Nina shilingi milioni 64, niwekeze kwenye biashara gani kati ya hizi?

Nina shilingi milioni 64, niwekeze kwenye biashara gani kati ya hizi?

Wazo lako la kwanza ni zuri ongeza na nguruwe a.k.a kitimoto utanufaika sana kwani soko lao ni kubwa sana
 
Njoo korogwe tanga, wekeza kwenye mashamba ya mkonge...... Utanishukuru baadae

Kabisa kaka Wazo zuri na Ema zangu 60 nishamaliza kulisafisha Alhamdulilah nasubiri Mvua ziishe nikatandaze Mkonge inshallah
 
Habari wakuu.

Natumaini mnaendelea vizuri na maandalizi ya sikukuu.

Bila kuwachosha sana, nimeweza ku save jumla ya shilingi milioni 64 hadi sasa, kiasi hiki nimeweza kukisave kuanzia mwezi April mwaka huu kutoka kwenye mshahara wangu. Nipo mkoa wa Dodoma.

So far, nimefikiria kuwekeza katika mojawapo ya mambo yafuatayo:

  1. Ninunue eneo la shamba kubwa maeneo ya Dodoma nje ya mji au Dodoma vijijini kisha nianzishe kama ranchi hivi ya ufugaji wa mbuzi.

    Nimefikiria mbuzi kwa sababu kwa utafiti wangu wa muda mfupi nimeona kuwa mbuzi hawana complications nyingi kulinganisha na wanyama wengine wa kufuga, na pia kuna fursa zaidi kwa mbuzi nchini, na demand ambayo haijawa satisified.

    Lengo la hii ni baadae niweze kuwa na kiwanda kabisa cha kuchinja na kuprocess nyama ya mbuzi, na kuweza hata kuuza ndani na nje ya nchi products za nyama ya mbuzi.

  2. Nifungue park kwa ajili ya michezo ya watoto kwa Dodoma. Moja ya gaps ambazo nimeziona Dodoma ni kukosekana kwa eneo zuri la maana kwa ajili ya michezo ya watoto na watu kupumzika pia.

    Hapa nafikiria ninunue eneo Dodoma then nilitengeneze vizuri na kuweka michezo ya watoto (indoor na outdoor) ya kutosha, pamoja na kutengeneza garden nzuri ya kuvutia kwa ajili ya watu na familia zao kupumzika na kupigia picha.

    Kwa nje kwenye ukuta nawaza pia kuwe na frame kadhaa ambazo nitakodisha kwa watu waweke maduka ya vyakula, vinywaji, na vitu vya watoto.

  3. Nifungue kiwanda cha maji ya kunywa yale ya kwenye dispenser kwa ajili ya matumizi ya majumbani na maofisini. Nimeona gap pia hapa kwa sababu makampuni yaliyopo hapa Dodoma kwa hii huduma hayatoshelezi mahitaji kwa kiasi kikubwa, mara nyingi sana unakuta yanapotea sokoni kwa muda fulani (no consistency of supply).

  4. Ninunue kiwanja saizi ya kati maeneo ambayo sasa hivi ndo yanajengeka (eg Ilazo, NALA) halafu nipige vyumba vya low-cost (behewa style), niweke hapo vyumba kadhaa, then nipangishe nile kodi kila mwezi hata 50K kwa kila room. Baadae kadri ninavyopata mpunga zaidi, niongeze idadi ya vyumba zaidi na zaidi.

    Wenye uzoefu wa biashara na ideas na mnaoifahamu Dodoma, niambieni hapo nianze na ipi kati ya hizo kwa mtaji huu nilionao (milioni 64), au hata idea nyingine ambayo sijaitaja hapo juu.

    Mimi maisha yangu yote nimeajiriwa tu hadi sasa (nina umri wa miaka 35). Sijawahi kufanya buashara hata ya kuingiza shs 500. Nimeona ni bora pia niangalie upande huu wa business pia maana siwezi ajiriwa milele, na pia kama mjuavyo hizi ajira zetu, leo ipo kesho haipo hasa huku private sector.

    Natanguliza shukrani.
Ya mbuzi ndo Anza nayo,kumbuka pia kibanda Cha mfugaji hapo,mawazo Yako ni mazuri yote,Mimi nipo Dodoma kwa muda mrefu Hilo la sehemu ya watoto ni muhimu pia!
 
64 milioni ni pesa nyingi, ila utakapoiingiza kwenye uwekezaji itaonekana ndogo. Ukiwekeza kwenye lodge kama ulivyoshauriwa hiyo pesa itaisha kabla ya kumaliza. Lodge yenye vyumba 12 hiyo pesa haitoshi. Ni kuanzia 100+

Kwenye magari, Fuso hizi kwa sasa zinazolipa sio zile single. Kuna zile double dif au almaarufu tandam hiyo pesa haitoshi. Tandamu moja kwa sasa ni zaidi 100+

Hardware hapa ndio naweza kukushauri. Maana kwa sasa ujenzi kwa mkoa wa dodoma umeshika kasi. Hiyo pesa unaweza kuanza nayo. Na kwa kuwa umeweza kuseve 64 mln kwa mwaka 1. Basi mshahara wako unakupa nafasi ya banki kukuamini na kukukopesha. Angalao uanze na 100mln.

Anza na Mabati geji 28, 30,32, nondo size zote cement za makampuni yote. Dsm Tanga na Dangote. misumari size zote. Mbao na mazagazaga mengine. Baada ya mwaka m1 huo mtaji utakuwa umedouble kama sio mara mbili yake.

Hakuna sekta inayoinua kama sekta ya ujenzi.
Vipi kuhusu spear parts ikoje hii
 
Jenga Lodge!!! Hiyo hela inatosha Sana, Tena hata lodge mbili, ulifanya hivyo matunda utayaona mapema sana.
Watu mna masihara sana, milioni 64 ijenge standard lodge mbili kweli??? Kwa uzoefu wangu hata Moja standard haijengi, acheni utani...
 
mi niko mwanza nataka ninaujuzi wa biashara ya viazi ulaya vya jumla kutoa kenya nyombe na bukoba lakin mtaji ndio sina. NAOMBENI KUFAAMISHWA SEHEMU YA KUKOPA MILIONI 10 au 15 alaf ntalejesha kwa liba Naombeni msahada hapo je ntakopa wapi???? au kama mtu anamtaji aje tufanye maana inafaida saana kwa maelezo zaidi nichek 0767845301
 
Fanya biashara hii hutojutia maisha yako milele Geita MPUNGA vijijini una 70000 junia njoo chukua junia za kutosha subiri a mwezi wa 12 karibu na Christmas mchele Kilo 2500-2800 we kila junia ukipewa 150000 utakuwa na faida ya 80000 kwa kila junia hahahaaaa njoo uone matajiri vijijini japo sio matajiri Sana ila ni matajiri
 
Kafungue biashara ya accesories kariakoo... uuze vifaa vya kielektroniki kijana, hasa simu na kompyuta. Tumia mtaji wa 10m-15m, lipa na kodi ya mwaka... wekeza nguvu na mawazo kwenye biashara. Utaona jinsi watoto wa mjini wanatoboaga wanaitwa wanga, mashoga na wauza unga.

Ila uweke na kabajeti ka uganga kidogo.
Ahahaha, nimecheka hapo kwenye "uganga", biashara ni noma aiseh[emoji23].
 
mi niko mwanza nataka ninaujuzi wa biashara ya viazi ulaya vya jumla kutoa kenya nyombe na bukoba lakin mtaji ndio sina. NAOMBENI KUFAAMISHWA SEHEMU YA KUKOPA MILIONI 10 au 15 alaf ntalejesha kwa liba Naombeni msahada hapo je ntakopa wapi???? au kama mtu anamtaji aje tufanye maana inafaida saana kwa maelezo zaidi nichek 0767845301
Mwanza unapanga kufanyia baishara soko gani?
 
Back
Top Bottom