Ninaishi na mke ambae hatujaoana ila tuna watoto na tunaishi vizuri. Ndoa ni sheria ya kijinga inayoweza kunivuruga

Nadhani kiserikali kwa muda ulioishi naye ni kama umeshamuoa kwa hiyo akiwa na tamaa za Mali anaweza kwenda mahakamani na akadai mgao wake bila shida yoyote
 

Utakuja kuwakosesha haki zao za urithi bure hao watoto, mmoja wenu akitangulia.
 
We jamaa ni mbinafsi sana kama una hofu hiyo hukupaswa kuishi na huyo mwanamke.

Vipi ikitokea ukatangulia kudedi, si mkeo hatapata kitu zaidi zaidi ndgu zao ndo watachukua kila kitu na kumwacha mkeo atangetange na wanao.
Kama ni kukuua ili achukue mali anaweza hata sasa mkiwa hamna ndoa ni vile tu kakupenda ila wewe ulivyo mbinafsi unahisi ukimuoa atakuwahisha.

Kwa hilo umezingua sana.
 
Una tabia za kikafiri sana wewe ndo ulileta uzi wa kuwaponda wazanzibar nilijua kama una tabia za kishenzi
 
Kama umelipa mahari haina shida hamna sehemu niliona kwenye biblia mtu akifungiwa ndoa na mchungaji ama padri,nakubuka yakobo alijichukulia mkewe kwa malipo ya kuchunga sikuona mahali akifungishwa ndoa,
 
Si wafunge ya serikali kama hawaitaji usumbufu
 
Sijaelewa, mara tumeishi muda mrefu na kwa kujibu wa sheria mkiishi miaka miwili na zaidi tayari nyie ni mke na mume,mara sijui kuna wanawake mkishafunga ndoa baadaye wanataka muachane ili mgawane mali! Je sasa hiyo ndoa uliyesema mnatambulika nyie tayari wanandoa mkiachana hamgawani mali?
 
Kama umelipa mahari haina shida hamna sehemu niliona kwenye biblia mtu akifungiwa ndoa na mchungaji ama padri,nakubuka yakobo alijichukulia mkewe kwa malipo ya kuchunga sikuona mahali akifungishwa ndoa,
Mkuu umeongea point sanaa...

Sijaona mtu humu anazungumzia ndoa ya kiserikali,,,pia wengi wamekomaa na urithi, urithi as if cheti cha ndoa faida yake pekee ni pale ukifa...ila ukiwa hai hakina maana.. (Hii inaonyesha ni jinsi gani Cheti hakina faida wakati mkiwa mnaishi).

Ninachojua mm asilimia kubwa ya makabila yetu,, Ukishamaliza taratibu za kitamaduni(Mahari),, tayari unakuwa umeoa... na lolote litakalotokea mbele ya safari litakuwa treated kama watu walio kwenye ndoa...
 
Dini gani wewe inayoruhusu kufanya ngono isiyo halali!?!?
 
Kila binadamu afanye mambo yao, ahsante kwa taarifa...
 
Endelea kunikataa sijui nani atakuoa[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3].

Sina chuki yoyote na wanawake ila THE TRUTH HAS TO BE TOLD ,nyie mna umimi sana.

Nadhani hii ni dhambi ya asili na ilianzia pale Edeni.


Mfano; ni kawaida wanaume tukienda labda kula na tupo watatu au 4 mmoja akalipia bill yote.
Ila ikiwa ni nyie wadada kila mtu atalipa kivyake.

Ni kawaida sana labda unapita filling station na rafiki baada ya kujaza mafuta akalipia yeye au hata akaongezea kiasi flani.

Ila kwa wadada sio rahisi shosti kapewa trip mfike filling station afungue mkoba wake kuchangia angalau lita kazaa za mafuta.

Anyway ndoa ni jambo la watu wawili kwa kadri wao watavyoamua liwe regardless limepita kanisani au halikupita.
 
Kufunga ndoa ni kuweka maagano kanisani...serikalini au kimila pia ukisema unaishi na mwnaamke bila ndoa Haina maana ni mkeo maana hata dada ako unaweza ishi nae tu tofauti unazini na huyo mwanamke so kuepusha tafrani ebu Funga ndoa
 
Umewaza kitoto sana.. Umejiangalia wewe na fikra zako, bila faida jumuishi za ndoa.. Huna hata haki ya kufumania. Umewaza uchoyo wa Mali bila pia kuangalia haki za baadae za malezi kwa watoto wako..
NB: Mke anayekuacha leo, alishapanga kukuacha miaka 5 iliyopita akiwa katika hali ya furaha. Usimchukulie powa kuwa hajui chochote
 
Labda kama unaongelea kitu kingine lakini kama kweli unazungumzia ndoa naomba nikwambie tayari UPO NDANI YA NDOA!!! HIYO NI NDOA!! Inawezekana unazungumzia harusi au kitu kingine! LAKINI JINSI ULIVYOJIELEZA, UMO NDANI YA NDOA!! HIYO NDOA, haijalishi mmeifunga kanisani, msikini, kimila, porini, mkiwa wawili au mbele ya umati mkubwa!! Haijalishi!
 
Hiyo ni ndoa ila bado harusi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…