Nina tatizo gani mimi? Napenda sana kuwa peke yangu

Nina tatizo gani mimi? Napenda sana kuwa peke yangu

Ni kipindi katika makuzi kitapita, ila uamuzi utakaochukua sasa ndio utakuwa haiba yako
Asante kaka mshana jr. Ushauri kuna post yako nimewahi kusoma nahisi inaongelea sana hizi stages. Niko kwenye my late 20s. Nakaribia 30 yrs. Asante mkuu. Naomba hii hali ipite.
 
nilishafikiria kuleta uzi km huu;niko chuo kimoja hapa dar na yote uliyoandika ndo natak yawe hivyo!
sema mm muda mwingi huwa nasoma vitu vingi sana na kutafakari xn mpk najikuta natak kuwa mm t!
Aisee kumbe tuko wengi. Mimi nasoma masters hapa morogoro. Nikiwa alone nasoma sana vitabu pia. Sipendi wageni, sipendi group discusions ila naenda ili kumaintain collegiality tu. Uzuri ni kwamba nafanya vizur darasani kwa kipindi chote cha masomo yangu.
 
Utakua na pepo aina ya surbiani au markatta, nenda ukaombewe na km ulishawah weka nadhiri zinazohusu damu zifute kbs
Asante kwa ushauri. Siamini katika mapepo wala sijawahi kuweka nadhiri au maagano yoyote katika maisha yangu. Nitaenda kuombewa anyway. Thank you
 
Mimi pia Nina tatizo la kutaka kuwa peke angu mda Mwingi. Kwa mfano nimekutana na mtu ninayemfahamu njiani.na akataka kuongozana nami. Nipo tayari kumdanganya kuna sehemu napitia ili aondoke tu. Au rafiki yangu aniambie nakuja kwako nipo tayari kumwambia sipo. Ili tu nikae mwenyewe.mpaka najishangaaga
 
Yaa ni tatizo mkuu mimi pia ninalo hilo ila linatokana na sababu mbalimbali kwa upande wangu mimi tatizo hilo Lillian mwaka 2003 hadi leo ndo nimekua adicted kabisa.

Kikubwa kilichosababisha ni kukosa upendo katika familia yangi haswa upande wa baba wakati kipindi hicho nipo secondari kidato cha pili ni wakati ambao nilikua nahtaji sapoti ya baba kimasomo kuanzia,pesa,hadi ushauri lakin hakujali.

Nilikosa michango nikawa nashinda ndani tu shule siendi akatokea mwalimu wangu mmoja wa msingi akanilipia michango nikaendelea na shule toka kipindi hicho niliumia moyo na sikujua maana ya upendo.

Niliajiriwa mwka2012-lakin kazini nilikuwa man alone na baada ya miaka miwili nikaenda chuo saiv nipo chuoni mwaka wa tatu ila sipendi mazoea na mtu kiviile. Nina mchumba ambae kiukweli siwezi kaaa nae zaid ya masaa matatu tutagombana akiaanza vijistory vyake vya ooo mara hivi kiukweli sina upendo tena hata furaha ya maisha sina.

Makuzi ya utoto yasipoenda vizuri ni hatari sana. Hauko peke yako mkuu!
 
Ingekua uko hivyo toka utotoni si mbaya, ila kwa sababu ni new character jaribu kuwacheki akina Chriss Mauki
 
Mimi pia Nina tatizo la kutaka kuwa peke angu mda Mwingi. Kwa mfano nimekutana na mtu ninayemfahamu njiani.na akataka kuongozana nami. Nipo tayari kumdanganya kuna sehemu napitia ili aondoke tu. Au rafiki yangu aniambie nakuja kwako nipo tayari kumwambia sipo. Ili tu nikae mwenyewe.mpaka najishangaaga
Aisee tupeane pole tu. Hili ndilo linalonikuta sasa
 
Una psychotic depression coz inaonesha ulikuwa too much stressed kwa muda mrefu, jitahd kujichanganya ili ucje kufikia hatua mbaya zaid. Talk to them your problems....
Thank you so much. Noted
 
yaa ni tatizo mkuu mimi pia ninalo hilo ila linatokana na sababu mbalimbali kwa upande wangu mimi tatizo hilo Lillian mwaka 2003 hadi leo ndo nimekua adicted kabisa kikubwa kilichosababisha ni
kukosa upendo katika familia yangi haswa upande wa baba wakati kipindi hicho nipo secondari kidato cha pili ni wakati ambao nilikua nahtaji sapoti ya baba kimasomo kuanzia,pesa,hadi ushauri lakin hakujali nilkosa michango nikawa nashinda ndani tu shulr siendi akatokea mwalimu wangu mmoja wa msingi akanilipia michango nikaendelea na shule toka kipindi hicho niliumia moyo na sikujua maana ya upendo, niliajiriwa mwka2012-lakin kazin nilikua man alone na baada ya miaka miwili nikaenda chuo saiv nipo chuoni mwaka wa tatu ila sipendi mazoea na mtu kiviile nina mchumba ambae kiukweli siwezi kaaa nae zaid ya masaa matatu tutagombana akiaanza vijistory vyake vya ooo mara hivi kiukweli sina upendo tena hata furaha ya maisha sina, makuzi ya utoto yasipoenda viziri ni hatari sana. huko peke yako mkuu
Duh! Kuna mambo naanza kuyagundua baada ya hii historia yako. Nahisi nitahitaji kumuona psychological counsellor. Makuzi yana mchango mkubwa sana katika maisha yetu. Asante na pole sana mkuu
 
Nikudadavulie kidogo...

Upweke sio kutokua na watu waliokuzunguka bali ni kutokua karibu na wewe...

Huo sio ipweke ni hali yako inayokupa furaha maana..maana furaha jipe mwenyewe usisubiri kupewa sababu ukipewa utakua umefurahishwa na utakua hujafurahi...
 
Congrats for being an INTROVERT..

Hilo sio tatizo unless limesababishwa na kitu kama family problems au loneliness..

Kuwa introvert sio kuwa lonely.. ni kupenda kuwa alone.. and you enjoy it so much unaishia kuchukia social gatherings..

Welcome to the group guys..
 
Back
Top Bottom