Ninaamini, leo angelikuwepo Mwl. Nyerere, angekuwa wa kwanza kusema yalikuwa makosa kuwapa Wazanzibari Ardhi ya RAZABA huko Bagamoyo

Ninaamini, leo angelikuwepo Mwl. Nyerere, angekuwa wa kwanza kusema yalikuwa makosa kuwapa Wazanzibari Ardhi ya RAZABA huko Bagamoyo

Tulivyo wa hovyo, Hasira yetu ni Jina "Serikali ya ZANZIBAR"!
Lakini kama angepewa ardhi hiyo muwekezaji Sheikh Mansoor toka falme za uarabuni au Johnson Johnson kutoka Marekani au Amri Abeid toka Unguja kama ilivyo maeneo mengi tusingetia neno. Bado hatuna ufahamu Kuwa serikari zinaweza kufanya uwekezaji kwenye ardhi ya nchi nyingine ili mradi tu masharti na vigezo vinazingatiwa. Tena tafadhari Zanzibar waliomba ardhi kwa ajili ya uwekezaji uzalishaji mifugo, kuna nchi zinaomba ardhi kwa ajili ya kuhifadhi vifaa vita kumwaga taka hatarishi.
Hizi zinazojitokeza ni siasa za kutoona mbali.
Watu binafsi kutoka nje, mashirika, taasisi na hata serikali zinamiliki ardhi na majengo ndani ya Tanzania.
Kwa nini hili la Serikali ya Zanzibar ndilo lionekane tatizo zaidi?
Hata hivyo, Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, wazanzibari wengi wanamiliki ardhi Tanganyika na kama utafanyika utafiti rasmi, yawezekana wanamiliki ardhi , majengo na uchumi ambao kwa pamoja vyaweza kuwa vikubwa kuliko Zanzibar yenyewe.
Kama Zanzibar yaweza kutoa Rais wa Tanganyika, kipi cha ajabu katika kumiliki ardhi Bagamoyo?
Inaelekea siasa zetu hazina akili.
 
Kwani alipokuwa hai alisema nini? Kwa taarifa yako, Zanzibar ilipewa ranch ya makurunge zamani wakati baba wa taifa akiwa bado yuko hai. Lengo lilikuwa ni kuipa smz ardhi ili ifuge ng'ombe na kurahisisha upatikanaji wa nyama huko zenji. Kwa hiyo point ya kusema baba wa taifa angesema sijui nini haina mashiko.
Ni kuazimwa,sio kupewa.unapewa ardhi kwa kazi maalum ya kipindi maalum,sio unapewa ardhi kwa mda woote.
 
Nafikiri ungejifunza kwanza ujue historia ya hilo Eneo na kwanini walipewa wazanzibari, mwalimu JKN ndiye alibariki wazanzibar kupewa Ardhi hiyo.

Hili Eneo limevamiwa na si wananchi wakazi bali ni wahuni ambao walishirikiana na maofisa wa ardhi wakapima viwanja na kuviuza.

Tatizo la ufamizi wa ardhi nchi hii ni kubwa sana, na mbaya kabisa maofisa wa Ardhi wakishirikiana na makampuni ya upimaji wana magenge ya wahuni kazi yao ni kuvamia ardhi na kujimilikisha.
Wewe ungetusaidia kutupa historia ya hiyo ardhi,zanzibar walinunua?,walipewa kama zawadi? Au eneo hilo lilikuwa ni lao toka siku zoote?
 
Kwani alipokuwa hai alisema nini? Kwa taarifa yako, Zanzibar ilipewa ranch ya makurunge zamani wakati baba wa taifa akiwa bado yuko hai. Lengo lilikuwa ni kuipa smz ardhi ili ifuge ng'ombe na kurahisisha upatikanaji wa nyama huko zenji. Kwa hiyo point ya kusema baba wa taifa angesema sijui nini haina mashiko.
Sawa Mwalimu aliwapa hiyo ardhi ili wafuge ng'ombe wapate kitoweo huko Zenj, sawa lakini hawakuitumia hiyo Ardhi kwa madhumuni yaliyotarajiwa hivyo kukiuka makubaliano ya matumizi ya Ardhi!! Hawa wazenj wasifikiri kwa vile Samia anatoka huko basi watatutia vidole machoni!! Hawana haki ya kudai hiyo Ardhi ya makurunge kwani ndio wameanza mwisho watadai ukanda wote wa pwani kuwa ni sehemu yao hivyo tusiwaendekeze hata kama rais anatoka kwao!
 
Nakupa pole kwa vile hukujua jambo hil.hati ipo toka mwaka 77 uje ushangae leo,? Mbona kuna maeneo kibao hapa tanzania watu wanayamiliki na wala hawatumii na wapo .nenda amador kule kigambon unatembea ndan ya shamba na gari.bill Gates ana mamilion ya heka kannunua. Sasa shida yako mwandish ni nini?
 
Hiyo ni sawa.
Pia, kama smz hawajaiendeleza hiyo ardhi, rais anayo mamlaka ya kufuta huo umiliki na ku-asign matumizi mengine ya hiyo ardhi.

..hiyo ardhi haijaendelezwa.

..Na miaka ya 80 SMZ ilikumbwa na kashfa kuhusu mradi wa Ranchi ya Makurunge.

..Nadhani kuna fedha zilifujwa na Viongozi na kupelekea mradi huo kufeli.

..Tujiulize kama SMZ wameitumia ardhi hiyo kikamilifu na kulingana na masharti ya kupewa ardhi hiyo.
 
Kwani alipokuwa hai alisema nini? Kwa taarifa yako, Zanzibar ilipewa ranch ya makurunge zamani wakati baba wa taifa akiwa bado yuko hai. Lengo lilikuwa ni kuipa smz ardhi ili ifuge ng'ombe na kurahisisha upatikanaji wa nyama huko zenji. Kwa hiyo point ya kusema baba wa taifa angesema sijui nini haina mashiko.
walipewa waitumie tu kwa ajili ya mifugo lkn hawakuitumia . lengo lilikuwa ni kuwarahisishia kupata nyama kirahisi na kusuply zbar, na si kuimega nchi na kuibadili iwe nchi ya zbar NO. kwa kuwa matumizi yaliwashinda, Basi ardhi inabaki kwa wazawa.
 
Nakupa pole kwa vile hukujua jambo hil.hati ipo toka mwaka 77 uje ushangae leo,? Mbona kuna maeneo kibao hapa tanzania watu wanayamiliki na wala hawatumii na wapo .nenda amador kule kigambon unatembea ndan ya shamba na gari.bill Gates ana mamilion ya heka kannunua. Sasa shida yako mwandish ni nini?
ardhi inarudi kwa wazawa, hata Kama walipewa hati as long as bagamoyo sio zbar , Basi case closed!! na kwa sheria za zetu ardhi yote ya tz ni Mali ya serikali , serikali inaweza kuamua matumizi ya ardhi yeyote ile , tumeshuhudia watu wakihamishwa maeneo yao pale serikali inapotaka kulitumia eneo kwa miradi yake !!

bagamoyo sio zanzibari .as well as zbar haiwezi kuwa bagamoyo.
 
Tulivyo wa hovyo, Hasira yetu ni Jina "Serikali ya ZANZIBAR"!
Lakini kama angepewa ardhi hiyo muwekezaji Sheikh Mansoor toka falme za uarabuni au Johnson Johnson kutoka Marekani au Amri Abeid toka Unguja kama ilivyo maeneo mengi tusingetia neno. Bado hatuna ufahamu Kuwa serikari zinaweza kufanya uwekezaji kwenye ardhi ya nchi nyingine ili mradi tu masharti na vigezo vinazingatiwa. Tena tafadhari Zanzibar waliomba ardhi kwa ajili ya uwekezaji uzalishaji mifugo, kuna nchi zinaomba ardhi kwa ajili ya kuhifadhi vifaa vita kumwaga taka hatarishi.
Wa hovyo vipi unapolinganisha na wazenji wanaoshinda wakiutukana muungano mkuu
 
Hadi hivi sasa huko Razaba, kuna watu wanaendesha shughuri zao za kila siku, na hii ni kwa sababu, hapakuwa na kufahamu iwapo eneo hilo linamilikiwa na Wazanzibari

Unajiuliza, watu hao sasa wahamie wapi

Kwamba nchi iliyo na watu milioni 59+ igawe aridhi yake kwa nchi yenye watu milioni 1+ ???

Nchi ambayo inabeba madeni mengi kutoka huko, kuyalipa bila kujali, deni la mabilioni ya pesa yaliyotokana na malimbikizo ya umeme tumefuta, lakini bado tunaogeshwa matusi na hawaridhiki na wema wetu!

Nchi ambayo kila leo inashuhudia mauwaji ya wakulima na wafugaji kugombania malisho ya mifugo, Isingwezekana kupewa wa Zanzibari

Ni wakati wa Watanganyika sasa kuamka na kudai urithi wao waliopewa na muumbaji!

Kupewa haiwezi kuwa sawa na kununua, hivyo, pewa yao isitishwe rasimi ili shughuri zilizokuwa zikiendelea, ziendelee
Nyerere ndiye aliyewapa.
 
Ukiwa kiongozi, simama kama kiongozi, kubali kukosa tamu za stori za watu wa chini yako, ukijishusha sana ili ufaidi stori zao ukawa kama hao unaowasimamia, mwishowe katika stori zao za utani watakushika mpaka tako yako wewe kiongozi kwa sababu umeshakuwa kama wao.
Hivyo watanganyika ni Viongozi, ila sijajua wamefikiriwaje?!
 
Wa hovyo vipi unapolinganisha na wazenji wanaoshinda wakiutukana muungano mkuu
Hata bila ya Muungano, bado tuna mataifa na wawekezaji wa kimataifa wamepewa ardhi ya Tanganyika na sijaona mtu akihoji. Jina "Serikali ya Zanzibar" kuwekeza Makurunge tena kwa ajili ya kufuga tu kuinusuru Zanzibar na uhaba wa.malisho linawatia watu kichefuchefu.
 
Back
Top Bottom