Nina umri wa miaka 30, naishi kwa kaka yangu, watu wananidharau naombeni ushauri

Umeongea mambo yamenigusa kabisa yaani nondo za kufa mtu achukue huu ushauri mzuri mno.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Acha kuwaza mambo ya umri bwana mdogo . Ingia mtaani pambana.

Ukiwa na hela suala la umri halitakubabaisha. hata ukiwa na miaka 80 pesa unayo utaitwa kijana tu
 
Naomba nikuulize huwezi kuanza kupamabana ukiwa hapo kwa kakako mpaka uhame, sasa ukiuza simu tuseme labda shilingi laki 2, kwa sababu mtu wa kufugwa huwezi miliki simu zaidi ya Techno na Infinix. Umeuza laki 2, kodi chumba uswahili labda elfu 30 anataka miezi 6, dalali mwezi mmoja hiyo tayari 190K, Huna godoro, kitanda, jiko, ndoo nk.
 
Ahsante mkuu ni moja ya hatua umenipa wala usijali nimekuelewa sana
 
Kama mimi nakushauri hama tafuta getho uswahilini ukaishi. Ongea na kaka yako akulipie chumba kwa miezi 3. Ila kula juu yako.
Utakuja unishukuru. Kichwa bila kupata moto hakiwezi kufikiri
1. Unataka ule
2. Uvae
3. Ulipie chumba
4. Ununue vitu
Ni kweli mkuu na hichi ndicho nakifikiria kufanya
 
Note: Umri wangu ni miaka 30,
ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu

 
usichague kaz haswa hizi za kutumia nguvu kama kibarua saidia fundi, viwandani, mwaloni kama afya inaruhusu.. pia jumuika na watu wa maana tu ukishinda maskan hupat michongo. Kila kitu kikifeli nenda unakosali kama msikitin/kanisan omba msaada inakuaga zali sometime unapata hata kaz ya kujishkiza kupitia waumini
 
Bro wangu ana daycare nusery school na kaajili watu zaidi ya kumi pia ana school bus kadhaa ila cha kushangaza ni huwa apendi sisi tusogee kazini kwake kwahiyo hata kutuajili awez anaajili watu baki tu
 
Kaka mimi naona nikapange tu bila kuwa na chochote vingine nitavipata huko huko mbele kwa mbele
 
Ni kweli mkuu na hichi ndicho nakifikiria kufanya
Ila kubali kudharauliwa na kukataliwa. Yakitokea mambo kama haya ndiyo muda mzuri
1. Kuongeza bidii katika utafutaji.
2. Usibishane wala kugombana na mtu kwasababu amekudharau hauna kitu. Muoneshe hakuna mtu aujae kesho. Ongeza bidii kwenye utafutaji wa pesa. hakuna mtu mwenye hati miliki wa hela
3. Nunua vitu vya thamani na wekeza
4. Usiwaoneshe watu sasa umepata na unataka kuwakomesha kwakuwa walikudharau. Kuwa bize na mambo yako, wasalimie ila mazoea nao kaa nao mbali
5. Usifuate sana mawazo ya marafiki au kutaka kutumia hela yako ili kuwafurahisha
6. Usiwekeze kwa wanawake, pombe, sigara au starehe yoyote maana hautaendelea. Mwanamke akikuomba 50,000 mpe 5000 au 10,000 hiyo nyingine kanunue kitu ndani hata pazia litakusaidia sana kwanini wanawake hawana shukrani utajitoa sana ila mwisho wa siku utaishia kudharaulika
7. Ukipata pesa usidharau, usiwe na kiburi au kuwa na majivuno maana hivi ni dalili la kuanguka kiuchumi.
8. Saidia wazazi, ukipata chochote mpe usisubiri mpk akuombe.
9. Usiogope kuhusu kesho itakuwaje, utakula nini, utapata hela wapi. Ukiondoa hayo mawazo utaona mambo yanaenda tu na kazi utapata.
Kila la kheri
 
Nimekuelewa kaka ahsante sana
 
Kadithi gani za kipumbavu hadithi za kutoona fursa hvi upo 30 alafu huna hata kitu kinachokuletea hata buku tatu kwa siku alaf unajiona binadamu kabisa umekamilika?
Hakika nimekuwa mpumbavu sana
 
Uliponiudhi ni pale ulipotongoza demu. Kwanini ueiende kumtongoza mwenye banda la simu ufanye bure upate ujuzi badala ya kuficha hela ya nyanya ili uhonge?
Hakika nasikitika mno kwa uamuzi wa kipumbavu nliochukua
 
Kaka mimi nimeamua tu kutoka coz bro pia naona kapendezwa na mimi kutoka kashanibeba sana sasa inatosha
 
Ukweli ndio huu acahana na hizo story za kufurahisha genge
 
Nimekuelewa kaka ahsante sana
 
Ahsante sana kiongozi kwa ushauri mzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…