Ninaamini, leo angelikuwepo Mwl. Nyerere, angekuwa wa kwanza kusema yalikuwa makosa kuwapa Wazanzibari Ardhi ya RAZABA huko Bagamoyo

Hizi zinazojitokeza ni siasa za kutoona mbali.
Watu binafsi kutoka nje, mashirika, taasisi na hata serikali zinamiliki ardhi na majengo ndani ya Tanzania.
Kwa nini hili la Serikali ya Zanzibar ndilo lionekane tatizo zaidi?
Hata hivyo, Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, wazanzibari wengi wanamiliki ardhi Tanganyika na kama utafanyika utafiti rasmi, yawezekana wanamiliki ardhi , majengo na uchumi ambao kwa pamoja vyaweza kuwa vikubwa kuliko Zanzibar yenyewe.
Kama Zanzibar yaweza kutoa Rais wa Tanganyika, kipi cha ajabu katika kumiliki ardhi Bagamoyo?
Inaelekea siasa zetu hazina akili.
 
Ni kuazimwa,sio kupewa.unapewa ardhi kwa kazi maalum ya kipindi maalum,sio unapewa ardhi kwa mda woote.
 
Wewe ungetusaidia kutupa historia ya hiyo ardhi,zanzibar walinunua?,walipewa kama zawadi? Au eneo hilo lilikuwa ni lao toka siku zoote?
 
Sawa Mwalimu aliwapa hiyo ardhi ili wafuge ng'ombe wapate kitoweo huko Zenj, sawa lakini hawakuitumia hiyo Ardhi kwa madhumuni yaliyotarajiwa hivyo kukiuka makubaliano ya matumizi ya Ardhi!! Hawa wazenj wasifikiri kwa vile Samia anatoka huko basi watatutia vidole machoni!! Hawana haki ya kudai hiyo Ardhi ya makurunge kwani ndio wameanza mwisho watadai ukanda wote wa pwani kuwa ni sehemu yao hivyo tusiwaendekeze hata kama rais anatoka kwao!
 
Nakupa pole kwa vile hukujua jambo hil.hati ipo toka mwaka 77 uje ushangae leo,? Mbona kuna maeneo kibao hapa tanzania watu wanayamiliki na wala hawatumii na wapo .nenda amador kule kigambon unatembea ndan ya shamba na gari.bill Gates ana mamilion ya heka kannunua. Sasa shida yako mwandish ni nini?
 
Hiyo ni sawa.
Pia, kama smz hawajaiendeleza hiyo ardhi, rais anayo mamlaka ya kufuta huo umiliki na ku-asign matumizi mengine ya hiyo ardhi.

..hiyo ardhi haijaendelezwa.

..Na miaka ya 80 SMZ ilikumbwa na kashfa kuhusu mradi wa Ranchi ya Makurunge.

..Nadhani kuna fedha zilifujwa na Viongozi na kupelekea mradi huo kufeli.

..Tujiulize kama SMZ wameitumia ardhi hiyo kikamilifu na kulingana na masharti ya kupewa ardhi hiyo.
 
walipewa waitumie tu kwa ajili ya mifugo lkn hawakuitumia . lengo lilikuwa ni kuwarahisishia kupata nyama kirahisi na kusuply zbar, na si kuimega nchi na kuibadili iwe nchi ya zbar NO. kwa kuwa matumizi yaliwashinda, Basi ardhi inabaki kwa wazawa.
 
ardhi inarudi kwa wazawa, hata Kama walipewa hati as long as bagamoyo sio zbar , Basi case closed!! na kwa sheria za zetu ardhi yote ya tz ni Mali ya serikali , serikali inaweza kuamua matumizi ya ardhi yeyote ile , tumeshuhudia watu wakihamishwa maeneo yao pale serikali inapotaka kulitumia eneo kwa miradi yake !!

bagamoyo sio zanzibari .as well as zbar haiwezi kuwa bagamoyo.
 
Wa hovyo vipi unapolinganisha na wazenji wanaoshinda wakiutukana muungano mkuu
 
Nyerere ndiye aliyewapa.
 
Ukiwa kiongozi, simama kama kiongozi, kubali kukosa tamu za stori za watu wa chini yako, ukijishusha sana ili ufaidi stori zao ukawa kama hao unaowasimamia, mwishowe katika stori zao za utani watakushika mpaka tako yako wewe kiongozi kwa sababu umeshakuwa kama wao.
Hivyo watanganyika ni Viongozi, ila sijajua wamefikiriwaje?!
 
Wa hovyo vipi unapolinganisha na wazenji wanaoshinda wakiutukana muungano mkuu
Hata bila ya Muungano, bado tuna mataifa na wawekezaji wa kimataifa wamepewa ardhi ya Tanganyika na sijaona mtu akihoji. Jina "Serikali ya Zanzibar" kuwekeza Makurunge tena kwa ajili ya kufuga tu kuinusuru Zanzibar na uhaba wa.malisho linawatia watu kichefuchefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…