#COVID19 Ninachokifahamu sahihi kuhusu Chanjo ya Covid-19, niulize swali nitakujibu

kumekua na sintofahamu nyingi mtaani na wengi wanajiuliza maswali kuhusu Chanjo ya Covid, Naomba nieleze kwa jinsi ninavyofahamu na kama una swali niulize nitakujibu kadri ninavyofahamu,

Kwanini Chanjo ya COVID 19 inapigiwa chapuo sana Licha ya kwamba ni hiyari?

- Hii ni kwasababu dunia nzima ipo katika mpango na juhudi za kutokomeza kabisa ugonjwa huu, ndio maana chanjo inasisitizwa sana kwasababu bila watu wote kuchomwa chanjo itakua ni ngumu sana ugonjwa huu kuisha,

Kwanini wanaochoma chanjo wanaendelea kuvaa barakoa? Je nikipata chanjo naweza kuambukizwa na kuambukiza?

- Wanaopata chanjo wanashauriwa kuvaa barakoa kwani wanauwezekano pia wa kupata maambukizi ya korona, iko hivi,
Chanjo Ya korona inapoingia mwilini mwako inaboost immunity, yaani inauongezea kinga mwili wako, kinga hii inayoongezwa inauwezo mkubwa wa kupambana na UVIKO, maana yake wewe uliepata chanjo tayari utakua na kinga utakapopata maambukizi ya UVIKO mwili wako utaweza kupambana na virusi hivyo na hatimaye kutoweka maana tayari una kinga ya kujilinda,

Kwanini baaadhi ya chanjo inatakiwa uchomwe zaidi ya mara moja?

Ni kawaida sana baadhi ya chanjo kuchomwa zaidi ya mara moja ili kuimarisha zaidi kinga mwili, mfano kuna chanjo za Tetanus Taxoid (chanjo ya tetenasi) hii huchomwa mara tatu kwa mwanaume na mara tano kwa wanawake pia zipo chanjo nyingine za watoto ambazo huchomwa zaidi ya mara moja,
pia katika chanjo za korona zipo baadhi ambazo unachomwa zaidi ya mara moja na nyingine ni mara moja tu kama Johnson Johnson

Kwanini baadhi ya mataifa ya magharibi licha ya chanjo ila uginjwa bado upo na watu wanakufa kwa covid?

Ni kwel hata baadhi ya mataifa ambayo chanjo imetengenezwa huko bado wanaugonjwa na watu wanakufa lakini kiuhalisia sio kwa idadi ile kama ya mwanzo,
mfano mzuri anagalia China ambako ugonjwa umeanzia, kule sasahivi wanaelekea kusahau mambo ya Corona kwasababu zaidi ya 90% wamepata chanjo,
Angalia ulaya sasahivi hata watu wameanza kufunguliwa angalia michuano ya Euro watu waliruhusiwa kuingia uwanjani na ugonjwa ulienea lakini sasahivi upo very week kwasababu watu wameshapata chanjo,

Angalia nchi ya Italy kipindi cha COVID walikufa sana kwa siku walikua wanakufa zaidi ya watu elfu 6, lakini kwa sasa idadi ya vifo haipo kwasababu wengi wameishapata chanjo hivyo virusi vya korona vimedhoofishwa sana havina nguvu tena,

Kwanini Chanjo ya COVID imechukua mda mfupi sana? je tutaaminije kama haitaleta madhara baadaye?

hakuna muda malumu uliowekwa wa chanjo kutengenezwa, hata hiyo chanjo ya kifua kikuu ambayo wewe umezaliwa ukaikuta, pia kipindi inatengenezwa wapo watu waliokua wa kwanza kuitumia na haijawadhuru,
rejea ugonjwa wa Ebora ulilipika Congo, Siera lion, na equatorial Guinea, ugonjwa ule ulilipuka ghafla na utengenezaji wa chanjo yake haukuchukua muda mrwfu na chanjo ilionyesha ufanisi mkubwa mpaka leo hii ebora imebaki kuwa historia,

Je chanjo ya Covin ndiyo Alam ya 666?

hayo mambo yamekaa kiimani zaidi na sio kisayansi na kusema kwamba chanjo ni chapa ya 666 ni sababu zisizo na mashiko kwani hata kwenye maandishi chapa ya mnyama hadi itokee tayari dunia itakua imeshapitia kipindi cha kuabudu siku moja na kuwa na serikali moja pia chapa ya mnyama itakua inahusisha moja kwa moja mpinga kristo,

Je, Wazungungu wanataka kutuua kupitia chanjo?

wakuue kwa lipi, wangetaka kukuua wasinheruhusu nchi mbalimbali zitengeneze chanjo chanjo ingekua ni moja dunia nzima, lakini mpaka sasa nchi nyingi zimetengeneza chanjo ikiwemo Africa kusini china na india kama mpango ungekua ni kuuwa watu basi ingetumika chanjo moja dunia nzima,

lakini vilevile ieleweke kwamba Mzungu akiamua kukuua, hauna ujanja wa kukwepa
 
Bourgeoisies kama akina Bill Gates walitabiri miaka sita iliyopita kwamba kungetokea mlipuko hatari ambao ungewaua watu kwa mamilioni, na kweli ikatokea since last year.

Ndiyo kusema wamekuwa prophets, au wao ndio waliwafadhili wataalamu wa Marekani nchini China ili wafinyange virusi vya korona kwenye maabara!???
 
Kirusi kinabadilika according to wataalam, je! Ni kweli kirusi Delta kimetoka na chanjo hizihizi?
Nasikia wale jamaa wenye Kovidi yao, ukifanikiwa kutengeneza the so-called vaccination, wao wanaibuka na variant mwingine. Recall yule wa SA, alpha, na sasa delta. Hii ni hatari na nusu.
 
Ni kwa nini watu wamekuwa na hofu ya chanjo?

Ni sababu ya kauli ya Dr Magufuli kuwaambia chanjo hazifai?
Ni kwa sababu korona inapewa uzito mkubwa kuliko hali halisi; mbaya zaidi chanjo hazina mashiko; mbaya zaidi kabisa, watu wanaohongwa ili wapigwe chanjo mwendokasi.
 
Labda swali gani vile ulitegemea aulize!???
Labda nikuulize wewe kwanza whats so special about 5G? Maana kulikuwa na 2G,3G,4G, then kuna 5G (Mimi naitumia hiyo). Na huu siyo mwisho wa Gs, kuna nyingine zinakuja, why hii 5G iwe tofauti na hizo Gs nyingine?
 
Kama dhumuni la chanjo nikuitambulisha Covid mwilin kwa kuziboost imuneet sijui mnaita, je inatofauti gani nasisi ambao tuliumwa phase 1 na kupana na miili yetu ambao tuliumwa awali nasasa ata tukiumwa hatusumbuliwi tena kama awali
 
Kwanini wanaodungwa chanjo wanaugua tena corona? Hapa mimi ndo nina was wasi na hii chanjo.
kumekua na sintofahamu nyingi mtaani na wengi wanajiuliza maswali kuhusu Chanjo ya Covid, Naomba nieleze kwa jinsi ninavyofahamu na kama una swali niulize nitakujibu kadri ninavyofahamu,

Kwanini Chanjo ya COVID 19 inapigiwa chapuo sana Licha ya kwamba ni hiyari?

- Hii ni kwasababu dunia nzima ipo katika mpango na juhudi za kutokomeza kabisa ugonjwa huu, ndio maana chanjo inasisitizwa sana kwasababu bila watu wote kuchomwa chanjo itakua ni ngumu sana ugonjwa huu kuisha,

Kwanini wanaochoma chanjo wanaendelea kuvaa barakoa? Je nikipata chanjo naweza kuambukizwa na kuambukiza?

- Wanaopata chanjo wanashauriwa kuvaa barakoa kwani wanauwezekano pia wa kupata maambukizi ya korona, iko hivi,
Chanjo Ya korona inapoingia mwilini mwako inaboost immunity, yaani inauongezea kinga mwili wako, kinga hii inayoongezwa inauwezo mkubwa wa kupambana na UVIKO, maana yake wewe uliepata chanjo tayari utakua na kinga utakapopata maambukizi ya UVIKO mwili wako utaweza kupambana na virusi hivyo na hatimaye kutoweka maana tayari una kinga ya kujilinda,

Kwanini baaadhi ya chanjo inatakiwa uchomwe zaidi ya mara moja?

Ni kawaida sana baadhi ya chanjo kuchomwa zaidi ya mara moja ili kuimarisha zaidi kinga mwili, mfano kuna chanjo za Tetanus Taxoid (chanjo ya tetenasi) hii huchomwa mara tatu kwa mwanaume na mara tano kwa wanawake pia zipo chanjo nyingine za watoto ambazo huchomwa zaidi ya mara moja,
pia katika chanjo za korona zipo baadhi ambazo unachomwa zaidi ya mara moja na nyingine ni mara moja tu kama Johnson Johnson

Kwanini baadhi ya mataifa ya magharibi licha ya chanjo ila uginjwa bado upo na watu wanakufa kwa covid?

Ni kwel hata baadhi ya mataifa ambayo chanjo imetengenezwa huko bado wanaugonjwa na watu wanakufa lakini kiuhalisia sio kwa idadi ile kama ya mwanzo,
mfano mzuri anagalia China ambako ugonjwa umeanzia, kule sasahivi wanaelekea kusahau mambo ya Corona kwasababu zaidi ya 90% wamepata chanjo,
Angalia ulaya sasahivi hata watu wameanza kufunguliwa angalia michuano ya Euro watu waliruhusiwa kuingia uwanjani na ugonjwa ulienea lakini sasahivi upo very week kwasababu watu wameshapata chanjo,

Angalia nchi ya Italy kipindi cha COVID walikufa sana kwa siku walikua wanakufa zaidi ya watu elfu 6, lakini kwa sasa idadi ya vifo haipo kwasababu wengi wameishapata chanjo hivyo virusi vya korona vimedhoofishwa sana havina nguvu tena,

Kwanini Chanjo ya COVID imechukua mda mfupi sana? je tutaaminije kama haitaleta madhara baadaye?

hakuna muda malumu uliowekwa wa chanjo kutengenezwa, hata hiyo chanjo ya kifua kikuu ambayo wewe umezaliwa ukaikuta, pia kipindi inatengenezwa wapo watu waliokua wa kwanza kuitumia na haijawadhuru,
rejea ugonjwa wa Ebora ulilipika Congo, Siera lion, na equatorial Guinea, ugonjwa ule ulilipuka ghafla na utengenezaji wa chanjo yake haukuchukua muda mrwfu na chanjo ilionyesha ufanisi mkubwa mpaka leo hii ebora imebaki kuwa historia,

Je chanjo ya Covin ndiyo Alam ya 666?

hayo mambo yamekaa kiimani zaidi na sio kisayansi na kusema kwamba chanjo ni chapa ya 666 ni sababu zisizo na mashiko kwani hata kwenye maandishi chapa ya mnyama hadi itokee tayari dunia itakua imeshapitia kipindi cha kuabudu siku moja na kuwa na serikali moja pia chapa ya mnyama itakua inahusisha moja kwa moja mpinga kristo,

Je, Wazungungu wanataka kutuua kupitia chanjo?

wakuue kwa lipi, wangetaka kukuua wasinheruhusu nchi mbalimbali zitengeneze chanjo chanjo ingekua ni moja dunia nzima, lakini mpaka sasa nchi nyingi zimetengeneza chanjo ikiwemo Africa kusini china na india kama mpango ungekua ni kuuwa watu basi ingetumika chanjo moja dunia nzima,

lakini vilevile ieleweke kwamba Mzungu akiamua kukuua, hauna ujanja wa kukwepa

Kwanini kwenye fomu ya chanjo, serikali ilijitoabkuwajibika kwa lolote litakalotokea?

- chanjo kazi yake ni kuboost immunity ili mwili wako uwe na uwezo wa kupambana na Covid pale unapoipata,

sasa basi kipaumbele cha kwanza ni wenye magonjwa sugu, na wenye magonjwa sugu wengi immunity zao ziko chini sana so serikali ikisema iwalipe

ikitokea mtu yytr amepiga chanjo na akafa hata kwa ugonjwa mwingine watadai fidia,

means mimi niwe na Chronic heart diseases nikaamua kuchoma chanjo, mwezi mmoja ukipita nikafa kwa ugonjwa wa moyo au mwingine wwte ule lazima ndugu waidai serikali fidia,

sasa serikali italipa wangapi?

maana hapa ingesema ihusike watu wangeenda kuiangushia serikali jumba bovu, mtu anakufa kwa TB ila kwakua alipiga vaccine ya covvid atataka alipwe
 
Ni kwa nini watu wamekuwa na hofu ya chanjo?

Ni sababu ya kauli ya Dr Magufuli kuwaambia chanjo hazifai?
Nakumbuka 2010 kwenye utawala wa kikwete seerikali ya marekani kupitia wizara ya Afya walitoa vyandarua vya msaada, wapo watu wengi sana walipotosha kwamba vyandarua vile vinadawa wazungu wanataka kutuua, lakini haikua kweli mpaka sasa watu waliovitumia wapo hawajafa na bado vinaendelea kugawiwa,

dhana ya kuogopa chanjo kwa kiasi kikubwa ni kwasababu ya kutokea watu kwenye jamii ambao wanapotosha ndio maana ukimuuliza mtu kwanini unapinga chanjo hana sababu zaidi ya kusema magufuli alikataa, gwajima amekataa mbona ulaya corona bado ipo, wazungu wanataka watuue,

imekua ni kawaida sana kwa baadhi ya watu kupotosha ukweli aidha kwabkujua au kwakutokujua
 
Labda nikuulize wewe kwanza whats so special about 5G? Maana kulikuwa na 2G,3G,4G, then kuna 5G (Mimi naitumia hiyo). Na huu siyo mwisho wa Gs, kuna nyingine zinakuja, why hii 5G iwe tofauti na hizo Gs nyingine?
Umeona!??? Kumbe na wewe una maswali kama huyo jamaa uliyemzimisha!??? Mbona sasa unamkatisha, wewe Kibwetere!??? Ungemwacha huyu mtaalamu wa CDC atujibie aiseee!!! 🙂
 
Kwanini wanaodungwa chanjo wanaugua tena corona? Hapa mimi ndo nina was wasi na hii chanjo.
mbona ilo swali limeshajibiwa au hujasoma vizuri, chanjo inaboost immunity ya mwili uwe tayari kupambana na covid pale unapoambukizwa,

ieleweke chanjo haizuii kuambukizwa isipokua inakuongezea kinga mwili ya kuushambulia vile virusi pale unapoambukizwa
 
Mtu anajikuta mtaalamu wa kuichambua covid in positive ways only, anasahau kuwa hii ni dunia, na hii dunia inaendeshwa kwa ushindan na majigambo, uku mwenye nguvu akitaka kuwa na nguvu milele, kama ilivyokuwa kw falme na dola zilizopita, zltumia kila njia kuimarisha dola zao il zidumu, sasa ile mitindo bado ipo na itaendelea kuwepo, ni mpumbav na mjinga pekee atakaepinga kuwa covid haina agenda nyuma ya pazia, mpumbv kama huyu ni aina ya wale watu ambao wanazan dunian kuna aman, na mataifa yanapendana, suala la covid lilishatabiliwa na wao kitambo sana kupitia njia za fasihi watumiazo kupitisha ujumbe,pia kupitia media zao, haya mambo yakishatabiliwa na wao, wenzao wanaojua kuchambua lugha za siri walikwisha elewa kitambo kuwa kuna ugeni unakuja na hawa ndy watu pekee wanaoelewa nn kipo nyuma ya pazia kwenye covid19. Achana na hawa wanasiasa na madactar uchwara wa kibongo wanaojifanya wajuwaji wa kuamasisha chanjo wakat wao dawa ya mbu na panado vimewashinda kutengeneza,..Nasisitiza namm tumia hiari hii kukataa chanjo,,iyo chanjo mnazosema ni sarama ndan yake kuna materials walizotumia hatujui n nn na zna fanyaje kaz, kuna waliopata chanjo miili yao imegeuka magnetic yaan inaattract vitu vya chuma sehem walizodungwa chanjo, kuna wengine wanalalamika wakipachika balbu ya zaid ya watt60 sehem Walz chanja balbu inawaka na kutoa mwanga mkubwa tu sasa wew unaesema hiyo kitu ni salama why this?? Kuna siri kubwa ktk hili, ndio maana wanaopinga hiy kitu wanaandamwa na kutukanwa kila aina ya matusi mara ooh wajinga wanajitenga na dunia, upuuz huu...mwenye akil na afungue ufaham wake, we are not safe
 
Nakumbuka 2010 kwenye utawala wa kikwete seerikali ya marekani kupitia wizara ya Afya walitoa vyandarua vya msaada, wapo watu wengi sana walipotosha kwamba vyandarua vile vinadawa wazungu wanataka kutuua, lakini haikua kweli mpaka sasa watu waliovitumia wapo hawajafa na bado vinaendelea kugawiwa,

dhana ya kuogopa chanjo kwa kiasi kikubwa ni kwasababu ya kutokea watu kwenye jamii ambao wanapotosha ndio maana ukimuuliza mtu kwanini unapinga chanjo hana sababu zaidi ya kusema magufuli alikataa, gwajima amekataa mbona ulaya corona bado ipo, wazungu wanataka watuue,

imekua ni kawaida sana kwa baadhi ya watu kupotosha ukweli aidha kwabkujua au kwakutokujua
Hivi ili madhara yatokee, inachukua muda gani kwani!??? I mean study ya kutosha imefanywa juu ya chanya na hasi za vaccines zako hizi!???

Na hivi umeangalia side-effects kwenye websites ya akina J&J, Pfizer, Mordena, nk!??? Usikute wewe ni miongoni mwa madalali waliolipwa kupigia korona upata bila kujali chochote.

Nawakumbuka sana wauzaji wa barakoa ambao wao wenye hata ndiyo kwanzaaaaaaa hawana taimu nayo --- midomo na pua viko wazi kama tu kama jana 🙂 🙂 🙂
 
Nakumbuka 2010 kwenye utawala wa kikwete seerikali ya marekani kupitia wizara ya Afya walitoa vyandarua vya msaada, wapo watu wengi sana walipotosha kwamba vyandarua vile vinadawa wazungu wanataka kutuua, lakini haikua kweli mpaka sasa watu waliovitumia wapo hawajafa na bado vinaendelea kugawiwa,

dhana ya kuogopa chanjo kwa kiasi kikubwa ni kwasababu ya kutokea watu kwenye jamii ambao wanapotosha ndio maana ukimuuliza mtu kwanini unapinga chanjo hana sababu zaidi ya kusema magufuli alikataa, gwajima amekataa mbona ulaya corona bado ipo, wazungu wanataka watuue,

imekua ni kawaida sana kwa baadhi ya watu kupotosha ukweli aidha kwabkujua au kwakutokujua
Watakufa tu wape muda ipite kama miaka 100 hivi lazima wengi wao watakuwa wamekufa🐒
 
Unakumbuka WHO ilisema mwaka jana kwamba watu wasivae barakoa, then wakasema baadaye wavae!??? Sababu walisema walidhani ugonjwa wa korona hauzuiliki kwa barakoa. Kisha wakachukua V-turn!!!
mbona ilo swali limeshajibiwa au hujasoma vizuri, chanjo inaboost immunity ya mwili uwe tayari kupambana na covid pale unapoambukizwa,

ieleweke chanjo haizuii kuambukizwa isipokua inakuongezea kinga mwili ya kuushambulia vile virusi pale unapoambukizwa
 
Watakufa tu wape muda ipite kama miaka 100 hivi lazima wengi wao watakuwa wamekufa🐒
Mbona unakata tamaa mapema hivi!??? Huku Bongo kukata tamaa kwa sababu yoyote ile iwayo ni mwiko wa ugali wa sherehe.
 
Nakumbuka 2010 kwenye utawala wa kikwete seerikali ya marekani kupitia wizara ya Afya walitoa vyandarua vya msaada, wapo watu wengi sana walipotosha kwamba vyandarua vile vinadawa wazungu wanataka kutuua, lakini haikua kweli mpaka sasa watu waliovitumia wapo hawajafa na bado vinaendelea kugawiwa,

dhana ya kuogopa chanjo kwa kiasi kikubwa ni kwasababu ya kutokea watu kwenye jamii ambao wanapotosha ndio maana ukimuuliza mtu kwanini unapinga chanjo hana sababu zaidi ya kusema magufuli alikataa, gwajima amekataa mbona ulaya corona bado ipo, wazungu wanataka watuue,

imekua ni kawaida sana kwa baadhi ya watu kupotosha ukweli aidha kwabkujua au kwakutokujua

Sababu ulizozitaja zinamantiki, lakini kwanini hausemi pia kwamba ilionekana wanaopata chanjo damu inaganda? Na vile vile kuhusianishwa kwa mabadiliko ya vinasaba na chanjo? Na hivi karibuni EU wanataka kuigomea AstraZeneca inayotengenezwa India, kwanini watake ya UK pekee? Hauoni hapo maslahi ya kibiashara yanataka kuwa mbele zaidi ya kutoa matibabu?
 
Ukweli 70%
Pumba 30%

Ume address upande wa madhara yanayoweza kutokea kwenye chanjo kisiasa sana na hata upande wa jinsi chanjo inavyopatikana umetoa majibu yafunika kombe mwanaharamu apite

Wasomi wakiafrica mnakasumba moja mna elimu lakini uwezo wa ku reasoning mmeshikiwa na waliowapa elimu.Ni mara chache sana kukuta msomi wa kiafrica aliye na mawazo tofauti ya wazungu.

Nadhani wengi wenu mnaamini mkiwa tofauti ni kama mnakuwa vilaza au tulishaaminishwa kwenye haya maelimu tunayopewa kwamba wewe ni inferior huna unalojua hivyo ninachosema mimi jifunZe kukielewa na kukibeba km kilivyosababu wewe ni mjinga hutakiwi kuwa na mawazo yako binafsi!!haya chukua hiki cheti kitumie kutetea maslahi yangu tu
 
Back
Top Bottom