Ninaiomba Serikali ifungue mtandao wa JamiiForums

Ninaiomba Serikali ifungue mtandao wa JamiiForums

Serikali ipi hiyo unayoiomba.?

Mosi haina uhalali wa kuongoza maana haikuchaguliwa.

Pili amri ya kufungia JF ilikua haramu wakicite Polepole kuongelea kashfa ya mgodi wa makaa ya mawe ilichapishwa humu bila mizania ya habari kwamba Rostam hakupewa nafasi ya kujibu lakini kiukweli Rostam alistage interview na Tido Mhando , sasa je baada ya hapo Tido Mhando alimuomba Polepole mahojiano?

Pia mapicha ya lile bonge la silaha walipiga wao huko ikulu wakasambaza wao picha kuletwa humu jukwaa ndio likafungiwa kosa la JF liko wapi?

Max alisema walifanya uvamizi na CCTV footage anazo ila Msigwa anasema walipeleka wito , JF ikafungiwa pia bila kupewa nafasi ya utetezi akina Msigwa wanaouita mizania ya habari.

Tatu amri haramu ilikoma tarehe 6 mwezi jana ila bado imeendelea na utekelezaji kimya kimya .

Hao mnaowaita viongozi ndio wamefungia X , ClubHouse, Tiktok kimyakimya na wao wanaingia kwa VPN ambayo walisema ni kosa kisheria kutumia.

Na bado utakuta Misigwa anakuja kuchungulia humu na VPN ambayo wanasema kutumia ni kosa.

Account ya bunge lililotunga sheria hizo za kipuuzi nayo inatweet kwa VPN kutokea Hongkong.
Screenshot_20251211_065438_X.jpg
 
Kwako maisha yanasonga ila Jf inaathirika na hii ban
Inaathirika nini?
Hii ni Jamii Africa, kokote inachana mawimbi.
Mnaothirika ni nyie miungu watu mnaoteseka kunyamazisha kila mtu anayekuwa kinyume na nyie..!!

Ungekuwa na akili usingeshabikia viongozi haramu.

Nikuulize swali, serikali haramu imeifungia JF na bado nyie machawa wake mnaendeleza porojo zenu. Je, hauoni kama kama ni uonevu na mabavu yanatumika kufunga raia na biashara zao midomo?

Kumtishia raia uhai wake ni sawa sababu hawapendi kukosolewa?
 
Humu nyie wajuaji wengi, mkiupromote sana huu mtandao ni anguko lao.

Wanachofanya ni hizo funga, fungua ili msijikusanye wengi mkawa tishio.
 
inakoseaga vizuri tu na haina shida kukosolewa, shida inakuja HAKI inatumika kuhalalamisha utovu wa nidham, tiktok ishafunguliwa
Kwahiyo wewe ulitaka raia waombe haki na sio wapewe haki? Uliona wapi haki inaombwa? Huu ujinga ndiyo umetufikisha hapa, ujinga wa kusema eti naishukuru serikali kwa kutujengea kitu hiki mara kile, mwishowe wanajiona wanatusaidia badala ya kutimiza wajibu wao, serikali haiombwi ni lazima wafanye vile raia wanataka, mana serikali imeajiriwa na wananchi, so ni lazima kufanya kile wanaambiwa na wananchi.
 
Tunachowaambiwa ni lazima wafanye, wasipofanya watakuwa ni wakaidi na kinachofuata ndiyo hiki unachoona maandamano yasiyokuwa na kikomo mpaka wajitambue kwamba lazima wafuate kile ambacho sisi tunataka.
 
inakoseaga vizuri tu na haina shida kukosolewa, shida inakuja HAKI inatumika kuhalalamisha utovu wa nidham, tiktok ishafunguliwa
Utovu wa nidhamu unatokea pale muajiriwa anapojiona Boss, wananchi ndiyo maboss mnatakiwa mjue hivyo, hili litasemwa hata mkiua wananchi wote bado mawe yatawakumbusha hili.
 
Kheri ya Mwaka Mpya!

1. Kwa heshima na taadhima. Ninapenda kuchukua nafasi hii.

2. Kuiomba serikali iufungulie mtandao wa Jamiiforum ili mambo mengine yaendelee.

3. Jamiiforum ni moja ya mambo ambayo serikali ya Tanzania inaweza kujivunia kwa wananchi wake.

4. Malumbano, mivutano na migogoro iwe ya kisiasa au kijamii inaweza kuweko lakini isiwe sababu ya kurudisha jitihada na nguvu zinazoipaisha nchi yetu katika Nyanja kama za kiteknolojia na kidijitali.

5. Watu wengi ikiwemo serikali imefaidika na uwepo wa jamiiforum kuanzia kwenye elimu, habari, maarifa na mawazo mapya, ajira, miongoni mwa mambo mengine.

6. JF kupitia anonymous imesaidia serikali na vyombo vya usalama kupata baadhi ya data ambazo ingetumia nguvu nyingi kuzipata.

7. Ingawaje zipo changamoto za kashfa au tuhuma. Lakini suala hilo lisiwe sababu ya kufungiwa kwa mtandao mzima.

8. Naiomba serikali ifungulie mtandao huu. Hakuna haja ya hasira, chuki, kukomoana, kutunishiana misuli. Kuonyeshana ubabe.

9. Ukubwa ni busses, hekima, unyenyekevu kama sehemu ya kuonyesha njia ya Wema na kuwa mfano Bora wa UTU.

10. Mwaka 2026 mwaka wa UTU WA KALE.
11. No hate. One nation one destination.

Mungu awabariki.
Kwa walio Morogoro. Jioni tutakuwa Pale mjini. Kufurahia mwaka 2026.

TaikonMaster
Kwa sasa Soko la Kingalu, Morogoro Mjini
Kufanya hivyo ni sehemu ya juhudi za mchange na ilewizara changa zaidi kulidunisha taifa kwa faida ya familia chache!
 
Utovu wa nidhamu unatokea pale muajiriwa anapojiona Boss, wananchi ndiyo maboss mnatakiwa mjue hivyo, hili litasemwa hata mkiua wananchi wote bado mawe yatawakumbusha hili.
Life is unfair, lazima kue na madaraja bila hivo life is useless! tatizo huanza pale uko daraja la kawaida na unaishi kama dunia ni yako, ipo sku patakuponza
 
Kwahiyo wewe ulitaka raia waombe haki na sio wapewe haki? Uliona wapi haki inaombwa? Huu ujinga ndiyo umetufikisha hapa, ujinga wa kusema eti naishukuru serikali kwa kutujengea kitu hiki mara kile, mwishowe wanajiona wanatusaidia badala ya kutimiza wajibu wao, serikali haiombwi ni lazima wafanye vile raia wanataka, mana serikali imeajiriwa na wananchi, so ni lazima kufanya kile wanaambiwa na wananchi.
hakuna kitu kinaitwa HAKI duniani, wote tunaishi kwa madaraja, katika siasa maneno kama Haki, wananchi ndo wenye nchi, ni kauli za siasa na hazina uhalisia wowote katika maisha! ukitaka kuheshimika lazima uwe na nguvu kisiasa ama kifedha, leo hii marekani anaendeshwa na israel kwa sababu ya nguvu, wayahudi wanaendesha uchumi wa marekani hivo basi hata gaza walalamike miaka 1000 uhalisia ni HAKI ni kibwagizo kwan mkono mtupu haulambwi, siku zote tegemea mkiwekwa wawili wewe na mo dewji na mmoja anatakiwa kusikilizwa basi mo atakua wa kwanza, Jitahidi kuishi kwa uhalisia
 
Tunachowaambiwa ni lazima wafanye, wasipofanya watakuwa ni wakaidi na kinachofuata ndiyo hiki unachoona maandamano yasiyokuwa na kikomo mpaka wajitambue kwamba lazima wafuate kile ambacho sisi tunataka.

Ni sawasawa kabisa.
Lakini huwezi kuagiza au kutoa amri kama huna nguvu au mamlaka.
Kwa sababu unapoagia unakuwa na option moja tuu kwamba akikaidi utatumia mamlaka au nguvu ulizonazo
 
Ila mtani upo kwenye stage za mabidiliko ya kuwa KIAZI kwanini lakini bwashee?

Mtani. Maisha hayahitaji mbinu Moja ya kukariri.
Hata shetani kuna wakati itampasa awe malaika ili mambo yake yaende.
Halikadhalika Malaika kuna wakati huwa shetani. Usisahau kanuni Mtani.
 
Back
Top Bottom