Ninafungua Barbershop: Je Vinyozi Walipwe Mishahara au Wakabidhi Hesabu?

Apo kuna mtu anatakiwa apate ajira na kuna watu wapate kibarua asa kama wewe hautakuwepo na mbaya zaidi ww huwez kufanya iyo kaz (muajiliwa ni mtu mmoja tu keshia na ndio unapaswa kumuamini kama meneja na kuwasimamia wengine kama vinyoz na hao warembo na kwa vinyoz na warembo hao kila siku wapate chao
 
Ila ungekua mwenyewe au mwenza wako au kijana wako ndio msimamiz ungekula bingo maana ungekua unakusanya mwenyewe mpatao bila kujal vinyoz na wahudum wengine mngekubalianaje
 
Nimeipenda hii ya kutuma mtu na kisha kuja kucheki daftari for verification ili kuzuia leakage za wizi

CCTV nitafunga lakini kwenye main room, reception na cashier, sijapanga kuifunga chumba cha scrub kwa sababu naona nitakuwa na violate privacy.

I stand to be corrected kama sipo sahihi!
 
Asante mkuu, ninachojaribu kufanya ni kuwa na consist employees....naamini nikimuajiri mtu na kumlipa kwa mwezi basi atalazimika kuwepo walau mwezi mzima mpaka alipwe mshahara ndipo afanye maamuzi yake ya kuondoka japo kwenye mkataba nitaweka kipengele cha muajiriwa kutoa notisi ya walau wiki moja au mbili kabla ya kuondoka.

Kuna muda vinyozi ni pasua kichwa nikiajiri kama vibarua wa kulipa kila siku, kuna siku anaweza akaja siku nyingine akapotea au wakapotea ghafla nikabaki na saluni bila vinyozi nikaanza kutafuta vinyozi upya. Sasa hapa nitafeli kwenye consistency ya biashara ukizingatia mimi sio kinyozi nina mishe zangu zingine.
 
Hapa nimekuelewa....Huku kwenye scrub nita-monitor vipi mapato? Maana sitokwepo hapo muda wote.
Scrub haikuhusu ww.
Inamuhusu Dada wa huduma na Kinyozi.

Vipodozi vya scrub hununui ww.
hata sabuni na mataulo ni wao.

Ww mpe hesabu kila Kinyoz kuwa kwa wiki unahitaji Laki 2.

Wao ndio wapambane.
Wadada ww wala hutakiwi hushughulike nao kabisa.
Kinyoz ndio atamtaguta na kumfundisha Mdada wa huduma.

Ww ni Kulipa Bill za maji na umeme tu.
Ila ndio unahakikisha kila wiki unakagua saloon yako.
 

Usiingilie hela za huku kwa scrub kaka.
Utapoteza Vinyozi na Wadada wa huduma wengi.

Wale hawalipwi. Wanajilipa.
Ww huhusiki nao kabisa yaani.

Na kwa kuwa hawalipwi , basi waconvice wateja wafanye huduma. Na wakifanya huduma . Dada anapata na Kinyozi anapata. Na kinyozi akipata na ww umepata.

Ukisema uwalipe mshahara. Hakuna mdada wa huduma atamconvice mteja kufanya scrub. Na kuwaosha wataosha ili mrad tu.
 
Nikiwa Zanzibar pale Catalunya ndio salooni yangu, ni kweli kuna dada ana mtako ndio anakusanya hesabu zote za huduma ulizofanya unalipa kwake anakupa na risiti. Wapo rada sana wale jamaa.
 
Kuwa na receptionist ni must!.

Huku niliko, 99.9 ya barbershops...wanalipa vinyozi kwa mwezi 200,000-250,00

Wanapatiwa chai asubuhi+ugali dagaa(hichi mm sikiiti chakula)...na mpishi alieajiriwa na ofisi
Ila hii biashara bila ya kuweka CCTV Camera itabaki kuwa ni ubatili tu,labda kama wewe mwenyewe utakuwa hukauki hapo salon...
 
Asante kwa ushauri wako lakini 50/50 percent HAPANA! Naweka mtaji (10 M+), nalipia rent, nalipia leseni, nalipa fee BASATA, nalipa kodi TRA, bill za maji, umeme. 50/50 HAPANA kabisa.
Hiyo ya asilimia mnakubaliana tu inaweza kuwa 60/40 au 70/30 hii ndio njia ambayo pande zote wanapata pesa ya halali.
Ngoja nikupe challenge fulani kwa mfano ukisema wakulipe flat rate kila siku let say 60k kwa siku haya kwa mfano siku biashara imewaendea vizuri wakapata 300k kisha wewe wanakupa 60k tu huoni kwamba hapo utakuwa umepunjika?
 
Biashara kama hiyo bila uwepo wa muhusika kiutendaji au kiusimamizi ,kwa sasa ni kama kucheza kamari...
 
Ukisema uwalipe mshahara. Hakuna mdada wa huduma atamconvice mteja kufanya scrub. Na kuwaosha wataosha ili mrad tu.
This is noted for action 💯 mkuu, hapa kwenye kujilipa mm napataje hesabu yangu? Nikimaamisha per kila kichwa kinachofanyiwa huduma ili mdada ajilipe na mimi nipate percentage kwa sababu vipodozi naweka mimi ili ku maintain consistency na quality.
 
Nikiwa Zanzibar pale Catalunya ndio salooni yangu, ni kweli kuna dada ana mtako ndio anakusanya hesabu zote za huduma ulizofanya unalipa kwake anakupa na risiti. Wapo rada sana wale jamaa.
Hapo Catalunya napita sana, huwa naenda kujaza mafuta pale sheli nikiwa zanzibar.....next time nitaingia kujifunza zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…