Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Ahsante sana mzee wa nondo nyuzi zako huwa zinani inspire sana
Endelea na bidii ya kutafuta maisha hujachelewa kuna watu wana miaka 50 na mambo bado wapo kwa wazazi au ndugu zao.Habarini za weekend ndugu zangu natumai mmeamka vema sana.
Mimi kuna jambo kidogo linanitatiza nahitaji ushauri wenu.
Ni hivi january ya mwaka 2020 kaka yangu alikuja mkoani basi baada ya kutusalimia aliamua kunichukua na kuja nae hapa dar es Salaam.
Basi baada ya kuja huku alinipeleka kwa mtu mmoja kwa ajili ya kunifunza ufundi wa CCTV ila mambo hayakwenda vizuri, baadae akanipeleka DIT nikajifunza ufundi wa simu.
Ila baadae tukaja gundua pale chuo wanapiga brash tu lakini ufundi kamili unakuwa bado hauko fresh baada ya kumaliza nikaonekana bado sijawa fiti. Ila kwa kipindi chote hicho nipo na bro kapanga chumba kimoja.
Basi nikaamua kutulia kwanza home, kumbuka hapo tayari nishamaliza miaka miwili na sijapiga hatua yoyote na hapo bro kashatumia kama milioni hivi kwa ajili yangu lakini ni kama amna alichokifanya.
Sometime naona kabisa kama anasononeka maana kajitoa sana kwa ajili yangu ili nifanikiwe lakini inaonekana kama hakuna kitu alichokifanya na kila siku lazima aniachie hela ya matumizi.
Sasa hicho kitu kinaniumiza sana moyo hapa tayari nishamaliza miaka mitatu ila bado sina chochote na mbaya zaidi majirani pia wameanza kuniletea dharau.
Kuna kibinti fulani hivi nilikitongoza pia kinanipenda sana, sasa walivyojua wakaanza kumjaza maneno kwamba mimi sina chochote ndio maana miaka yote naishi kwa kakaangu.
Ilimbidi yule binti aniache halafu mbaya zaidi hapo tunapokaa vijana wengi ni umri wangu tayari wameoa na wengine wana magari yao kiukweli naona aibu sana. Hata nivae vizuri bado inaonekana sio chochote, naambiwa nafugwa. Kiukweli hii hali inaniumiza.
Sina pesa ila hapa nawaza kuuza simu yangu niende nikatafute chumba uswahilini huko nilipe hata miezi mitatu halafu nianze kujichanganya kitaa kuliko hizi fedhea nazozipata hapa home.
Note: Umri wangu ni miaka 30, naombeni ushauri ndugu zangu nipo katika msongo mkubwa wa mawazo.
Sawa kaka lakini binafsi kwa wazo langu naona hapa kwa bro nimeshakaa sana so nilikuwa na plan niuze simu yangu niongeze na pesa kidogo niweze kupanga chumba hata kama nitalala chini halafu niingie mtaani kujichanganya nahisi nikichukua hii hatua itanifanya nijitume zaidi kuliko kuendelea kubaki kwa bro maana tayari ntakuwa na majukumu tofaut na sasaMaisha hakuna faida wala hasara.
Yasikupasue kichwa.
Fursa ulizonazo Kwa sasa,
1. Afya.
Hi ndio fursa namba moja. Kuna wenzako magonjwa yanawaandama kila iitwapo leo.
2. Ndugu anayekupenda.
Hii ni fursa ambayo wengi Hawana siku hizi. Wapo Vijana wenzako mamia hunipigia simu
Kunieleza changamoto zaidi ya zako.
Wewe unandugu anayekuthamini.
Itumie fursa hiyo vizuri Kabla naye hajakuchoka, fursa/baraka/nafasi zinatabia ya ku-expire hivyo ni vizuri kuzitumia vizuri.
3. Unakula na sehemu ya kulala.
Fursa ya Ndugu anayekupenda imetengeza fursa hizi mbili.
Ukishakula na kujua pakulala una-advantage ya kufikiria kw Utulivu nini chakufanya tofauti na MTU ambaye hanapakuishi wala pakulala.
Itumie fursa hiyo kujitafuta nawe uweze kujitegemea ili baadaye Kakaako asikuchoke.
4. Wewe ni mwanaume.
Kuzaliwa mwanaume pekee ni fursa kubwa ambayo hata Wanawake wenyewe wanaitamani.
Mwanaume umejaliwa nguvu na Akili.
Wakati Mwanamke amejaliwa tuu Akili nguvu za misuli Hana.
Hii inamaanisha unaouwezo wa kufanya kazi za nguvu au za Akili kujikwamua.
Toka, changamana na watu, ulizia kazi hat za dayworker, kutunza Bustani, au uza matunda, au jifunze kupaka Wanawake kucha,
Ni kazi rahisi zenye mtaji nafuu ambazo ukizifanya hazitakupa kikubwa lakini hautokosa Pesa ya kuvaa, Kula na sehemu ya kuishi. Ambayo hatua hiyo kibongobongo nihatua nzuri na yakumshukuru Mungu.
ahsante kwa kunitia moyo mkuuEndelea na bidii ya kutafuta maisha hujachelewa kuna watu wana miaka 50 na mambo bado wapo kwa wazazi au ndugu zao.
Yes...kila siku nenda pale Lumumba...we sema sifa zote nzuri za CCM kwa kila.mtu...ingia mule ndani...Anza kuimba CCM mbele kwa mbele...mpaka kufikia Saa 10 jioni utakuwa na zaidi ya buku 10, hii ni uhakika ndugu...wahi harakaBaada ya kuchukua kadi nini kinafuata mkuu je nitaweza kuingiza kipato chochote kwa siku
Duuh..kwahiyo ntakuwa naimba tu muda wote au kuna shughuli nyingine ntapewa na kuanzia asubuhi mpaka jion ntakuwa hapo hapo ofisini kwaoYes...kila siku nenda pale Lumumba...we sema sifa zote nzuri za CCM kwa kila.mtu...ingia mule ndani...Anza kuimba CCM mbele kwa mbele...mpaka kufikia Saa 10 jioni utakuwa na zaidi ya buku 10, hii ni uhakika ndugu...wahi haraka
Kama mimi nakushauri hama tafuta getho uswahilini ukaishi. Ongea na kaka yako akulipie chumba kwa miezi 3. Ila kula juu yako.Vipi kaka na wazo langu la kuhama unalizungumziaje?
Sio kweli aisee. Hata yeye mwenyewe mhusika amekiri kuwa hapo mtaani vijana wa rika lake wameshamuacha kimaendeleo.Kiafrika Afrika, miaka 30 kwa mwanaume ndio kwanza kunakucha. Angekuwa mwanamke au mchezaji wa mpira, umri huo tungesema ni Mzee.
Hajachelewa, aende kwa mafundi akajitolee ili aongeze ujuzi
Kama kijijini kwao kupo vizuri kwenye masuala ya kilimo amuombe kaka yake fedha za kwenda kuanzisha miradi ya kilimo. Akitulia kwenye kilimo atatoboa, siku hizi bei za vyakula na mazao mengine zipo juu sana.Kiafrika Afrika, miaka 30 kwa mwanaume ndio kwanza kunakucha. Angekuwa mwanamke au mchezaji wa mpira, umri huo tungesema ni Mzee.
Hajachelewa, aende kwa mafundi akajitolee ili aongeze ujuzi
Huyo kakwambia kiutani, lakini hiyo nayo ni fani inayoingiza pesa.Duuh..kwahiyo ntakuwa naimba tu muda wote au kuna shughuli nyingine ntapewa na kuanzia asubuhi mpaka jion ntakuwa hapo hapo ofisini kwao
Hiyo kazi ya saidia fundi, niliipata mwaka 1997 akili ilinikaa vizuri. Yaani siku ya kwanza nililala kama nimekufa. Ila ilinipa uelekeo mzuri sana kwenye maisha yangu. Hadi sasa namshukuru Mungu mambo yangu sio mabaya sana.Mwaka unaweza usiishe ukajikuta unarudi mkoani, maana kurudi kwa kaka yako utaona aibu. Embu toka tafuta ata kazi za saidia fundi, ukishakuwa na akiba ya kutosha ndo ukapange sasa.
Yani uko busy kutongoza mademu wakati unalishwa na kaka yako badala ya kupambana upate ridhki, eti kupendeza unataka kupendeza 🤣 ili mademu wakuone wakati huna kipato chochote. We mshukuru kaka yako kakushika mkono kakuleta mjini na kakupa hifadhi vitu vingine unatakiwa ujiongeze mwenyewe ata kama ni kubeba zege ili mradi ufikie malengo yako.
Ushauri mzuriElimu ya bongo, huwezi maliza mafunzo alaf ukawa competent.
Kwavile ushapata basic knowledge ya ufundi simu, sogea kariakoo au kwa fundi yoyote wa hayo mambo, muombe uwe Msaidizi wake bila malipo, lengo ikiwa ni kupata ujuzi.
Baada ya hapo mambo yatajiset. Ila ukisema uanze kutongoza madem na huku hujajua unatoboaje, mwaka huu pia utaisha ukiwa kwa kaka yako.
Sahih Sana asikimbie popote abaki hapo Kisha aanze mishe mishe za udereva bodaUtahama huna kipato? Utaishije
Baki hapo mradi hujafukuzwa ila weka juhudi ya kazi
Acha kumtuksna huyu bwana maisha ya mwanadamu Ni hadithiWw ni fakeni sana ulikuwa wapi muda wote ulipokaa kwa kaka yako usijishughulishe, leo ndipo ukauze simu ili uanze maisha na utakufa masikini nyie ndio wale mkibebwa mnajilegeza badala ukaze popoma mkubwa ww
Sawa kaka lakini binafsi kwa wazo langu naona hapa kwa bro nimeshakaa sana so nilikuwa na plan niuze simu yangu niongeze na pesa kidogo niweze kupanga chumba hata kama nitalala chini halafu niingie mtaani kujichanganya nahisi nikichukua hii hatua itanifanya nijitume zaidi kuliko kuendelea kubaki kwa bro maana tayari ntakuwa na majukumu tofaut na sasa