Ninahisi mpenzi wangu ana mwanaume mwingine

Ninahisi mpenzi wangu ana mwanaume mwingine

Mimi Sisyphus leo, nimeliona joto la jiwe ... mtu nilimuamini ameanza rasmi kuonyesha MAKUCHA yake ... ni miaka minne sasa niko na huyo mwanamke, ni muda mrefu sasa mwenzangu alikua anaomba ndoa mara nyingi sana..nimejaribu kumuelewesha asubiri tujipange kwanza (na najipanga kweli sio uhuni) .. maana tushamleta na mtu duniani, naona sasa muda wa uvimilivu wake umaenza kufika kikomo ....

Story inaanzia kati, leo alienda kutafuta chumba mana kuna short course alikua anataka kusomea kwahiyi ikambidi akatafute chumba sasa amefika dalali akamwambia asubiri mama mwenye nyumba arudi kwahiyo itambidi akae masaa matatu kumsubiri... akanipa taarifa mimi nikaona hakuna logic ya kumsubirisha mana anakoishi(siishinae) amecha mtoto ( 1.9 year) basi bwana nikampigia dalali , dalali akaanza kuropoka “ ooh bro msiondoke mana mkiondoka hiki chumba mtakikosa” ... la haula ikabidi ni muulize nisiondoke na nani, akajibu “ we si yule jamaa mumewe ambae uko nae” bila kufikiri mara mbili nikajibu hapana mimi ni mumewe ila sipo huko.

Dalali akaanza kuuma uma maneno mwisho akasema aaah basi ngoja kidogo nitaku-check ... nikamuambia embu subiri nipe maelezo kidogo huyo mwanamama amekuja na nani? ... kwa sababu alishaanza ikabidi aseme amekuja na jamaa akamtambulisha ni mumewe ( mimi nilipo ikabidi nikae chini kwanza ) ... lakini dalali akaendelea itakua basi boda... nikamwambia sawa fatilia hilo swala la mama mwenye nyumba kwanza.

Nikatulia kwanza alafu nikamtafuta vipi mwenzangu leo umeenda na nani? Mara ooh sijaenda na mtu mara oohh ni boda ndiye niliyemtambulisha mume wangu ... kwa kifupi taarifa aliyonipa dalali ni kwamba walienda wawili na aliwaacha wawili ukiacha boda.
Ikanibidi nimuulize vizuri boda ndio unamtambulisha mumeo ,? ( ...ghafla akaanza ule mchezo wao anakurudishia maswali kwani wewe huniamiani blah blah).

Baada ya haya ikabidi nianze ku-analyse wapi nilikosa umakini mpka nikashindwa kuona hili kwa hupitia uwezo wa roho mt. nikaanza kuona vingi nilivyokua sitilii maananini kwanza AMEACHA KUSISITIZIA NDOA , pili amepunguza wivu na anakaribia kuacha kabisa , tatu amekua na majibu ya mkato na kujifanya anajiamini( now days ana-vihela mana kuna-business nilimpa akaweza ku-make kwa kipindi kifupi).

Nne .. kuna mambo anayafanya mwenyewe mwenyewe na hua tunashirikishana kila kitu ila nimeanza kuona gap upande wa pili
NB: huyu mwana-mama nimefanya nae vitu vingi sana hata kipindi na mpiga tarehe anafaham hasa nini nilikua nafanya, nilivyofanya na naendelea kufanya . MAAZIMIO shetani amenijia na ujumbe wa kumpiga chini mapema maana nilivyokua nafanya nafanya kwa ajili yetu sote isingekua hivyo mi ningeenda zangu SHULE KITAAMBO nikabukue zangu masters ya masimulizi...

WAJAMENI ...nipeni ushauri mana shetani ananizonga na mawazo yake... ni chukue hatua gani easy way , hard way Au mixing
Kijana unakaaje katik mahusiano na Mwanamke miaka minne bila kumuoa ? Kama huna mpango wa kuoa tulia ukiwa tayari kuoa tafuta Mwanamke uoe.

Huyo Mwanamke amejiongeza ameona hakuna muelekeo,kwahiyo usimlaumu sana.

Ushauri wa kiutu uzima na wa busara,kama umeshajiridhisha na hilo,achana nae aendelee na maisha yake,ukiwa tayari kuoa tafuta mwanamke oa. Siyo mnakaa kwenye mahusiano kijinga jinga tu.
 
Ulifanya vibaya Sana mpka ukapata jina la kijana wa hovyo kabisa

Ni lazima ujiandae ndiyo uoe siyo utafute mwanamke harafu ndiyo ujiandae.


Anataka ndoa na mimba hiyo alipata kama mtego na yawezekana siyo wako , huyu mtoto anaweza kuw na Kadi tatu za kliniki moja ya jina lako mbili za majina ya Baba wengine .

Maana yeye anahitaji ndoa si mbali Sana anaweza kuolewa na mwanamme mwingine atakayekuwa tayari hata kama utamtema , kumbe naye ashakutema hapo ndo unajua Ngoma draw.
Yaani mtoto sio wake... anadanganywa kadi za clinic... anachapiwa nje... na bado mnamlazimisha ndoa na huyo malaya??
 
Piga chini, kitendo cha kumtambulisha mwanaume mwingine kama mume wake maana yake ushakosa mwana na maji ya moto
 
Hii kujipanga haijawai kumuacha mtu salama kama uliyenaye si mtu sahihi
 
nashindwa kabisa kuelewa vijana wa siku hizi kupenda kutumia neno 'basi bwana'. Hili neno si wanatumia wanawake?
 
Shida sio kuoa ... ANAAMINIKA,?
Kwani we huna maamuz binafsi mpaka hapo ulipofikia.
Kwanza umeshapata ukakasi juu ya mwanamme aliye tambulishwa,
Pili kashapunguza baadhi ya vitu kwako kama unavyodai, kuanzia maongezi mpaka vitendo. Mpaka hapo pashakucha ushajua wapi panavuja swala la kumuacha au kutomuacha liko juu yako. Nijuavyo mapenzi hayashauriki, kuna watakwambia achananae kwa full evidence but value yake unaujua ww, pia kuna watakaokushauri mrudie alihali tayari ulisha tia mashaka juu yake.
NB. Swala la kumuacha au kutomuacha liko juu yako.


Sent from my SH-02J using JamiiForums mobile app
 
Ndoa sio majaribio! Hakuna mwanaume yupo tayari kuoa tabia chafu!

Wewe mwenzio kaja hapa anaugulia moyoni sababu anampenda mwanamke wake halafu wewe unamwita tabia chafu? Hivi unajua nafsi yake ingekua inawaza hicho unachowaza wewe asinge andika aliyoyaandika?

Mwanaume ndio mwenye maamuzi ya kuoa na kuchagua mke, kwa maana hiyo Kuoa tabia chafu kunaanzia kwenye utayari wa mwanaume kuchagua tabia chafu na kufanya maamuzi ya kuishi na hiyo tabia chafu hadi kuamua kuleta kiumbe duniani na hiyohiyo tabia chafu.
 
Unadhani ndoa ni ya kufanyia majaribio? Kwani kuzaa watoto ndio nini? Yaani niteseke na ndoa kwa kuona mke wangu analiwa nje kisa watoto? Wanaume lazima tujue tabia kwanza tujiridhishe
Tabia itakuchukua muda gani kujiridhisha?
 
USIMDANGANYE.


JAMAA UAITHUBUTU KUMUOA HUYO DEMU ET KISA UMRIDHISHE.

USIMUOE ET KISA MMEZAA NAYE MTOTO


ACHA MARA MOJA.


POTEZEAA.

MAADAM KESHAKUPA MTOTO.....NIAMIN ATAKUJA SIKU MOJA AKILIA NA KUKUBEMBELEZA[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mwanaume ndo alianza kutoeleweka ndo maana mwenzake akatafuta kidumu. Akimuoa tu akajihakikishia yy ndo mke amemaliza kazii
 
Mwanaume ndo alianza kutoeleweka ndo maana mwenzake akatafuta kidumu. Akimuoa tu akajihakikishia yy ndo mke amemaliza kazii
Kwann huwa hamna uvumilivu?


Je Yeye kukuchelewesha kuitwa Mke ili hali tayari mmeshazaa, kunakupa sababu ya Kuchepuka??

Au kwako bora lipi. Kumuweka wazi ili uendelee na mahusiano mapya?

Au ndio nanyie siku hizi mmeamua Kuwafanya wanaume "Viporo".


Ikiwa nikweli demu sasa ana mtu mwingine.... Basi jamaa ampotezeee.. Siku zaja ambazo Demu atarudi kwa kasi .
 
Yap tukiongelea ndoa tukaona haieleweki tunatafuta pengine
Kina dada acheni utapeli..mwambie basi huyo mwanaume kuwa unaondoka kwake rasmi,usiendelee kula vyake huku unasubiri mambo yako yakae sawa upande mwingine.

This is not right Dina.
 
Back
Top Bottom