Nina umri wa miaka 30, naishi kwa kaka yangu, watu wananidharau naombeni ushauri

Achana na mambo ya kwenda kupanga wakati huna kipato cha uhakika. Hapohapo kwa kaka yako jichanganye mtaani
Nimeshakaa muda mrefu sana hapa so siwez kuendelea kuishi bora nikajichanganye huko mbele
 
fungua genge la chipsi na nyama choma
 
Riziki ni kitu cha ajabu sana ikifika wakati utashangaa kikubwa muombe mungu na pambana usiforce ukajikuta jera tu.
Kuna jamaa kaja kutajilika akiwa na miaka 52 siku zote alikuwa anaomba mpaka mirungi hapa kenya
 
Nimekuelewa sana mkuu hakika umekuwa ukinipa mawazo mazuri sana nashkuru sana ndugu yangu
 

Pole Sana Mkuu.
Hiyo ni sehemu ya Maisha yako.
Usijilaumu wala kumlaumu yeyote.

Nawe toka ujitafutie vibarua, usikae ndani
 
Riziki ni kitu cha ajabu sana ikifika wakati utashangaa kikubwa muombe mungu na pambana usiforce ukajikuta jera tu.
Kuna jamaa kaja kutajilika akiwa na miaka 52 siku zote alikuwa anaomba mpaka mirungi hapa kenya
Kaka nitapambana kwa kazi za halali tu siwezi kuforce nikaingia kwenye dilo ambazo zitaniletea shida mtaani
 
Kitendo tu Cha kuwa jasiri na kuja hapa jukwaani na kueleza ukweli ukitaka ushauri, maana yake una akili. Unakosa tu miongozo midogo midogo kutoka kwa kaka yako na watu wa karibu. Kifupi hujachelewa, lakin pia usibweteke. Kama umeamua kuwa fundi, kajipendekeze na kajichanganye huko kariakoo kama saidia fundi. Baada ya muda na wewe utakuwa master na kujitegemea mwenyewe. Kuhusu majirani wapuuze. NEVER GIVE UP!!
 
Huenda nae kaka amekuchoka ila ameshindwa kukuambia, tumia tu hako kaelimu ulikopata, jichanganye na watu, uwe na nidhamu ya pesa na mwisho utatoboa.
Nahisi hivyo maana jana nilimwambia kwamba nataka kuhama nilitegemea angeniambia nibaki kwanza nijipange ila ch kushangaza alinijibu tu kwamba yeye awez kunifukuza swala ni mimi mwenyewe kuchukua uamuzi
 
Kakaako ameshamaliza jukumu lake ameshakupa mwangaza, wew endelea kujiongeza mitaani, mafunzo utayapata pia YouTube kwenye channel za wahindi wale jamaa ni noma.
Yeah ofcourse hao jamaa huwa nawatumia sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…