Sijatulia vizuri ila jioni nitakujibu kwa vifungu vya Biblia. Nifahamuvyo, Uponyaji wa kimungu umejengwa katika imani za namna 3.
1. Imani ya Muombeaji. Wewe unayeombea mtu una imani ya namna gani mbele za Mungu. Lazaro alilala mauti ila Yesu alimfufua. Petro na Yohana walimuombea yule Mlemavu pale kwenye lango la Hekalu katika kitabu cha Matendo ya Mitume. Kilichofanyika pale ni uponyaji wa kimungu pitia imani waliyokuwa nayo akina Petro.
2. Imani ya muombewaji. Yesu alikuwa anawauliza sana wale aliokuwa anataka waombea kama unaamini. Inawezekana wewe muombeaji una imani ya kuhamisha milima ila muombewaji hana imani hata chembe. Na hii ndio maana hata wakati Yesu akiwa duniani hakuwa anajisumbukia kufuata wagonjwa mahospitalini au majumbani mwao.
3. Imani ya Tatu ni ya Mungu mwenyewe hapa namaana ni yeye kutaka kujitwalia utukufu. Sisi Wakristo imani hii ya Mungu tumepewa sisi pitia mamlaka ya Yesu kristo.
Bali kwa ushuhuda wako, binafsi ni mkristo na nimeokoka maswali TAG ila katika kitu ambacho siamini na binafsi nakwenda nacho taratibu ni shuhuda za Mungu kaniambia moja mbili tatu. Ukiangalia shuhuda hizi nyingi hazina msingi wa Neno la Mungu. Leo unatabiri eti Mungu kanionesha nimuombee mtu kavaa nguo fulani, soksi fulani n.k then huyo mtu anakuja kanisani kwa kuvaa kama ulivyosema. Hilo halina msingi wa Kibiblia.
Naweza hitimisha kuwa, Matendo ya uponyaji na miujiza ni Karama za Roho Mtakatifu naye humpa amtakaye lakini Karama hizi zina Lengo moja tu. Kulijenga kanisa la Yesu na sio Kujijengea heshima binafsi ya Nabii/Mtumishi kama ilivyo sasa.