye kuulizia...
 
Wanachukua gari au kadi ya gari?
 
Njoo upaki kwangu. Kuna nafasi kubwa sana, hata mabasi 10 yanaingia bila shida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…