#COVID19 Ninachokifahamu sahihi kuhusu Chanjo ya Covid-19, niulize swali nitakujibu

#COVID19 Ninachokifahamu sahihi kuhusu Chanjo ya Covid-19, niulize swali nitakujibu

Mbona umekimbia uzi, maswali yamekuwa magumu?
kumekua na sintofahamu nyingi mtaani na wengi wanajiuliza maswali kuhusu Chanjo ya Covid, Naomba nieleze kwa jinsi ninavyofahamu na kama una swali niulize nitakujibu kadri ninavyofahamu,

Kwanini Chanjo ya COVID 19 inapigiwa chapuo sana Licha ya kwamba ni hiyari?

- Hii ni kwasababu dunia nzima ipo katika mpango na juhudi za kutokomeza kabisa ugonjwa huu, ndio maana chanjo inasisitizwa sana kwasababu bila watu wote kuchomwa chanjo itakua ni ngumu sana ugonjwa huu kuisha,


Kwanini wanaochoma chanjo wanaendelea kuvaa barakoa? Je nikipata chanjo naweza kuambukizwa na kuambukiza?


- Wanaopata chanjo wanashauriwa kuvaa barakoa kwani wanauwezekano pia wa kupata maambukizi ya korona, iko hivi,
Chanjo Ya korona inapoingia mwilini mwako inaboost immunity, yaani inauongezea kinga mwili wako, kinga hii inayoongezwa inauwezo mkubwa wa kupambana na UVIKO, maana yake wewe uliepata chanjo tayari utakua na kinga utakapopata maambukizi ya UVIKO mwili wako utaweza kupambana na virusi hivyo na hatimaye kutoweka maana tayari una kinga ya kujilinda,



Kwanini baaadhi ya chanjo inatakiwa uchomwe zaidi ya mara moja?

Ni kawaida sana baadhi ya chanjo kuchomwa zaidi ya mara moja ili kuimarisha zaidi kinga mwili, mfano kuna chanjo za Tetanus Taxoid (chanjo ya tetenasi) hii huchomwa mara tatu kwa mwanaume na mara tano kwa wanawake pia zipo chanjo nyingine za watoto ambazo huchomwa zaidi ya mara moja,
pia katika chanjo za korona zipo baadhi ambazo unachomwa zaidi ya mara moja na nyingine ni mara moja tu kama Johnson Johnson




Kwanini baadhi ya mataifa ya magharibi licha ya chanjo ila uginjwa bado upo na watu wanakufa kwa covid?

Ni kwel hata baadhi ya mataifa ambayo chanjo imetengenezwa huko bado wanaugonjwa na watu wanakufa lakini kiuhalisia sio kwa idadi ile kama ya mwanzo,
mfano mzuri anagalia China ambako ugonjwa umeanzia, kule sasahivi wanaelekea kusahau mambo ya Corona kwasababu zaidi ya 90% wamepata chanjo,
Angalia ulaya sasahivi hata watu wameanza kufunguliwa angalia michuano ya Euro watu waliruhusiwa kuingia uwanjani na ugonjwa ulienea lakini sasahivi upo very week kwasababu watu wameshapata chanjo,

Angalia nchi ya Italy kipindi cha COVID walikufa sana kwa siku walikua wanakufa zaidi ya watu elfu 6, lakini kwa sasa idadi ya vifo haipo kwasababu wengi wameishapata chanjo hivyo virusi vya korona vimedhoofishwa sana havina nguvu tena,




Kwanini Chanjo ya COVID imechukua mda mfupi sana? je tutaaminije kama haitaleta madhara baadaye?

hakuna muda malumu uliowekwa wa chanjo kutengenezwa, hata hiyo chanjo ya kifua kikuu ambayo wewe umezaliwa ukaikuta, pia kipindi inatengenezwa wapo watu waliokua wa kwanza kuitumia na haijawadhuru,
rejea ugonjwa wa Ebora ulilipika Congo, Siera lion, na equatorial Guinea, ugonjwa ule ulilipuka ghafla na utengenezaji wa chanjo yake haukuchukua muda mrwfu na chanjo ilionyesha ufanisi mkubwa mpaka leo hii ebora imebaki kuwa historia,




Je chanjo ya Covin ndiyo Alam ya 666?

hayo mambo yamekaa kiimani zaidi na sio kisayansi na kusema kwamba chanjo ni chapa ya 666 ni sababu zisizo na mashiko kwani hata kwenye maandishi chapa ya mnyama hadi itokee tayari dunia itakua imeshapitia kipindi cha kuabudu siku moja na kuwa na serikali moja pia chapa ya mnyama itakua inahusisha moja kwa moja mpinga kristo,


Je, Wazungungu wanataka kutuua kupitia chanjo?

wakuue kwa lipi, wangetaka kukuua wasinheruhusu nchi mbalimbali zitengeneze chanjo chanjo ingekua ni moja dunia nzima, lakini mpaka sasa nchi nyingi zimetengeneza chanjo ikiwemo Africa kusini china na india kama mpango ungekua ni kuuwa watu basi ingetumika chanjo moja dunia nzima,

lakini vilevile ieleweke kwamba Mzungu akiamua kukuua, hauna ujanja wa kukwepa



Kwanini kwenye fomu ya chanjo, serikali ilijitoabkuwajibika kwa lolote litakalotokea?

- chanjo kazi yake ni kuboost immunity ili mwili wako uwe na uwezo wa kupambana na Covid pale unapoipata,

sasa basi kipaumbele cha kwanza ni wenye magonjwa sugu, na wenye magonjwa sugu wengi immunity zao ziko chini sana so serikali ikisema iwalipe

ikitokea mtu yytr amepiga chanjo na akafa hata kwa ugonjwa mwingine watadai fidia,

means mimi niwe na Chronic heart diseases nikaamua kuchoma chanjo, mwezi mmoja ukipita nikafa kwa ugonjwa wa moyo au mwingine wwte ule lazima ndugu waidai serikali fidia,

sasa serikali italipa wangapi?

maana hapa ingesema ihusike watu wangeenda kuiangushia serikali jumba bovu, mtu anakufa kwa TB ila kwakua alipiga vaccine ya covvid atataka alipwe
 
Mtu anajikuta mtaalamu wa kuichambua covid in positive ways only, anasahau kuwa hii ni dunia, na hii dunia inaendeshwa kwa ushindan na majigambo, uku mwenye nguvu akitaka kuwa na nguvu milele, kama ilivyokuwa kw falme na dola zilizopita, zltumia kila njia kuimarisha dola zao il zidumu, sasa ile mitindo bado ipo na itaendelea kuwepo, ni mpumbav na mjinga pekee atakaepinga kuwa covid haina agenda nyuma ya pazia, mpumbv kama huyu ni aina ya wale watu ambao wanazan dunian kuna aman, na mataifa yanapendana, suala la covid lilishatabiliwa na wao kitambo sana kupitia njia za fasihi watumiazo kupitisha ujumbe,pia kupitia media zao, haya mambo yakishatabiliwa na wao, wenzao wanaojua kuchambua lugha za siri walikwisha elewa kitambo kuwa kuna ugeni unakuja na hawa ndy watu pekee wanaoelewa nn kipo nyuma ya pazia kwenye covid19. Achana na hawa wanasiasa na madactar uchwara wa kibongo wanaojifanya wajuwaji wa kuamasisha chanjo wakat wao dawa ya mbu na panado vimewashinda kutengeneza,..Nasisitiza namm tumia hiari hii kukataa chanjo,,iyo chanjo mnazosema ni sarama ndan yake kuna materials walizotumia hatujui n nn na zna fanyaje kaz, kuna waliopata chanjo miili yao imegeuka magnetic yaan inaattract vitu vya chuma sehem walizodungwa chanjo, kuna wengine wanalalamika wakipachika balbu ya zaid ya watt60 sehem Walz chanja balbu inawaka na kutoa mwanga mkubwa tu sasa wew unaesema hiyo kitu ni salama why this?? Kuna siri kubwa ktk hili, ndio maana wanaopinga hiy kitu wanaandamwa na kutukanwa kila aina ya matusi mara ooh wajinga wanajitenga na dunia, upuuz huu...mwenye akil na afungue ufaham wake, we are not safe

magonjwa mengi tukianza na Ukimwi ule ni mpango wa watu na ni biashara za watu, mtu anatengeneza ugonjwa na natengemeza dawa sasa ukiishalijuabhilo kama unaakilibtimamu lazima aidha utengemeze dawa au ununue dawa
 
Ingekua vizuri pia ukajitambulisha wasifu wako kitaalam tujue uwezo na aina ya mtu tunaejadili nae. Sina maana ya kudharau uelewa wako, la hasha, nafikiri unaelewa kwamba kila eneo lina taaluma yake.
 
Ila hujasema pumba zake ni zipi na punje ni gani!??? Halafu, hiyo 30% na 70% umetumia kanuni ya nani, maana Prof. Majimarefu hakuacha fomyula hiyo mpaka amefariki dunia.
Ukweli 70%
Pumba 30%

Ume address upande wa madhara yanayoweza kutokea kwenye chanjo kisiasa sana na hata upande wa jinsi chanjo inavyopatikana umetoa majibu yafunika kombe mwanaharamu apite

Wasomi wakiafrica mnakasumba moja mna elimu lakini uwezo wa ku reasoning mmeshikiwa na waliowapa elimu.Ni mara chache sana kukuta msomi wa kiafrica aliye na mawazo tofauti ya wazungu.

Nadhani wengi wenu mnaamini mkiwa tofauti ni kama mnakuwa vilaza au tulishaaminishwa kwenye haya maelimu tunayopewa kwamba wewe ni inferior huna unalojua hivyo ninachosema mimi jifunZe kukielewa na kukibeba km kilivyosababu wewe ni mjinga hutakiwi kuwa na mawazo yako binafsi!!haya chukua hiki cheti kitumie kutetea maslahi yangu tu
 
Unakumbuka WHO ilisema mwaka jana kwamba watu wasivae barakoa, then wakasema baadaye wavae!??? Sababu walisema walidhani ugonjwa wa korona hauzuiliki kwa barakoa. Kisha wakachukua V-turn!!!
kazi ya WHO ni kufanya tafiti kila kukicha na kugundua mambo mapya, tangu umezaliwa mpaka umri huo ulionao dawa zote unazotumia ni matokeo ya tafiti za WHO, ndio maana zamani wagonjwa wa HIV walimeza ARV zaidi ya moja lakini kwa sasa ni moja tu kwa siku,

hayo ni matokeo ya tafiti na ugunduzi wa mambo mapya
 
magonjwa mengi tukianza na Ukimwi ule ni mpango wa watu na ni biashara za watu, mtu anatengeneza ugonjwa na natengemeza dawa sasa ukiishalijuabhilo kama unaakilibtimamu lazima aidha utengemeze dawa au ununue dawa
Kama ndivyo, kwa nini tusiamini basi kwamba hata chanjo zipo feki kwa lengo tu la kibiashara na maslahi binafsi yao hayo mabwanyenye ya barafuni Antaktiki!???
 
Nasikia wale jamaa wenye Kovidi yao, ukifanikiwa kutengeneza the so-called vaccination, wao wanaibuka na variant mwingine. Recall yule wa SA, alpha, na sasa delta. Hii ni hatari na nusu.
Ndo hapo sasa sijui tutakuwa na phase 50
 
Ingekua vizuri pia ukajitambulisha wasifu wako kitaalam tujue uwezo na aina ya mtu tunaejadili nae. Sina maana ya kudharau uelewa wako, la hasha, nafikiri unaelewa kwamba kila eneo lina taaluma yake.
Kwa hiyo, hata akikwambia ana Piihechidii mia, lazima uamini tu!??? Elimu ya vyeti haina maana sana. Tumeshamchora huyu jamaa hapahapa. 🙂
 
Swali langu ni je chanjo ya UVIKO 19 inasaidia pia mty kumkinga na mafua haya ya kawaida?
Hawezi kukujibu huyo. Ngoja nikusaidie. Unajua, kama tu chanjo haisaidii kwenye ugonjwa lengwa wa korona, akili nyepesi inaonesha kwamba the so-called chanjo haiwezi kusaidia kwa lolote zaidi ya kuongeza kemikali mwilini na kusababisha madhara ambayo tayari yameshaoneshwa na wataalamu wengi tu.
 
Ila hujasema pumba zake ni zipi na punje ni gani!??? Halafu, hiyo 30% na 70% umetumia kanuni ya nani, maana Prof. Majimarefu hakuacha fomyula hiyo mpaka amefariki dunia.

Huyu mtu ameongelea chanjo ya corona kama kitu kizuri na bora kwa sasa

Lakini mtu yeyote mwenye utimamu kdg tu akifuatilia chanjo ya corona lazima apate ukakasi

Limekaa kisiasa kihuni kitapeli sana hata wao wenyewe wanaotuletea hizi chanjo hawana majibu ya kueleweka ila huyu anataka kulifanya jepesi sana na tulipokee km jambo jepesi..

Sasa ndo tunasema kasoma uwezo wake wa kufikiri umeboreshwa .Je ambao shule hawajaenda kabisa!!!
 
Mbona machanjo wanayopewa watoto wenu baada ya kuzaliwa hamyakatai?! Maafrka majinga sana, asilimia 99 ya dawa na chanjo zimeletwa na wazungu na yanatumia. Eti leo yanagomea chanjo ya korona! Maajabu.
 
Mbona machanjo wanayopewa watoto wenu baada ya kuzaliwa hamyakatai?! Maafrka majinga sana, asilimia 99 ya dawa na chanjo zimeletwa na wazungu na yanatumia. Eti leo yanagomea chanjo ya korona! Maajabu.
Hivyo umejitukana na wewe, au u ngozi ya samawi!??? Halafu, usidhani hao jamaa zako wao wanaikubali hii chanjo ya mwendokasi, sawa!???
 
Wewe ndo mjinga namba moja. Jiulize kwanini chanjo ya corona pekee ndio watu wapate ukakasi?
Mbona machanjo wanayopewa watoto wenu baada ya kuzaliwa hamyakatai?! Maafrka majinga sana, asilimia 99 ya dawa na chanjo zimeletwa na wazungu na yanatumia. Eti leo yanagomea chanjo ya korona! Maajabu.
 
Kwa hiyo, hata akikwambia ana Piihechidii mia, lazima uamini tu!??? Elimu ya vyeti haina maana sana. Tumeshamchora huyu jamaa hapahapa. 🙂

Sitaamini ila ntajua najadili hoja na mtu mwenye uelewa wa kiwango gani nauzoefu wake katika eneo husika. Itanisaidia kuchagua maswali ya kumuuliza.
 
ungejikita zaidi kuuliza swali linalokutatiza nisingekujibu mimi angekujibu mwingine mwenye uelewa zaidi

Ok, basi anza kwa kujibu hayo niliyouliza kuhusu kudanda damu na AstraZeneca ya India kutiliwa shaka EU, kwamba hata kama umepatiwa chanjo, lazima wakuweke karanteen na upimwe. Ahsante
 
Back
Top Bottom