Ninahama CRDB; ni benki gani inayoweza kuwa mbadala bora kwa Dar es Salaam?

Nunua kibubu kwa fundi Maiko au kwa Mangi u manage pesa zako mwenyewe(just joking)
 
zamani ukiweka fedha bank wanazifanyia bishara na kukuwekea interest angalau ya kufanya hela zako zisipungue baada ya makato yao, tofauti na sasa ukiweka laki mbili kwenye account baada ya miaka mitatu unaweza kuta zimebakia 140,000
Nahisi kuna kitu hakipo sawa kwenye makato kwa wateja
 
Equity kama upo Darisalama ni bank bora sana. Lakini mkoani huwezi kuimudu! Equity nimetumia sana ni bank nzuri hakuna makato ya hovyo kama CRDB. CRDB kila mwezi hunitumia statement Mara maintenance 300, nini fees 1500, kitu cha mtume 2000, ni wizi sana
 
Siku moja nilidownload App ya CRDB nilijua ni mambo ya Equity bank, unaingia bure, unatoka bure. Due! Kumbe ukiingia tu wanakata JERO sijui. Equity App ni bure. Muda wote unachungulia salio lako bando lako tu
 
Siku moja nilidownload App ya CRDB nilijua ni mambo ya Equity bank, unaingia bure, unatoka bure. Due! Kumbe ukiingia tu wanakata JERO sijui. Equity App ni bure. Muda wote unachungulia salio lako bando lako tu
Kumbe ukiingia tu kwenye app wanakata hela?? Hii sikuwa najua kwakweli
 

aisee pole sana
 
CRDB Majambazi msiweke pesa huko, wajitathmini yawezekana kunawafanyakazi wa humo wameanzisha mchezo mchafu, juzi kuna mtu hajakuta hata cent kwenye account yake.

Wenye account CRDB mkakague account zenu mapema, kisha muamishe pesa zenu mabenki mengine. Benki nzuri ni NMB Bank.

Serikali iwachukulie hatua za kisheria CRDB Bank, kuna mchezo mchafu umeibuka wa kuiba pesa za watu wanadanganya makato.
 
Hakuna bank salama. Hakuna atakaekuwekea pesa yako Bure. Unataka yeye akale wapi. Apande daladala? Wese je. Kwa ufupi anayehangaika na benki anapteza raslinali pesa na muda kuhusu pesa bulky je huna cha ikuzifanyia? Hakba tafuta njianngine kuweka savings sio lazima benki. Kama ni mamilion kwa nn usiifanye fixed sasa
 
Fanyeni utafiti kwanza.. Halafu muwe makini na aina za akaunti mnazofungua benki.

Pia ukisoma alama za nyakati utagundua CRDB ipo under sabotage, haiwez kuwa na huduma nzuri kwa sasa
 
nlfikiri watu wanaongea tu kumbe haya mambi ni ya kweli baada ya mimi kwenda leo kutoa hela hapo ninunulie familia tukuku na soda.. aisee ndani ya tar 10 mpak 24 wamenikata charges 40k.. somthing is wrong.. na hii ndo itakua transaction yangu yamwsho...nimekomba kila kitu
 
Mh. Check statement n branch desk watakufafanulia.kuna card fees kwa mwaka=zinanzia 19800, 29800 nakuendelea ikiwa ni mastercard yakawaida/visa 19800 kwa mwaka,izo platnumz infinity and so on ndo zinaanzia 29800 kwenda juu
 
Pole sana mkuu. Mi mwenyewe jamaa wananipiga panga kila mwezi. Mungu jalia mkopo wao ukiisha wataona manyoya tu
 
Kadi yangu ya CRDB ilipotea, eti kupata nyingine sh 23800 niliwahama siku hiyo hiyo
CRDB hawako open kwenye gharama za huduma zao.

Bot wanatakiwa kufuatilia jinsi mabenki wanavyotoza wateja wao wanapowahudumia. Unfortunalely, siku hizi toka Ndullu afariki Bot imezoorota sana hata section ya Bank supervision hawafanyi kazi yao inavyostahiri na ndio maana benki kama CRDB wanatengeneza faida kuwa kutokana na charges na sio kwa kuwakopesha wateja!!Something has to change.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…