Nina shilingi milioni 64, niwekeze kwenye biashara gani kati ya hizi?

Nina shilingi milioni 64, niwekeze kwenye biashara gani kati ya hizi?

Kuna eneo la kutosha nje ya mji Chiwondo karibu na Segu - NALA litakufaa kwa ajili ya ufugaji. Pia mahali nilipo hakuna Hardware ya mbao ni takribani vijiji vitatu vinafuata hiyo huduma Dodoma mjini.. ikitokea umeweka hardware ya mbao umeula, umeme upo maji yapo usafiri sio tabu.
 
Na 2 na 4 ni nzuri.
1.zinalinda mtaji
2.Wateja ni uhakika
Kama huna changamoto za usimamiaji fanya no 2 kwanza then mapato fanya no 4.
Kama mda wa kusimamia ni tatizo jenga za kupangisha zitakuokoa wakati wa shida.
Wakati wa shida ni upi
1.Kamba kukatika kazini
2.kusimamishwq Kazi
3.kufukuzwa
4.ulemavu nk

Ushauri kama una pesa fanya maendeleo haraka sana kabla ujaingia kwenye ndoa, kufanikiwa kwenye ndoa utegemea na utulivu wa mke
Asante sana mkuu.
Uzuri nilishaoa mapema sana mkuu, ndoa yangu ina miaka 10 hadi sasa.
 
Kuna eneo la kutosha nje ya mji Chiwondo karibu na Segu - NALA litakufaa kwa ajili ya ufugaji. Pia mahali nilipo hakuna Hardware ya mbao ni takribani vijiji vitatu vinafuata hiyo huduma Dodoma mjini.. ikitokea umeweka hardware ya mbao umeula, umeme upo maji yapo usafiri sio tabu.
Asante sana mkuu, nitafuatilia
 
Kipindi tuna hangaika na maisha mimi na jamaa yangu tukaandika wazo la kuwa na kituo cha mafuta! Eti tukopeshwe na bank, halafu tuwe tunanunua mafuta TOTAL! Masharti tuliyokutana nayo tulitamani kulia! Yaani ni zaidi ya 500M ndiyo unaweza miliki kituo cha mafuta, na hapo umeweka pump ngapi?? Tuliishia kunywa maji kwenye spenser za ofisi za TOTAL nakurudi getho kulala
Atleast mlikua na ndoto kubwa,tena hamkuishia kwenye makaratasi mkaenda hadi kwenye ofisi za TOTAL!!.kwa hili nawapongeza sana

kilichowakwamisha ni capital,endeleeni kupambani big up sana
 
Una mshahara mkubwa kwa mwez na hujawah fanya biashara kabisa, kwako naona ukijenga na kupangisha itakufaa zaidi… real estate ni biashara nzuri pia unaweza jenga nyumba moja ukaipasua kazi ukafanya viself 2 room 2 each kodi huku wanakula had 300k kwa mwezi kwa self ya vyumba 2 sebule jiko choo

Dodoma bado demand ya nyumba za kupanga ni kubwa…biashara nyingine zitahitaji usimamiz wa karibu sana na ukiwa mtu wa kuwa busy na hujawah fanya biashara itakusumbua sana kusimamisha hizo biashara
 
Mkuu Mapambano bado yanaendelea

1. COCO =Company Own, Company! Operate!
2. CODO =Company Own, Dealer Operate!
3. DODO =Dealer Operate,Dealer Own!

Hapo kwenye CODO ndiyo tuliambiwa ili uweze walau kuwa na kituo! Uwe na Capital si chini ya 500M, hiyo 500M ni kwa ajiri yakununua mafuta tu! Sasa hapo hujajenga kituo mtaji wake si utakua mkubwa zaidia ya hapo!
Yeah ukaangalia kwa kawaida 500m ni parefu


Kwahyo hapo kwenye CODO,nyie mnakua mnanunua mafuta kutoka TOTAL na kituo cha mafuta kinakua na Brand ya TOTAL au Brand yenu
 
Asante kwa wazo.
64m napata Fuso la kuanzia? Na je, Fuso moja inaweza nipa return nzuri ya kuonekana? Unaweza nipa insights zaidi?
We usijaribu hii biashara tafadhari...

Jenga nyumba ya wapangaji au fuga mbuzi maana bei zake zinapaa kila siku
 
Mkuu twende kisomi!

Petral Station inatakiwa kua na

1. Car Wash
2. Super market
3. Tanks zakuweka chini
4. Paa la kituo
5. Vibali kutoka NEMC, wakala wa vipimo
6. Na mambo mengine mengi
Hapana sio lazima hivo vingine viwepo Kama supermarket car wash maana Kuna leseni za Aina mbili Petro station na filling station au service station hiyo Petro station ndo inainclude sijui car wash supermarket.mgahawa nakadhalika

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Okay wewe una filling station sasa na sio petrol station! Which is mara nyingi unajenga vijijini na target kubwa yako ni boda boda

Na unaweza kua na pump moja tu!
Mkuu mim nna petrol station unaweza kuwa leseni ya petrol station Ila we ukawa na vitu muhimu tu kwanza ofisi canopy generator pumpu hayo mange ukayaweka baadae sjui ya super market car wash sababu unaeneo kubwa ndo maana unaona mjini vituo vya makampuni makubwa kituo kipo kwenye eneo dogo tu yehutoa huduma ya mafuta tu

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom