kidonto
JF-Expert Member
- Jan 5, 2014
- 1,961
- 2,918
Shalom!
Nataka tu kujifunza na kuongeza Imani yangu!
Nimekua nikishuhudia Watu wengi wakifunguliwa Makanisani kwa Macho yangu!
Nimeshuhudia Baadhi ya watu wakifunguliwa kwa namna tofauti, katika kisa kimoja, mwanaume wa Makamo alikua Mgonjwa akiamini Kalogwa, alihangaika kutafuta Tiba toka kwa Mganga mmoja mpaka mwingine, Ndugu za yule Mgonjwa walikua hawaamini Nguvu ya Yesu Kristo katika Uponyaji, ila mmoja baada ya mwingine miongoni mwa Wanafamilia wakaanza kupokea Uponyaji, kwa mujibu wa Ushuhuda wa Ndugu na Mgonjwa, hata siku hiyo Jumapili wao wanajiandaa kwenda Kanisani, Ndugu yao anajiandaa kwenda kwa Mganga!
Ndugu wakamkamata kwa Nguvu na kwenda nae Kanisani, baada ya maombi akapona, sasa wakati anatoa Ushuhuda anasema, Nanukuu..
"Sikua hata na Mpango wa kuja hapa, nilikua nataka kwenda kwa Mganga coz alinambia nirudi leo nikachukue Dawa, mimi sikujui wewe Mchungaji wala simwamini Yesu, ila nashangaa tu baada ya maombi, nimejikuta Mwili kama unapigwa Shoti ya Umeme, nikaanguka, baada ya kuinuka, sasa najiona Mzima"
Mwisho wa kunukuu.
Nimekuwa nikibarikiwa sana na Mafundisho na Maombi ya Mtumishi mmoja Mkubwa ambaye hayupo Tanzania, huwa nafatilia Ibada zake live Youtube kila Jumapili.
Kuna siku akiwa anaendelea na Maombi, baadaye akaanza kusema Mungu anamwambia amuombee mtu mmoja mwenye shida ambaye hayupo Kanisa, akasema, Nanukuu.....
"Mungu ananambia nimuombee Mtu mmoja anaitwa Flani, anatatizo hili na hili, hapa naongea amevaa hivi na hivi, anakunywa Chai na ananitizama sasa hivi"
Mwisho wa kunukuu
basi akaanza kumuombea, baadaye Mchungaji akasema Mungu amemfungua kule alipo.
Dakika chache Misa haijaisha tangazo linatolewa Kanisani kwamba yule mtu ambaye sio member wa kanisa na Pastor aliyemuombea kabla amekuja Kanisani.
Anaingia Mwanaume wa Makamo, kashika Kikombe Mkononi, Kikombe, aina ya nguo mpaka Soksi vyote Pastor alivizungumzia wakati akimwelezea huyo mtu, akapewa nafasi ya kuongea akasema hivi, nanukuu....
"Mimi nina miaka sasa naumwa, nasumbuliwa na Maumivu Mgongoni kwa ndani upande mmoja, nimeacha kazi nimekua mtu wa kulala na kukaa ndani, mke kaniacha, leo wakati nakunywa Chai, nikwasha TV wakati natafuta Channel ya kuangalia nikajikuta nimewasha hii Channel, nasikia Pastor anataja jina langu na kuzungumza kuhusu Mimi na Ugonjwa wangu.... Mimi sio Mkristu, sina hata jina la Kikristo, mimi nimekulia katika jamii ambapo ikitokea shida tunaenda kwa Sangoma, nashangaa leo Pastor kaomba baada ya Muda nikaona nimekua Mzima, baada ya kufatilia location nikaamua nije hapa Kumuona huyu Pastor aliyeniombea"
Mwisho wa kunukuhu.
Kama Wakristo tunafundishwa juu ya Imani, kwamba Mungu hu deal na watu wenye Imani, wanaoamini 200%
Na tunaambiwa ukikosa Imani hakuna Jambo ambalo Mungu atahusika na wewe....!
Swali.
Kwa nini baadhi ya Watu Mungu anawafungua wakiwa hawana Imani kwake kabisa, yani hawana hata 10% ya Imani, na wengine wanaambiwa wakuze Imani yao ili Mungu aweze kuwasikia na kuwafungua.....!???
NB.
Kama hii mada unaona haikuhusu pita zako kimya kimya!