Nina soko Uingereza la maharage haya natafuta patner mwenye mtaji

Mkuu umemaliza kila kitu wahindi wanatumia Letter of Credit sio cash kama sisi huku.
 
Yote hayo tulielezwa mkuu...
Kuna wahindi na wafanyabiashara wengine wa kibongo siku hizi hawahangaiki na cash wanatumia Letter of Credit kwa benki zao kubwa na Wana export na import mizigo mpaka ya billions of money.

Sema sisi waswahili benki zetu haziweka nguvu kuwasapoti wamatumbi kwenye International Trade. Sisi packages zetu ni zile za weka,toa,junior account na promotion za kutumia visa card ushinde kirikuu.
 
Walitifugisha sungura wakidai mkojo wake unalipa mpaka leo hajatokea mnunuzi.
 
Nitakucheki
 
Kuna ombwe sana aise
 
Haha
pole sana kaka😀😀😂
 
Duh eka 400 na bado zikawa ndogo, si mchezo, sasa sisi wenye vihekari 15-20 wala tusithubutu..

Maana nilitaka nitandaze haragwe la PINTO mwanzo mwisho ni haragwe tu, kama ni hivyo ni aheri niendele kuvuna nazi zangu tu.
 
Vyakula vinatakiwa SA ni vile mambo ya vibali kuchukua Tanzania kwa ajili ya Export vipo ghari hata zile karanga za Malawi zilizokua zinakuja huku sasa hivi wanaenda kuuza wenyewe bondeni hapo Johannesburg yamejaa maduka ya chakula kutoka Malawi,Zambia na Msumbiji mkiweza nendeni huko soko lipo wazi Asali,dagaa,maharage,mchele na parachichi...unaanza kwa kupeleka kidogo unavyopata uzoefu na soko unachukua mzigo wa kutosha ila Asali mpaka upate kibali ukipeleka kienyeji wanakupokonya mzigo...
 
Mkuu upo mkoa gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…