Hizi zinazojitokeza ni siasa za kutoona mbali.Tulivyo wa hovyo, Hasira yetu ni Jina "Serikali ya ZANZIBAR"!
Lakini kama angepewa ardhi hiyo muwekezaji Sheikh Mansoor toka falme za uarabuni au Johnson Johnson kutoka Marekani au Amri Abeid toka Unguja kama ilivyo maeneo mengi tusingetia neno. Bado hatuna ufahamu Kuwa serikari zinaweza kufanya uwekezaji kwenye ardhi ya nchi nyingine ili mradi tu masharti na vigezo vinazingatiwa. Tena tafadhari Zanzibar waliomba ardhi kwa ajili ya uwekezaji uzalishaji mifugo, kuna nchi zinaomba ardhi kwa ajili ya kuhifadhi vifaa vita kumwaga taka hatarishi.
Watu binafsi kutoka nje, mashirika, taasisi na hata serikali zinamiliki ardhi na majengo ndani ya Tanzania.
Kwa nini hili la Serikali ya Zanzibar ndilo lionekane tatizo zaidi?
Hata hivyo, Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, wazanzibari wengi wanamiliki ardhi Tanganyika na kama utafanyika utafiti rasmi, yawezekana wanamiliki ardhi , majengo na uchumi ambao kwa pamoja vyaweza kuwa vikubwa kuliko Zanzibar yenyewe.
Kama Zanzibar yaweza kutoa Rais wa Tanganyika, kipi cha ajabu katika kumiliki ardhi Bagamoyo?
Inaelekea siasa zetu hazina akili.