Ninafungua Barbershop: Je Vinyozi Walipwe Mishahara au Wakabidhi Hesabu?

Kwa siku wakapata 20k wakanipa 60k huoni watakuwa wamecompensate?
 

Achana na Hesabu.
Hesabu mwambie Kila Kinyoz akutumie 150k au 200k kila wiki, atume mwenyewe.

Chagua kinyozi mmoja ndio awe msimamizi wa Saloon, na ndio hii yeye atahakikisha vipodozi viko na vikiisha vinanunuliwa na wao wenyewe.

Ww unatakiwa kununua kwa mara ya kwanza. Baada ya hapo. Haununui ww. Wananunua Vinyozi.

Ni Kama ilivyo Magic shaving powder au spirit, au tissue na vile vidude vya kufunga kabla ya kuwekewa kitambaa.

Hivi ukivinunua wakat unafungua Saloon. Vikiisha haununui ww tena.

Kila wiki unaenda kukagua saloon yako. Na ww mahitaj yanayokuhusu ni Maji na umeme.

Sabuni, na vitu kama hivyo ni wao wanahusika na kununua. Wakiongozwa na kiongozi wao.
Ww ni kwenda kwa kushtukiza kukagua mazingira ya saloon yako na kama.vitu viko.

Pia Wadada wa Saloon usiwazoee kabisa. Yaan wale hawakuhusu. Wala usiwatafute ww. Vinyozi huwa wana connevction zao na watajua watawatoa wapi. Na hata kulipana watajua wenyewe. Na Usije ukawatoomb* wakasambaza maneno ukajiharibia Heshima yako 😊😊😊😊
 
Hiyo hela wekeza hata UTT huko. Bado kwa maelezo yako hutaweza kusimamia hiyo biashara na utafeli. Wanaosema uwakabidhi vinyozi biashara ni wapuuzi. Yaani nipigike kutafuta mtaji halafu kenge fulani aje nimkabidhi biashara kirahisi tu? Mkuu zingatia kwenye biashara hakunaga huruma. Biashara kama hiyo inatakiwa wewe mwenyewe ukusanye kila senti inayoingia na uwalipe mishahara. Kama mtu hataki aondoke. Vijana wanaojua kunyoa ni wengi sana na kazi hawana. Kama una ndugu wa kike au rafiki wa kike mnoko mwenye msimamo mweke akusimamie akusanye hizo pesa.
 
Salon ambayo huwa naenda kuna mhasibu anakaa hapo malipo yote anapokea yeye. Kuna vinyozi kama watano hivi, na bei ya kunyoa ni 5000. Kule upande wa wadada consumables zote ananunua boss na wanakubaliana kwa kila huduma mdada anachukua kiasi fulani. Mfano kufanya scrub 10,000, mdada anachukua 3000 labda na akipewa tip na mteja husika. Saloon nzima ina CCTV camera kiasi kwamba boss anaweza kuona kinachoendelea na huduma zote zilizotolewa na hivyo ni rahisi kufuatilia.

Salon nyingine ninayoenda mmiliki ni kinyozi pia hapo ila ana vinyozi wengine. Kinachofanyika pale ni kuwa vinyozi wengine wanakuwa na wateja wao na consumables zao na wao wanakubaliana na wadada wanaoosha na kufanya scrubs na massage etc. Ila wao wanakua wanamlipa mwenye salon kwa kutumia salon yake kunyolea wateja wao, gharama za umeme, maji, kodi ya jengo, TRA na bills mbali mbali applicable kwa salon.

Ukipata eneo zuri, vinyozi wazuri na wadada wazuri na wasafi, hii kitu itakupa hela sana mkuu na hela nyingi haiko kwenye kunyoa, iko kwenye kufanya scrubs, massage ya kichwa na shingo, kuosha miguu, kufanya steam, na vile vihuduma vingine vidogo vidogo.​
 

Ww ndio hujui hii biashara inaendaje.

Mishahara kwa vinyozi na wadada wa huduma atafeli vibaya sana.
Mapema tu KO.

Kumbuka saloon mpya sio kwamba ita peak muda huo huo. Itatumia muda kidogo had biashara ichanganye.

Na inaweza isichanganye.
Hapo ushaingia mkataba na Wafanyakaz kuwa utawalipa.

Ni bora uwapangie wakupe kias flan. Na unachunguza. Ukiona wateja wengi basi unakiongeza . Ukiona wachache unapunguza vinyozi.
 
Kama biashara huwezi kusimamia mwenyewe USIIFANYE. Kuna option siku hizi ya kuwekeza UTT huko.
 
Hapo kichwani mwako unaona kama ukifungua tu wateja hadi nje wakisubiri kumbe siku inaweza kupita nzima nzima hata mteja hamna na yote unayowaza kuhusu wahudumu ikawa kazi bure

Sisemi hivi kukukatisha tamaa ila usiwe na matarajio makubwa sana

Nje ya mada, hizi barber shop zinachochea ushoga na umalaya ( hii sio ya muhm sana)
 
Mimi sitakwepo hapo muda wote japo CCTV zitakwepo, hii kuwalipa kwa siku iwe flat rate au kwa idadi ya vichwa alivyonyoa kinyozi?
Kumbuka tu hizi CCTV camera zako zitakukosesha baadhi ya wateja wasiopenda kurekodiwa
 
Mkuu biashara yoyote ina ups and downs, good days and bad days! Lakini hii haikufanyi ushindwe kufanya projection ya mauzo yako na kufanya strategic planning.
 
Kama biashara huwezi kusimamia mwenyewe USIIFANYE. Kuna option siku hizi ya kuwekeza UTT huko.
Asante kwa ushauri wako ila usifikiri kila biashara unayoiona basi mmiliki ndio msimamizi.

Bakhresa ana biashara kibao unafikiri anazisimamia mwenyewe au kaweka wasimamizi na kubaki mmiliki? Ni namna unavyoweka mikakati na "systems" ndiyo husababisha biashara kufanikiwa.

Ukiona unaendesha biashara ambayo ukikosekana mwezi mmoja haiwezi kujiendesha basi ujue bado una safari ndefu. Na biashara nyingi za kiafrika ndio zipo hivyo ndo maana mmiliki akiumwa au kufa na biashara inakufa naye.
 
Hii ni point na nimekuelewa sana, hilo la kuanza na mishahara mwenyewe nimelifikiria kwamba biashara mwanzoni inaweza isi peak na ni kawaida ya biashara hivyo nilishaweka plan ya kuwa na akiba ya miezi mitatu ya mishahara kwa vinyozi pamoja na kuwapa daily allowance kulingana na kiasi alichoiingizia ofisi.

Kwa wadada wa kuosha nimeona nisiwalipe mishahara wajilipe kwa idadi ya scrub wanazofanya maana nikiwalipa mishahara hawatawashawishi wateja kufanya huduma.
 
Asante sana
 
Asante, hii nimeipenda! Na kuwalipa je? Walipwe flat rate au per performance?
Chukua mfumo huu. Alafu walipwe kwa performance in terms of percentage of income per person depending on the activities. Weka flat rate ya percentage. Amefanya kazi ya milioni 5 kwa mwezi rate Yako let's say ni 20%. Basi calculations zinahusika. Ukiweka flat rate per head kazi haitachangamka na pia kutakuwa na kutegeana. Walipwe kwa commission uone watakavyochakarika. Kwasababu different customer have different preference in terms of services provided and needed.l
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…