bab-D
JF-Expert Member
- May 2, 2015
- 1,215
- 322
Asante sana naomba niandikie hiyo link
Nadhani jaribu www.heslb.co.tz ikigoma badae nitakuwa nishaangalia nitakupa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante sana naomba niandikie hiyo link
Ndugu Wanajamvi,,
Poleni na majukumu.
Historia:
Mimi ni kijana umri 25. Nilimaliza kidato cha 4 mwaka 2010. Nikafaulu na kuchaguliwa kujiunga form 5 (2011) Azania boys. Comb: PCB. Mlezi aliyekuwa ananisomesha alifariki 2009 mwaka 1 kabla ya kumaliza o'level.
Kwa neema nikafanikiwa kuanza form 5. Hata hivyo nililazimika kuacha kutokana na kushindwa kulipa ada na michango mbalimbali ya shule. Hata hivyo nikajiapizia kuendelea na masomo.
Update: Hivi karibuni nimejaribu kufuatilia MUHAS nikaambiwa nafasi zipo za kujiunga kama nikitumia cheti cha form 4 kupitia diploma. Kilichonikatisha tamaa ni ada yao yaani Tshs. 1,114,400 kwa mwaka na kozi hiyo itachukua miaka 3. Maana yake 1,114,400 X 3 =3,343,200/- Chuo kinaanza mwezi July 2015
Cheti changu kipo hivi:
2010
Chem B pass
Biology C pass
Physics D pass
Maths C pass
Geo C pass
Kisw C pass
Eng C pass
Hist C pass
Civ C pass
OMBI:
Nina kiasi cha Tshs. 300,000. Je,naweza kuifanyia nini pesa hiyo ili mpaka July niwe nimepata ada ya Tshs. 1,114,400?
Kaka zangu, dada zangu Naomaba msaada wa mawazo. Jinsi gani nisiikose nafasi hii maana bahati hairudi. Asanteni sana kwa utu wenu!!
Wadhamini mnakaribishwa.
Tuwasiliane: izackmanase@gmail.com au
0768577654
Nipo Dar. O'level nimesoma shule inaitwa Dar es Salaam sec sch ipo dar kidongo chekundu karibu na mnazi mmoja
Bro pole sana kumbe hukumaliza shule...mbona hukuapply diploma maalumu...Thabeet aliyekuwa Azania nae aliapply nadhani yupo udom sasa,nakujua vizuri...ulikuwa unapiga kitabu sana
Nitafute nikupe mikeka uwe una beti utapata zaidi ya iyo ela nje nje
dini yako tafadhal waweza kwenda kwa gwajima akufanyie maombi utapata tu wafadhili.
Tuanzie ukoo wao wako wapi mpaka wanashindwa kumsaidia
Nimevutiwa sana na huyu jamaa hasa kwa uwezo, juhudi na kutokukata tamaa.
Binafsi ninaona kuna issue mbili, yaani issue ya kupata Ada mwaka huu lakini issue ya kupata ada kwa mwaka wa
Pili na watatu plus pesa ya kujikimu wakati wote akiwa chuoni. It is a big challenge.
Binafsi ninaweza kukusaidia kwa ushauri madhubuti, lakini kama ukiweza kufafanua haya maswali
1/Kwa sasa unafanya nini kimaisha?
2/Una miliki kitu gani cha thamani?
3/Una familia(mke au mtoto)?
4/Uko karibu kiasi gani na jamii inayokuzunguka(marafiki, jamaa, taasisi za kiimani, kisiasa au kiuchumi)?
5/Umewezaje kupata hizo laki tatu?
6/Una ujuzi gani wa kimaisha?
7/Toka umalize shule mpaka sasa umekuwa unafanya nini?
Kuapply c tatizo ila ada yao c mchezo kama mm najitegemea na kipato kidogo bila mdhamini naishia kutamani tu licha ya kuwa na uwezo kitaaluma. Who are u?
Nimeipata ndani ya mwaka mzima kwa kuuza vitini vya methali na vitendawili mtaani. kitini kimoja Sh. 200