Nina Tshs. 300,000, Naweza kuifanyia nini ili mpaka July niwe nimepata ada ya Tshs. 1,114,400?


Thanks
 
Ndugu Wanajamvi,,
Poleni na majukumu.

Historia:

Mimi ni kijana umri 25. Nilimaliza kidato cha 4 mwaka 2010. Nikafaulu na kuchaguliwa kujiunga form 5 (2011) Azania boys. Comb: PCB. Mlezi aliyekuwa ananisomesha alifariki 2009 mwaka 1 kabla ya kumaliza o'level.

Kwa neema nikafanikiwa kuanza form 5. Hata hivyo nililazimika kuacha kutokana na kushindwa kulipa ada na michango mbalimbali ya shule. Hata hivyo nikajiapizia kuendelea na masomo.

Update: Hivi karibuni nimejaribu kufuatilia MUHAS nikaambiwa nafasi zipo za kujiunga kama nikitumia cheti cha form 4 kupitia diploma. Kilichonikatisha tamaa ni ada yao yaani Tshs. 1,114,400 kwa mwaka na kozi hiyo itachukua miaka 3. Maana yake 1,114,400 X 3 =3,343,200/- Chuo kinaanza mwezi July 2015

Cheti changu kipo hivi:
2010
Chem B pass
Biology C pass
Physics D pass
Maths C pass
Geo C pass
Kisw C pass
Eng C pass
Hist C pass
Civ C pass

OMBI:
Nina kiasi cha Tshs. 300,000. Je,naweza kuifanyia nini pesa hiyo ili mpaka July niwe nimepata ada ya Tshs. 1,114,400?

Kaka zangu, dada zangu Naomaba msaada wa mawazo. Jinsi gani nisiikose nafasi hii maana bahati hairudi. Asanteni sana kwa utu wenu!!
Wadhamini mnakaribishwa.
Tuwasiliane: izackmanase@gmail.com au
0768577654
 
kijana ulifanikiwa?
 
Jaribu kwenda ofisi ya mbunge wako au halmashauri yako unaweza saidiwa kwani kunakuwa na program za kusaidia MVCs(most vurnalable childrens).
 
Ni kweli ukifanikiwa kuwa dalali,
Ukapangisha nyumba 6 za kawaida za 200,000 utapata 1,200,000 bila kusahau viwanja na magodown.
Kila kitu kina thamani na hasara pia.
 
Mi nakushauri hivi Tafuta Mikoba Ya Kike kwa Bei ya Jumla Jumla halafu tafuta Wateja Katika Maofisi uwatembezee.. Najua Ukipata Mikoba Ya 10000 ukauza 30 utapata hela ya Ada
Ushauri mzur
 
Wewe hebu ngoja kwanza.......hivi ada ya advance kwa shule za sekondari ni bei gani kwa mwaka, maana kwa nikumbukavyo huwa haizidi laki kwa mwaka, na kama wewe ulishafika hadi form five na ukamaliza, na umebakiza only form six, sasa hadi hapo si umeshakula ng'ombe mzima umebakiza mkia tu, ni kwann usitumie hiyo laki tatu kumalizia form six , utakapokuwa ukingojea matokeo ndio uanze na hizo biashara za pwagu na pwaguzi, eeeeein.....eti wewe?!

Kwasababu wewe ufaulu wako ni mzuri na umesoma masomo ya sayansi ambayo kwa nijuavyo huwa madenti wa masomo ya sayansi tena kwa ufaulu kama wako huwa wanapata shavu sana kupata mkopo katika elimu ya chuo kikuu.
Sasa bado najaribu kurejea wazo lako la kuacha hiyo level ulipofikia ili uanze sijui kufanya biashara! Dogo utakosa kila kitu sasa!
Hizo idea waachie watu waliopata divisio four na three za mwisho, na wale waliosoma masomo ya arts, hao uhakika wao wa kutoka katika huu mfumo wa elimu ya tanzania tokea sekondari hadi chuo huwa ni wamashaka sana maana huwa wanapewa kipaunyuma katika kupata mkopo, lakini pia wanaguarantee kubwa ya kutakiwa kukomaa wenyewe huko mbeleni chuoni bila msaada wa serikali kifedha. Sasa wewe sijui umetoka wapi na hizo shobo, nadhani wewe ndio wale watu wanachukua tahadhari hata wakati pasipo na mazingira ya hatari.
So, achana na hizo habari, hako kalaki tatu kako omba uongezewe kidogo rudi shule umalizie, kwa shule ya serikali gharama zipo chini, mihula miwili laki tano tu inatosha.

Sasa ukitaka kuja kutuhadithia majuto endelea na huo mpango wako ambao sijui nani kakushauri maana kwa kuusoma tu inaonyesha umeshawishika ila zio zao la mawazo yako.

SONY Xperia Z5 Premium
 
Hata madongo nayo ni sehemu ya msaada maana yanakutia machungu na kukufanya ufikirie sawa sawa

SONY Xperia Z5 Premium
 
ukuchaguliwa kujiunga na shule za serikali maana uko ada ni sh 70000 tu
Safi wewe sasa nadhani ni miongoni mwa wanajamvi ambao kabla ya kuchangia huwa wanasoma thread kwa umakini kabla hawajacomment chochote....... Big up sana

Sasa, ipo hivi, hata mimi nimehoji hicho kitu huyu bwana anasema amechaguliwa Azania secondary school pale, ambayo ni ya serikali, na kipindi me napiga pale ilikuwa bei haizidi laki moja kwa miula yote miwili, na kama nilisoma vizuri pale juu mleta thread alidai kuwa yeye ameshamalizia form five na amestop kuingia form six sababu amekwama ada.....halafu hapo hapo anasema ana laki tatu na ameshafanya michakato ya kuapply vyuo, sasa wewe unadhani safari ya kutoka cheti hadi, diploma ni kazi ndogo, na hizo fedha utalipa hapo njiani ni bora kumaliza tu hiyo six vizuri piga tu division two au one subiria mkopo serikalini maana watu wa masomo ya pure science mnadekezwa na serikali.

SONY Xperia Z5 Premium
 
nenda serikalin...yaan advance kapige pcb...soma kwa bidii..ukifaulu mkopo utapata 100% ...pesa haizalishwa simple kias hicho
Kabisa.....ingekuwa kirahisi hivyo watu wangekuwa wanakaa tu home

SONY Xperia Z5 Premium
 
Huyo mwalimu mkuu anaitwa nani na akili zake sio nzuri......hana hata haya......yeye mbona hakwenda kutafuta hayo maisha au watoto wake wakatafute hayo maisha ndio aje kufukuza watoto wa wenzake......hayawani mkubwa huyo.

SONY Xperia Z5 Premium
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…