Ninaiomba Serikali ifungue mtandao wa JamiiForums

Sio ombi bali ni lazima, hakuna kuomba haki ni kitu cha lazima, unapoomba mana ukubaliwe au ukataliwe, lkn haki haiombwi ni kitu cha lazima.
 
dogo hii ni serikali sio dada wa kazi unamuendesha unavotaka, elewa neno MAMLAKA hivo make sure unajitahidi kutumia busara sehem zote
Hivi mnapotetea kila kitu huwa mnamaanisha nn? Kwahiyo hakuna kitu serikali inakosea? Acheni hiyo tabia, hamjengi mnabomoa.
 
Kwanini uombe ifunguliwe? Walikwambia imefungiwa kwa kosa gani baada ya zile siku 90? Haki haiombwi, kama hawawezi kuitendea haki JF basi waache tutaendelea kuingia kwa VPN na hakuna kitachoharibika. Nchi ya wapumbavu.
 
Kuomba huambatana na masharti lukuki ambayo wakati mwingine hupora uhuru wako. Haki inadaiwa haiombwi
 
Hivi mnapotetea kila kitu huwa mnamaanisha nn? Kwahiyo hakuna kitu serikali inakosea? Acheni hiyo tabia, hamjengi mnabomoa.
inakoseaga vizuri tu na haina shida kukosolewa, shida inakuja HAKI inatumika kuhalalamisha utovu wa nidham, tiktok ishafunguliwa
 
Wasiifungulie mbona tunaingia kama hivi na maisha yanasonga..!!

Hao watu ni wauaji hukuona interview ya Max aliposema walimpigia simu na kumtishia kumuua??

Anza kuwakemea kwanza na kuwataka waachie jukwaa liwe huru hii nchi ni yetu sote. Kila mwananchi anahitaji haki ya kuishi na kuongea kwa uhuru..!!

Na wewe uache uchawa this is 2026 ushakuwa mtu mzima tafuta pesa kwa jasho sio hizi blah blah za kung’ata na kupuliza..!!
 
Asichokijua serikali haramu inataka Max awalambe miguu ili wapate access ya kupewa taarifa za member ambao wanaanika madudu yao..!!
 
Kwako maisha yanasonga ila Jf inaathirika na hii ban
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…