Ninachoona kwenye Parade ya China Aisee! Kama taifa na bara tupo nyuma sana

Ninachoona kwenye Parade ya China Aisee! Kama taifa na bara tupo nyuma sana

Kupitia maonesho ya hii parade ya wachina kutimiza miaka 80 toka vita vya pili vya dunia baada ya kumnyuka Japan.

Kama taifa la Tanzania na bara zima la Afrika tujitafakari kidogo kwa kweli tupo nyuma kiulinzi.

Kwa hizi silaha wachina walizo amua kutuonesha japo nina mashaka kama wameonesha zote kabisa walizo nazo tupo nyuma sana ndugu zangu.


Tusijiongopee wakuu tumeachwa mbali sana hizi silaha tulizo nazo kwetu sijui hawa mabwana wameziacha store maana hapa sioni huu uchafu wetu naona vitu vizito vizito mpaka inatisha siku tukianzisha ka vita ka kirafiki sisi na wao maana kamanda wetu mmoja wa JW alisema sisi ni jeshi la sita kwa ubora😁

Ukitazama kwenye documentaries silaha walizokuwa wakitumia wachina wakati wanapambana na Japan na vita vya wenyewe kwa wenyewe ni magobore ya ajabu ajabu hata airforce walikuwa hawana wala jeshi la wana maji linalo jitambua ila leo wanaonesha vyuma vizito hapa.



Sisi bado tumejaza magobore
Size yetu ni kuhakikisha TL anafungwa ananyamazishwa asiongee ujinga wetu.
 
Dunia ipo kasi mkuu ni sisi tu tumebaki nyuma nyuma kwa kila kitu.
Na miaka inavyozidi kwenda ndio tunazidi kuachwa nyuma zaidi kwasababu wenzetu wanajenga juu ya misingi waliyojiwekea miaka ya nyuma. Sisi hata kwenye msingi bado 🙁
 
Kuna clip mwandishi wa habari wa bbc anamhoji waziri wa mambo ya nje ya china kuwa china ni rafiki, adui au mshindani wa uingereza.
Aisee jamaa alimpa jibu moja matata.
Akamwambia wao kama china hawaoni kama ni washindani wa uingereza katika chochote.
Akaanza kumtajia vitu ambavyo wanaongoza kuanzia mauzo ya EVs, export, ugunduzi na research, gdp n.k akasema kwa hiyo hakuna wanachoshindana na mwingereza maana wao ama ni wa kwanza au wa pili nyuma ya marekani katika kila kitu.
Akasema wao wanachokiona ni kuwa uingereza ni taifa tu ambalo wanapaswa kushirikiana nalo kwa amani wala si mshindani kwa lolote.
😀
 
Sio kweli Japan ndo alimpiga mchina,wachina wengi walikufa.
Kwenye vita kinacho tazamwa ni ushindi sio idadi ya watu wangapi wamekufa.

Hata wasoviet walikufa wengi kuliko wajerumani lakini wasoviet ndio walioshinda
 
Swali lako linaweza kujibiwa kwenye huu uzi
 
Youtube wale wanatengeneza content za kusafiri toka ulaya wanasema wazi kuwa china ina moundombinu, usafi kuliko kwao. Kuna mmoja toka Uingereza akasema amegundua kuwa nchi yake kwa sasa ni 3rd world country baada ya kufika china
Wanastahili pongezi kwa walipotoka,walipo na wanapokwenda sio kazi ndogo kabisa
 
CCM mgombea wao wa Urais aliombewa kufaulu darasa la saba na baba yake, CV yake ni ya mtu kasoma Lahore Pakistan, sasa imagine utashindana na China kwa lipi, Marais wa nchi ndio wanatarajiwa kuwa taswira ya taifa ila wetu ni ...
😁 Ila wabongo kwamba Sasha alisomea ususi Pakistan akashibdane na wakina Xi kazi kweli kweli
 
Back
Top Bottom