Marcostilone
JF-Expert Member
- Jun 25, 2023
- 7,018
- 17,932
Asante, hii nimeipenda! Na kuwalipa je? Walipwe flat rate au per performance?Fanya kama saloon za kike, walipe per day, weka cashier, na hakikisha unaweka mfumo mzuri wa rekodi,kila mteja arekodiwe kwenye mfumo (QMS)
Itakusaidia kujua umehudumia wateja wangapi, huduma ipi inatoka zaidi,nani anafanya kazi kati ya vinyozi wako wote n.k
Lipa flat rate ila weka commission kwa best perfomerAsante, hii nimeipenda! Na kuwalipa je? Walipwe flat rate au per performance?
Hongera kijanaHabari zenu wakuu? Natumaini wote mpo salama na mnaendelea vizuri.
Nina mtaji ambao ninatarajia kuwekeza katika kufungua barber shop eneo la Msamvu, karibu na Stendi Kuu ya Morogoro. Mpango wangu ni kuwa na viti vinne vya kisasa vya kunyolea, pamoja na chumba maalumu cha scrub chenye vitanda viwili na sinki la kuoshea. Tayari nimefanya makadirio ya gharama zote zinazohitajika, ikiwemo AC, heater ya maji, partition za ndani, pamoja na kupata eneo la biashara.
Niliwahi kumiliki salon ndogo miaka iliyopita, lakini niliiuza kutokana na kubanwa na majukumu mengine. Mimi si kinyozi, hivyo nilishindwa kuisimamia ipasavyo. Safari hii nimejipanga vizuri zaidi. Pia nimepanga kufunga CCTV kwenye eneo la kunyolea, reception na sehemu nyingine muhimu kwa ajili ya usalama na ufuatiliaji wa biashara. Isipokuwa ndani ya chumba cha scrub, ambapo sitaweka kamera kwa sababu za faragha.
Sasa naomba ushauri wa wenye uzoefu wa biashara hii. Je, mfumo gani ni bora zaidi wa usimamizi? Niwaajiri vinyozi kwa mshahara wa mwezi, au nimkabidhi kinyozi mmoja asimamie saluni? Au kila kinyozi awe na kiti chake na anikabidhi makubaliano ya mapato kila wiki au kila siku? Pia nimekuwa nikifikiria kama ni vyema kuajiri receptionist au secretary ambaye kazi yake iwe kupokea wateja, kurekodi mauzo, kukusanya mapato na kusimamia hesabu, kisha vinyozi walipwe kwa wiki au mwisho wa mwezi. Sipendi mfumo wa kuwalipa kwa siku.
Kwa wenye uzoefu, hasa wa biashara za barber shop katika maeneo yenye shughuli nyingi kama Morogoro, mnanishauri mfumo gani wa malipo na usimamizi? Kama ni mshahara wa mwezi, kwa sasa ni kiwango gani kinachofaa kwa kinyozi mzuri? Na kama ni mfumo wa makabidhiano ya mapato, kwa kawaida kila kinyozi anatakiwa kukabidhi kiasi gani kwa wiki ili biashara iwe na faida kwa pande zote?
Karibuni sana kwa ushauri, uzoefu na maoni yenu. Asanteni.
Yes Mkuu hiyo hiyoAsante kiongozi, hii Catalunia ya Zanzibar ni.ile ambayo ipo Kiembe Samaki sheli?
Vinyozi hawakubali hiiLipa flat rate ila weka commission kwa best perfomer
Mimi sitakwepo hapo muda wote japo CCTV zitakwepo, hii kuwalipa kwa siku iwe flat rate au kwa idadi ya vichwa alivyonyoa kinyozi?
Shukrani mkuuHongera kijana
Sawa nitafanya research pia nikienda visiwani tenaYes Mkuu hiyo hiyo
Asante kwa ushauri wako lakini 50/50 percent HAPANA! Naweka mtaji (10 M+), nalipia rent, nalipia leseni, nalipa fee BASATA, nalipa kodi TRA, bill za maji, umeme. 50/50 HAPANA kabisa.Mfumo bora zaidi duniani kote wa saluni ni commission, mfano 40% kwa kinyozi na 60% kwako baada ya kutoa gharama za umeme na vitu vingine au mnawekeana 50/50 kama vifaa vingine vidogo vidogo wanajitegemea wao wenyewe. Hii itamfanya kinyozi ajue kuwa asipofanya kazi na yeye hatoishi vizuri mjini na akijituma anapata hela, ni njia nzuri kwa mtazamo wangu.
Kwanini hawakubali?Vinyozi hawakubali hii
Hapa kwa kila kinyozi kuelewana na kumlipa mdada fafanua zaidi maana ninaweka cosmetics kibao kwa ajili ya scrub na facial, steaming etc na scrub zipo za bei tofauti from 5K, 10K mpaka 30K per person.Kila kinyoz ataelewana na kumlipa mdada kama akimuosha na kumfanyia huduma mteja wake.
Ukisema 50/50 Ndio mfumo mzuri kwa sasa ndugu, hapo ww ni kulipa kodi tu. Bill ya umeme, maji na vipodozi ni juu yao. Kwa upande wa kwenye scrub kule manicure na pedicure vipodozi vya kwako na wao hawapati mgao wowote.Asante kwa ushauri wako lakini 50/50 percent HAPANA! Naweka mtaji (10 M+), nalipia rent, nalipia leseni, nalipa fee BASATA, nalipa kodi TRA, bill za maji, umeme. 50/50 HAPANA kabisa.
Haujanielewa vizuri naona, maana yangu ni kwamba kila mwisho wa wiki au mwezi, mnakuwa mnapiga hesabu. Mfano, saluni imeingiza milioni mbili, unakata kwanza gharama zako zote za mwezi huo mfano makadirio ya umeme, maji, kodi, na uchaji wa leseni/BASATA/TRA). Ile net profit inayobaki ndio mnaigawa kwa asilimia mlizokubaliana mfano wewe 60% au 70%, vinyozi 30% au 40%.Asante kwa ushauri wako lakini 50/50 percent HAPANA! Naweka mtaji (10 M+), nalipia rent, nalipia leseni, nalipa fee BASATA, nalipa kodi TRA, bill za maji, umeme. 50/50 HAPANA kabisa.
Ukisema 50/50 Ndio mfumo mzuri kwa sasa ndugu, hapo ww ni kulipa kodi tu. Bill ya umeme, maji na vipodozi ni juu yao. Kwa upande wa kwenye scrub kule manicure na pedicure vipodozi vya kwako na wao hawapati mgao wowote.
Ubarikiwe!Haujanielewa vizuri naona, maana yangu ni kwamba kila mwisho wa wiki au mwezi, mnakuwa mnapiga hesabu. Mfano, saluni imeingiza milioni mbili, unakata kwanza gharama zako zote za mwezi huo mfano makadirio ya umeme, maji, kodi, na uchaji wa leseni/BASATA/TRA). Ile net profit inayobaki ndio mnaigawa kwa asilimia mlizokubaliana mfano wewe 60% au 70%, vinyozi 30% au 40%).
Kutokuwepo sio ishu funga cctv then tafuta mdada anaeweza kuaminika , siku moja moja unatuma hata watu wakafanye huduma alafu na kiasi watakachotoa then we pitia daftari uone kama kimeandikwa kilichotolewa hapo hata wao wenyew wataogopa kwamba unafatiliaHapa nimekuelewa....Huku kwenye scrub nita-monitor vipi mapato? Maana sitokwepo hapo muda wote.
Amina Mkuu.Ubarikiwe!
Ndio maana serikali ya CCM inapata wakati mgumu sana kutekeleza mikakati yake ya kuwaondolea umaskini watz walio wengi.Kufanya kazi na watanzania ni kazi sana ndio maana umaskini hauishi