Nina Tshs. 300,000, Naweza kuifanyia nini ili mpaka July niwe nimepata ada ya Tshs. 1,114,400?

Achana na wazo la biashara.

Chapuchapu kimbilia kwenye mashirika ya dini.

Kama mwislam nenda misikitini.
Kama mkristo nenda makanisani.
NAIMANI UTASAIDIWA.matokeo yako yanatia sana moyo.
Go there now! Hata kama huna dini.huko ndiko kimbilio.
Watakupokea,watakusaidia.
Amini utasoma,KWA KUWA UNANIA,BASI HII NDIO NJIA!
 
Ifike kipindi JF ifanye something kubwa zaidi ya kupeana habari kina @maxcence melo wanaweza anzisha program ya kusaidia watu kupitia jf watu wafuatilie kuhusu maisha ya huyu jamaa iandikwe thread sticky kwa ajili ya kumsaidia ipigwe kampeni ya mwezi mmoja ya kumchangia akishapata ada tutabuni njia ya kuwekeza ili huyu jamaa aende shule program maalumu ya kusaidia watu wa aina hii kupitia wafadhili tunaweza hata kuiunda kivipi..??NITARUDI..
 
samahani ndugu hiyo laki tatu ulipataje?tuanzie hapo tafadhari
 
Nipo Dar. O'level nimesoma shule inaitwa Dar es Salaam sec sch ipo dar kidongo chekundu karibu na mnazi mmoja

mkuu umesoma shule niliyosoma o level mimi ila nilimaliza 2009 ngoja ntakutafuta
 
mkuu umesoma shule niliyosoma o level mimi ila nilimaliza 2009 ngoja ntakutafuta

Ulimaliza na kina Bale John, Haika Godifrey au siyo?
Uliwahi kusikia Izack Manase pale school?
 
samahani ndugu hiyo laki tatu ulipataje?tuanzie hapo tafadhari

Nimeipata ndani ya mwaka mzima kwa kuuza vitini vya methali na vitendawili mtaani. kitini kimoja Sh. 200
 
Bro pole sana kumbe hukumaliza shule...mbona hukuapply diploma maalumu...Thabeet aliyekuwa Azania nae aliapply nadhani yupo udom sasa,nakujua vizuri...ulikuwa unapiga kitabu sana
 
Bro pole sana kumbe hukumaliza shule...mbona hukuapply diploma maalumu...Thabeet aliyekuwa Azania nae aliapply nadhani yupo udom sasa,nakujua vizuri...ulikuwa unapiga kitabu sana

Kuapply c tatizo ila ada yao c mchezo kama mm najitegemea na kipato kidogo bila mdhamini naishia kutamani tu licha ya kuwa na uwezo kitaaluma. Who are u?
 
Nimekusoma vizuri sana ila naona kitu kikubwa sana ndani yako Endelea kumtegemea MUNGU na usikate tamaa sababu i see the big picture before you.
 
Nimekusoma vizuri sana ila naona kitu kikubwa sana ndani yako Endelea kumtegemea MUNGU na usikate tamaa sababu i see the big picture before you.

watu wengi hufa kabla ya kutimiza vitu vikubwa vilivyo ndani yao lakini wapo wachache wanaobahatika.
 
What goes around, comes around.... If not today basi hata "kesho"
 
Jaribu kwenye foundation zile kama za flavianamatata foundation. Wanaweza wakakusikiliza.
 
Hapa ni penyewe mi nilikua najiuliza tu kuhusu hiyo laki 3 kapata wapi? msaada utapata ila ni vyema kujua zaidi vitu kama hivyo, kijana tueleze, unafanya nini kwasasa. Usiwe msiri sana kuna vitu lazima uweke wazi ili usaidiwe.
 
Kuapply c tatizo ila ada yao c mchezo kama mm najitegemea na kipato kidogo bila mdhamini naishia kutamani tu licha ya kuwa na uwezo kitaaluma. Who are u?

Walikuwa wanatoa mkopo 100%...sijajua kama mwaka huu watatoa.
 
Nimeipata ndani ya mwaka mzima kwa kuuza vitini vya methali na vitendawili mtaani. kitini kimoja Sh. 200

kwa hapo inakuwa ngumu nilitaka nikwambie ulipopata hiyo pesa uendelee na hichohicho ulichokuwa unafanya
 
Biashara yangu nauza vitini na hiyo pesa nimeipata kwa kum make kidgo kidgo ndani ya mwaka mmoja mkuu.
 
mkuu kama uko dar, kuwa tuu dalali...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…