Nina Virusi vya UKIMWI ila naogopa kumwambia mume wangu maana yeye yupo salama

Asiwe na Hofu wala Kusema Kwamba Atamwambukiza Mumewe maana Mpaka hapo Hawezi Mwambukiza. Kikubwa Atumie Vidonge kwa usahihi Na Akipimwa Iwe Inasoma TND. Hawezi Mwambukiza Sema Tu Akae Mbali na Wambea Na Siri yake Asimwambie Mtu Yeyote yule.
Viral road. Target not detected

Sent from my TECNO B1 using JamiiForums mobile app
 
Mwanachama #001

Tafadhali ficha kitambulisho changu Mheshimiwa.

Najua nimemkosea Mungu na ubinadamu..pole pole napoteza akili yangu...sikutaka yoyote haya...Nina miaka 25, mama na mke , nina VVU lakini mume wangu hajui.
IMEJIDHIHIRISHA KUWA:-
RISK YA KUPATA MAAMBUKIZI YA VVU KWA MWANAUME ALIYETAARIWA NI NDOGO UKILINGANISHA NA MWANAMKE KWA SABABU YA KIMAUMBILE.
 
I like this.
 
NAKUSHAURI: MWAMBIE UKWELI MUME WAKO KAMA KWELI UNAMPENDA VINGINEVYO UTAONGEZA HASIRA KWAKE PALE ATAKAPOTAMBUA UMEMUAMBUKIZA.
NA NAMNA YA KUMWAMBIA NENDA KWA WATAALAMU WA AFYA KWANZA PEKEE YAKO KISHA WEWE NA MUMEO.
 
1. Kwani kabla ya kuoana hamkuhitajika kupima afya zenu?

Maana kwa jinsi unavyoelezea ni kama haujawahi chepuka ukiwa kwa ndoa...

2. Jikaze umueleze mumeo, nina aamini utaeleweka na pengine ukaishi kwa amani na furaha zaidi ya hivi unavyoishi kama digidigi...
 
Pole.

Ila ukweli humuweka mtu huru.
Mwambie ukweli..kwa ajili ya kwake na nafsi yako.

Kabla hujafa haujaumbika bado,
Bado wewe ni wa thamani mno..kujitoa uhai ni dhambi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usiogope hata kidogo, mwambie ukweli ili mpime zaidi inawezekana yeye ni career.Career hata akipimwa kawaida anaonekana ni negative.Ila kila atakayepiga peku anao.Usiogope kwani kama ni kweli yeye hana utakuwa unamlinda na huo ndo upendo.
 
Akija kujua lazima akimbie nyumba na ndio itakua umeharibu zaidi na umekaribisha kifo chako (mgonjwa wa ukimwi mawazo ndio kifo chake).

SEMA NAE ili UOKOE NDOA YAKO.

#YNWA
 
Pole sana sana sana..ongea na Mungu kama ni muombaji. Mungu wetu ni mwaminifu mno,anatuwazia yaliyo mema haijalishi wengine watawaza nini. Kuna wenye cancer inawatafuna kila siku, covid 19 wako wanapumulia mashine. Pengine sisi tunaojiona wazima tunaweza kuondoka duniani kwa ajali au chochote. Mungu ni mwaminifu sana sana lakini ukweli utakuweka huru. DO NOT GIVE UP,hang in there!
 
Mwanachama #001

Tafadhali ficha kitambulisho changu Mheshimiwa.

Najua nimemkosea Mungu na ubinadamu..pole pole napoteza akili yangu...sikutaka yoyote haya...Nina miaka 25, mama na mke , nina VVU lakini mume wangu hajui.
Nina swali, mlipoenda kupima wote pamoja na mtoto, uliwezaje kupata majibu yako bila mumeo kujua?
 
Pole sana kwa hayo unayoyapitia. Kitu cha msingi kwenye ishu hii n kufanya maamuzi magum ya kudisclose(kumwambia uyo mme wako) nje ndan,mwambie kila kitu bila kujali matokeo,hio itakuweka huru zaid kwake/watoto na hata kwenye matumizi ya dawa.

Nn swali moja kwako....matumizi hako ya dawa yalikuaje kwa kipindi chote hiki?? Ulkua unakunywa kwa kujificha?? How comes hajagundua had sasa??
 
Maambukizi mapya ya ukimwi kwa mwaka huu kuanzia mwezi Jan - March ilikuwa ni watu laki tisa na elfu 45 (945,000). Hao ni wale tu waliopima kwa hiari kwa sababu wanaumwa au zingine. Hii ni kwa mjibu wa takwimu.

Enyi wajinga, mtu anaweza kuwa na HIV lakini kila akipimwa isisome. Sababu mojawapo ni kama anatumia dawa na kufanya viral load kuwa very low kiasi kwamba haiwezi kuwa detected.
 
Dada pole Sana,usijisikie vibaya,mshukuru MUNGU kwa kila jambo,siku hizi Ukimwi sio ishu ya kuogopa,watu tunahofia Corona tu ambayo ukiipata leo unaweza kufa ndani ya muda mfupi lkn sio Ukimwi kwasababu Ukimwi unaishi nao kwa muda mrefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…