Ninahama CRDB; ni benki gani inayoweza kuwa mbadala bora kwa Dar es Salaam?

CRDB NI JANGA, kuna tawi pale Arusha linaitwa Usa-River kuna binti yuko kwenye mikopo anaitwa sijui Tarimo D anavyowanyanyasa wateja sijawahi ona. Ukiwa na mkopo wanakuchukulia km jambazi, ni km uliiba. Ikifika tar 22 kila mwezi wanafunga akaunti mpaka tar 27 kila mwezi. Km leo siwezi kuacces A/C yangu mpaka tar 27 kisa nina mkopo pale. Halafu makato hayana fomula, mtu una take home ya sh 1,200,000/ unakatwa mpaka 980,000/ kwa mwezi. Nimejaribu kufuatilia nimeshindwa. Nasuburi muda wao uishe kwa sahv naishi km shetani.
 
Nategemea kipindi hiki cha ukosefu wa ajira vijana waliotoka law school watanusa kitu😊😊
 
Chupi za VIP unazifahamu mhenga?
 
Hata mi kwa sasa Equity ndio nawaelewa!
Uwe unatumia simbanking na atm zingine.

Hao crdb mi sina hamu nao, mwaka huu huu waliwahi kunifanyia mauza uza ambayo sitayasahau, VISA card yangu ilinigomea na ndio acc yangu iliyokuwa na hela na nilikuwa mbalii☹☹ yani ilinibidi nikawatafute hao crdb hadi twitter maana ndio niliona wanarespond haraka, napo wakasema niwatumie email ila mpaka walipokuja kurespond ilichukua muda na haikuishia hapo iliwachukua siku nyingi sana wao kutatua tatizo langu. Kiasi kama nisingekuwa na namna nyingine basi ningeadhirika mchana kweupee,

Toka hapo nikaanza kuithamini acc yangu ya Equity ambayo nilikuwa naidharau mno, kwanza nilikuwa naiwekea tu kama 10,000 kwa mwezi ili tu iwe active, lakini iliniokoa sana
 
Ningehamia huko, shida ni matawi yake sio mengi.
Hawa CRDB wapuuzi kweli
 
Online transactions waone ABSA hutojuta
 
Mkuu nenda Amana bank utanishukuru Mimi Niko nayo nina miaka 8 sasa nina account benk 3 lakini naona Amana anawazidi hawa wote kwa huduma murua yaani unahudumiwa Kama vile uko nyumbani.
 
Poleni sana... Hakuna Bank yenye unafuu...
 
CRDB siku hizi ni SACCOS, si benki ya kuaminika tena.
Malalamiko ya wengi ni mafoleni yaliyopo, na customer care mufilisi.

Majuzi wameniambia eti nikahakiki particulars zangu.
Nikawuliza nini kimebadilika?
Wakasema we njoo tu!
Nikawaambia siwezi kuja hapo kwa hiari kukaa masaa mawili kusubiri huduma, na nitaifunga hiyo account!
Niliyekuwa naongea naye akashtuka na kusema si hivyo!
Nikafikiri , hawa wanafaya mambo kwa mazoea, wana email yangu na wana simu, kama kuna mabadiliko si watuemie email?

CRDB iliondoka na Kimei!
 
Hivi KWA nn makato ya kibank si rafiki sanaaa,Yani kama wanatuvizia wateja tu tufanye service Kisha ujistukie umelimwa fedha ya maana,KWA nn wasiweke wazi ukifika bank una kuta kila kitu kiko wazi,ama wakutambulishe huduma unayo taka kufanya cost yake ni kiasi kadhaaa.

Mfano NMB,Atm card zao zipo local sana yani ukitumia sana inaanza kusumbua ktk atm,ukiuliza simple wanakujibu ni utunzaji,Ajabu Atm card naweka kwenye wallet KWA bank zote ninazo tumia,ila wao tu ndo haipiti miaka miwili naenda kubadilisha Card,afu makato ya kubadilisha ATM card yapo juu,Baada ya kuomba Atm Kisha uchukulie dirishani ,wanakulima mpaka unakuja juta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…