Nina Tshs. 300,000, Naweza kuifanyia nini ili mpaka July niwe nimepata ada ya Tshs. 1,114,400?

Kwanza pole sana kaka mkubwa, katika maisha iyo ni changamoto mojawapo ambayo itakuafanya akili izidi kukomaa katika kujipanga kimaisha.
Tukirejea katika swala lako mi ningekushauri ufanye biashara ya kukodisha baiskeli kama mazingira uliyopo hakuna msongamano wa vyombo vya moto.

NAMAANISHA;
Kwa mfano ungekua unaishi mikoa ambayo kuna tatizo la usafiri au hakuna msongamano wa vyombo vya moto, ningekushauri kwa hizo laki 3 ununue baiskeli za kawaida za shilingi elfu 60. Ambapo katika laki tatu utapata baiskeli 5 kwaajili ya kukodisha.
TANGA- BAISKELI 500/= Kwa saa moja
so 5 x 500 = 2,500/= kwa saa moja.
chukulia umekodisha kwa masaa 8
2,500 X 8 = 20,000 /DAY
Fanya kazi week end pumzika
20000 x 26 =52,0,000/= / month
may-july miezi 2 kama chuo kina funguliwa mwanzo mwa mwezi may. ila kama mwishoni inamaana ni miezi 3
520,000 x 3 =1,560,000/=

NADHANI ADA IMESHAPATIKANA HAPO NA PESA YA KUANZIA MAISHA.

MTAZAMO:

Huu ni mfano tuu wa kitu unachoweza kufanya ili uweze kupata kile unachohitaji, ndugu yangu unaweza ukalitafakari hili wazo kisha ukalirudisha katika uhalisia wa eneo unaloishi kwa kuangalia wakazi wanamahitaji gani muhimu ambayo kwao ni shida, hapo ndipo utapata wazo linaloweza kukukwamua na pia likawa endelevu hata kama utakua upo chuo lakini bado utapata pesa ndogo ndogo za kununulia sabuni na materials nyingine.

nadhani umenielewa ndugu.
ASANTE
 

ukuchaguliwa kujiunga na shule za serikali maana uko ada ni sh 70000 tu
 
ucjali nipe mm kama laki mbili tu,huku kwetu naweza kuifanyia kazi na ukapata hiyo, wahi maana nataka niingize shambani, kwan upo wapi?
 

You're genius,...I like it!
 

Nina imani amekuelewa mkuu!
 
Kaka IZAMA kwanza nikupe pole kwa hiyo situation! Hata hivyo mimi nakusisitiza kuufikiria Zaidi ushauri wa ndugu ajam ally hapo juu! Mungu akusaidie!
 
Last edited by a moderator:
nenda serikalin...yaan advance kapige pcb...soma kwa bidii..ukifaulu mkopo utapata 100% ...pesa haizalishwa simple kias hicho
 
nenda serikalin...yaan advance kapige pcb...soma kwa bidii..ukifaulu mkopo utapata 100% ...pesa haizalishwa simple kias hicho

Nilipomaliza form 4 nilipta div 2 point 20 nikafaulu kwenda Azania boys Dar es Salaam. Nikaanza kusoma form 5 PCB. Kilichonishinda ni ada na michango mbalimbali nikawa natolewa nje wakati wa mitihani mikubwa inayorekodiwa. Kwa sababu ya hayo nikashindwa kuendelea. O'level aliyenilipia ada ni kaka yangu ambaye alifariki 2009 mwaka mmoja kabla ya kumaliza form 4. 2013 nikarudi kuomba nafasi tena baada ya kupata mdhamini lakini mwalimu mkuu alinifukuza akaniambia niende mtaani nikatafute maisha . Ndio maana nataka nipitie diploma . Kilichonikwamisha mpaka sasa ni pesa tu maana nimefatilia nafasi zipo. Mambo yako hivyo.
 
UPDATES;

Nilipomaliza form 4 nilipata DIV 2 POINT 20. Nikafaulu kwenda Azania boys Dar es Salaam. Nikaanza kusoma form 5 PCB. Kilichonishinda ni ada na michango mbalimbali nikawa natolewa nje wakati wa mitihani mikubwa inayorekodiwa NECTA. Kwa sababu ya hayo nikashindwa kuendelea. O'level aliyenilipia ada ni kaka yangu ambaye alifariki 2009 mwaka mmoja kabla ya kumaliza form 4. 2013 nikarudi kuomba nafasi tena baada ya kupata mdhamini ambaye baadae aliondoka nchini lakini mwalimu mkuu alinifukuza akaniambia niende mtaani nikatafute maisha . Ndio maana nataka nipitie diploma . Kilichonikwamisha mpaka sasa ni pesa tu maana nimefatilia nafasi zipoMWAKA HUU. Mambo yako hivyo.
 
Nenda makanisani ukajielezee kama ulivyojielezea hapa...utapata msaada.

Mkuu kwa nini unashauri aende kanisani badala ya hapa JF kwenye umati mkubwa? Watanzania majuzi tu mmelipa viingilio mpaka vya milioni kwenye part ya masaa machache tuu pale mlimani city, hebu tumchangieni huyu dogo atimize ndoto zake!
 

Teaching ada yake unaijua? Milioni kasoro si heri apigane aende moja kwa moja Muhas hata kama ni mwakani
 
teaching ada yake ni laki mbili kakak! namaanisha grade A
Mkuu unaishi Sayari gani? Grade A imefutwa,mwisho ilikuwa mwaka jana,na sasa hivi ni diploma tu ambayo ada yake si chini ya laki saba pamoja na michango itafika karibu laki tisa huko.
 
Nifahamishe hapo kwenye media.



Hahahaaa!!

Majibu ya mkato!
 
Pole sana mdogo angu
na mambo mawili ya kukushauli
1. zunguka ktk shule za binafsi za advance na tafuta wamiliki wa shule hizo(wenyenazo) au mameneja ongea nao kwamba wakupe nafasi usome hata mkataba muandike makubaliano ya kuilipa baadaye ni jinsi mtakavyoona. unaweza bahatisha
2.hiyo kozi unayo taka kuchukua ni ipi, hebu fungua web ya heslb ya mikopo kuna kozi za diploma wanatoa mkopo fungua na isome vizuri
yangu ni hayo
 

Asante sana naomba niandikie hiyo link
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…