Ninachoona kwenye Parade ya China Aisee! Kama taifa na bara tupo nyuma sana

Sio kweli Japan ndo alimpiga mchina,wachina wengi walikufa.
 
Ni kweli miaka ya 60s na userious kabisa ni miaka ya 80s mpaka 2000s fulani hivi baada ya kuamua ku modernize jeshi lao
Youtube wale wanatengeneza content za kusafiri toka ulaya wanasema wazi kuwa china ina moundombinu, usafi kuliko kwao. Kuna mmoja toka Uingereza akasema amegundua kuwa nchi yake kwa sasa ni 3rd world country baada ya kufika china
 
Kuna mzee mmoja veteran hapa kapiga salute silaha zinapopita mbele mpaka chozi nafikiri atakuwa kakumbuka namna walivyokuwa wakipambana na Japan enzi kwa silaha za hovyo na kwa sasa jeshi lao lilivyo ni moment fulani hivi ya kishujaa
 
China kijeshi huenda ni taifa kubwa kuliko hata Urusi (japo kazidiwa wingi wa silaha za nyuklia).

T14 Armata Lee Van free
 
Labda kama ulikuwa hujui

Viongozi wote wa UVCCM ya China (Wing ya vijana ya CCP) wana elimu kubwa sana zaidi ya asilimia 60 wana PhD za Darasani, zaidi ya nusu ya hizo PhD ni za STEM (Science, Technology, Engineering and Mathematics), asilimia 40 iliyobaki wana Degree na Masters na nyingi pia ni za STEM

CCM mgombea wao wa Urais aliombewa kufaulu darasa la saba na baba yake, CV yake ni ya mtu kasoma Lahore Pakistan, sasa imagine utashindana na China kwa lipi, Marais wa nchi ndio wanatarajiwa kuwa taswira ya taifa ila wetu ni ...
 
Upo sahihi marekani ni mwamba mjanja sana anakuletea vita kwako na ndio maana haoni hasara kuwa na military bases kila pande ya dunia
 
Hii ilikuwa ni baada ya failure ya Cultural Revolution ya Mao. Deng Xiaoping aliposhika usukani kaigeuza china yote KWA muda mfupi wakati sisi tukiendelea kupiga jalamba la kijani.
Kuna clip mwandishi wa habari wa bbc anamhoji waziri wa mambo ya nje ya china kuwa china ni rafiki, adui au mshindani wa uingereza.
Aisee jamaa alimpa jibu moja matata.
Akamwambia wao kama china hawaoni kama ni washindani wa uingereza katika chochote.
Akaanza kumtajia vitu ambavyo wanaongoza kuanzia mauzo ya EVs, export, ugunduzi na research, gdp n.k akasema kwa hiyo hakuna wanachoshindana na mwingereza maana wao ama ni wa kwanza au wa pili nyuma ya marekani katika kila kitu.
Akasema wao wanachokiona ni kuwa uingereza ni taifa tu ambalo wanapaswa kushirikiana nalo kwa amani wala si mshindani kwa lolote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…