Dah pole kiongozi ,Kuna kitu nimejifunza sana kwenye maisha ,
Kuwa makini sana na watu hawa japo sio wote wako hivyo ,ila baadhi wanamatatizo hasa .
waangalie sana wanawake walioachika ,kabla ya kutaka kumuoa chunguza kwa makini ,kipi kilimshinda kwenye ndoa ya mwanzo ,huwenda ukapata cha kujifunza maana sio wote wanayoyazungumza kama walinyanyasika au kutendwa na wanaume ,wengine wao ndio sababu na mwanaume ameamuwa kubwaga manyanga.
pili mwanamke Alozaa bila kuolewa ,,hapa napo nieleweke sio wote ,ila wapo baadhi wenye kushindikana kuolewa kwa tavia zao ,mpaka mtu akamzalisha na kusepa,na wapo ambao wao walikuwa wazuri tu ila hawakupata mtu sahihi .
Tatu Mwanamke kama atafikisha umri mkubwa na bado hajaolewa au anapata wa mwanaume ila hamuowi ,
Dizaini ya hawa watu kabla hujafanya maamuzi ya kuwa na mahusiano nao ya kina ,kwanza fanya uchunguzi wa kina na ujiridhishe ,huyo unayetaka kuanzisha nae mahusiano ya kweli ,yuko katika hali gani ,
je amekumbwa tu na bahati mbaya za kilimwengu ikapelekea kujikuta mikononi ,mwa wanaume ambao si sahihi ? Au yeye chanzo cha tatizo ,
Pana kisa kimoja ,pana dada mmoja wa mjini hasa na maarufu ,Alitokea kunipenda hasa na paka kutamani nimuowe hata mke wa pili ,
Ila nilichomwambia. dunia yako na yangu ni tofauti,Ila akalazimisha kuwa anaweza kuishi hali yeyote ,na akawa analalamika hakupata mwanaume sahihi n.k ,kwa jinsi anavyongea unaweza ona kweli ,huyu hajapata mwanaume wa kweli ,lkn kwa kadri nilivyomsoma tabia na kuwa nae karibu tu kama rafiki ,nikagundua huyu mtu why hawezi olewa na kuwekwa ndani ,au kwann wanaume huchemka kumweka ndani kama mke ,zaidi ya kumchezea ,
Tatizo lao wengi huwa hawajitathmini na kupitia baadhi ya kasoro zao na kujirekebisha ,badala yake ,ni watu wa kutupa lawama tu ,na kujiona kila siku wao wanaonewa au kila mwanaume anayempata si sahihi ,Ila wanajisahau kuwa wakati unaona mwanaume si sahihi je wewe uko sahahi?.
. Ajabu wanawake wengi atakwambia anataka mwanaume mwenye hofu ya mungu ,ila cha kujiuliza wao wanayo iyo hofu ?
Na je akimpata atakubali kufata misingi ya mungu au atakubali kuongozwa katika kumjua mungu?
jibu wengi wao wanahubiri wasioyatenda ama kuyataka ,
MWISHO NI KUSHAURI NDGU YANGU ,Fanya maamuzi sahihi na kwa wakati sahihi ,Na hakikisha linapokuja swala la maamuzi tumia akili kuamua ,na kamwe usiuwache moyo wako ukafanya maamuzi