Youth champion
Member
- Feb 12, 2020
- 72
- 87
Siwezi kuplan safari wakati sina pesa pesa ipo ya kutosha tuHakuna elimu inayohitajika. Unahitajika tu kuwa na pesa namaanisha mkono mtupu haulambwi shekhe
Siku ya kwanza ukifika, toka nje ya nyumba uliyofikia kati ya saa saba na 11 aubuhi uwaambi “Good morning Americans”.
sawa MkuuKaribu Big [emoji519] ila unakuja kipindi cha baridi ndio inaanza anza. Wakati mzuri ni Kuanzia May mpaka September hali ya hewa kama bongo. Utamaduni tofauti kuna mambo yatakushangaza sana achana nayo angalia mambo yako. Pia ni mojawapo ya mji ghali duniani. Karibu sana
Ebhana kule ni nchi yenye kila aina ya Uchafu hapa Duniani.
Maana kila biashara uijuayo wewee kule ndiko mahala pake ni wewe tu...!
Sasa kama ni hivyo usije jihusisha na Magenge ya ulaghaifu na ukatengeneza connection utapotea.
Kubwa kuliko lote ni tabia ya Ubwabwa ndo usiseme usipo kuwa makini watakupa pesa taam wakufokoe mtaro.
Bro watch out.
Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Umenikumbusha miaka Zaid ya mitano nyuma nilipoenda marekani kwa mara ya kwanza, nilienda kwa mwaliko wa shirika na nilikua peke yangu kutoka tanzania..bas nikaingia kwenye ndege sijui chochote na kwenye gar hata sioni mbongo mwenzangu yaani niko peke yangu dah! Lakini sikua na wasiwasi sana zaid ya furaha tu! Kimbembe ni tulifika sehem tunataka kubadilisha ndege asee mpaka leo huwa nachekaaa akili ikanijia niulize wale polis mle ndani.
Sasa jaman ugeni huu..naenda kumuuliza na Kiingereza changu cha kuunga nimesahau sasa ntasema marekan? Aah polis hajui marekan kimoyo moyo nasema sasa hili jina la marekani lilitokea wap? Sasa niseme amerika? Amerika si bara hatonielewa aah nikaachana naye nikaanza kufata watu..baahat nzuri kulikua na muda mrefu kabla ya kubadili ndege ndiyo nikaenda kusoma kwenye zile board zao nikaona napotakiwa kwenda..kiufup ni kama vile kulikua tu na roho mtakatifu ananiongoza.
Mpaka baadae tunashuka airpot ya D.C ndiyo nikakutana na mbongo tukasalimiana sasa pale ndiyo tunatoka nje ya uwanja na vimbwa vyao vile vinatunusa dah! Nikachukua tax hadi hotelini lakini jina la marekan lilinisumbua sana kwakwel...tulikaa wiki mbili siku ya kurudi tena niko peke yangu uwanjani mle kuna sehem ya kupanda zile tren za ndani heehee nasikiliza tren imetaja kituo nikadandia chap..kutika ndan aah mbona tena kama siyo hii nikashuka fasta kufika chini tu nikauliza nikaambiea ndiyo hiyohiyo zena chap nikarukia kwa mlango mwingine jaman siku ile nilitetemeka uwiiii..ngoja niishie hapa lakin mkuu we nenda tu utafika tu wala hutopotea.
Ndio nihadithie nduguSitasahau nilivyo potea mitaa ya bevele hills ikabidi nimuulize bibi wa kizungu.
Ahsante sanaUS baby, karibu Maryland huku, by the way karibu US cha msingi hakikisha documents zako za kusafiria zipo poa, wale jamaa wako very serious katika watu kuingia nchini mwao.
Kuhusu safari ni ndefu kidogo almost masaa 26 kwa ethiopia airlines yaani kutoka dar mpka addis ababa to Washington to New York safari ndefu kidogo hivyo jiandae na kuvimba miguu.
Mimi huwa ni muoga sana hivyo tukishapewa zile blanket huwa nalala hadi muda wa kula nikiamshwa maana ile safari ya kuvuka atlantic ocean sio mchezo.
Ukifika hakikisha unakuwa na hela tu nzuri ya kutumia hapa na pale, by the way US ni pazuri sana independeza ukae hata mwezi