Ninaishi KIBAHA, Shughuli zangu ni Kariakoo. Lift inalipwaje, kama Asante?

Ninaishi KIBAHA, Shughuli zangu ni Kariakoo. Lift inalipwaje, kama Asante?

Akiingia sheli nawe jiongeze,uongezee hela ya mafuta
Ningekuwa nina gari nisingeruhusu aniongezee hela ya mafuta...kuruhusu afanye hivyo maana mwenye gari atakuwa amejiondolea uhuru wa gari lake...aliyechangia mafuta anaweza kuona ana haki ya hilo gari kwa vile tu amechangia mafuta!
 
Siku moja mwambie apitie petrol station tia mafuta ya 70k
Mengi sana hayo,akiweka hata ya 20K kwa baada ya miezi miwili ataonekana bonge la mtu.

Unadhani huyo anayemzungumzia amewapa lift wangapi but hakuna hata mmoja aliyewahi kuwaza kama anavyowaza mdau hapa.
 
Ila ndugu huna aibu kabisa. Mimi kupanda lift ya mtu kama hivyo ulivyo wewe itakuwa suala gumu sana. Mimi ninakushauri anza kupanda daladala kama ilivyokuwa mipango yako mwanzoni ili ubakiwe na ka-heshima. Ona aibu aisee. Hata kama ikibidi lift iwe mara chache kwa kulazimika.
 
Habari kwako wewe

Ninajirani anafanyakazi mjini. Anagari mimi sina inafahamika kitamaduni mtanzania humsaidia mwenzie anapoona inafaa.

Nitamlipajelipaje mtu anayenipa lift kila siku au mara mbili kwa wiki, mara nne tano kwa mwezi. Na najua nauli yangu inabaki mfukoni.

Mimi kama mtu mzima huyu mtoto amefanikiwa kupata usafiri.

Wenzangu tunaopewa lift mnalipaje fadhila?


NAOMBA MWENYE GARI ALIYEKWISHA TOA LIFTI NIAMBIE KAMA UNAJISIKIA VBY EE KUTUBEBA?
Wewe na huyo anayekupa lift jinsia zenu zikoje
 
Mimi naona tu niwe napanda Bajaji au daladala kuliko kuzamia zamia magari ya watu. Japo Chanika na Posta ni parefu ila bora nikomae hivyo hivyo.
Unajitungisha story za uwongo njia nzima unaongea wewe kimbembe mkutane na foleni kimya kinatawala maana story zimeshaisha hujui useme nini tena sasa unajikuta kushuka unataka kubaki unataka.
 
Unajitungisha story za uwongo njia nzima unaongea wewe kimbembe mkutane na foleni kimya kinatawala maana story zimeshaisha hujui useme nini tena sasa unajikuta kushuka unataka kubaki unataka.
Kwa mfano mimi huwa napata sana changamoto.
Huwa siwezi kupiga stori na mtu nisiyemzoea. Halafu unakuta mtu anakulengesha mjadili habari za serikali, hapo ndipo huwa napata mtihani zaidi.
 
Siku moja nilipewa lift na jamaa flan,nilipofika nikamwambia "shukrani"
Akanambia sema JAZAKALLAHU KHEIR (MWENYEZI MUNGU AKULIPE MEMA).
 
Katika kitu ambacho sipendi, ni mtu kuniwekea mafuta, inanifanya kama awe ananidai. Ni Bora uongee nae, kwamba naomba uwe unanipitia, na nichangie kiasi flani kwa week au mwezi. Ongea nae kiume. Usiseme tu tupitie kituoni apo tuweke mafuta bila kuongea nae.
Hii imekaa kiume zaidi.
 

Attachments

  • 1790277059497.png
    1790277059497.png
    1.4 MB · Views: 5
Katika kitu ambacho sipendi, ni mtu kuniwekea mafuta, inanifanya kama awe ananidai. Ni Bora uongee nae, kwamba naomba uwe unanipitia, na nichangie kiasi flani kwa week au mwezi. Ongea nae kiume. Usiseme tu tupitie kituoni apo tuweke mafuta bila kuongea nae.
Na hilo ombi lake lazima likataliwe, hiyo inakuwa kama sadaka tu in case siku sijakubeba hata nisikuwaze wala nini
 
Na hilo ombi lake lazima likataliwe, hiyo inakuwa kama sadaka tu in case siku sijakubeba hata nisikuwaze wala nini
Hakika. Akinunua mafuta atamtoa mchezoni bwana Mdogo.
 
Kama we ni mwanamke ye mwanaume mpe papa au kama upo design ya ommy dimpoz basi mwambie akupige miti.(In dudubaya voice)
 
Ila ndugu huna aibu kabisa. Mimi kupanda lift ya mtu kama hivyo ulivyo wewe itakuwa suala gumu sana. Mimi ninakushauri anza kupanda daladala kama ilivyokuwa mipango yako mwanzoni ili ubakiwe na ka-heshima. Ona aibu aisee. Hata kama ikibidi lift iwe mara chache kwa kulazimika.
Mnaopewa lift mbona mnajishtukia sana. Hakuna aibu yoyote bana na wala hatutarajii kuwekewa mafuta. Kuna muda tunamiss story mbili tatu msitukimbie.
 
Wengine wana fanya kwa moyo,hawa hitaji Return ya Vitu..Just be good to Him/Her
 
Katika kitu ambacho sipendi, ni mtu kuniwekea mafuta, inanifanya kama awe ananidai. Ni Bora uongee nae, kwamba naomba uwe unanipitia, na nichangie kiasi flani kwa week au mwezi. Ongea nae kiume. Usiseme tu tupitie kituoni apo tuweke mafuta bila kuongea nae.
Uko sahihi.
 
Back
Top Bottom