Ninaishi na mke ambae hatujaoana ila tuna watoto na tunaishi vizuri. Ndoa ni sheria ya kijinga inayoweza kunivuruga

Siku ukifa ghafla ndio utajua haujui .Kwanza hiyo dhambi ya uzinzi inazidi kukolea
 
Kama hamjafunga ndoa hamuwezi kuwa wanandoa,hata kama kwenu na kwao munafahamika! Ninyi ni wachumba tu,hata kama mumeishi miaka zaidi ya miwili bado hamtaweza kupeana talaka kwa sababu hamna ndoa,Ila mali mutakazo chuma mutagawana hata kama hamjafunga ndoa
 
kwenu na kwao mnajuana ila mungu hawatambueni mnaendelea kuzini
Unaona jinsi watu wanavyorahisisha ndoa,wanachukuana wanaishi kinyumba na kutambulishana then wanajiita mke na mume,na wanakwepa kufunga ndoa maisha yao yote,wanapaswa waitane wachumba sio mke na mume kama mtoa mada anavyodai
 
Kama alitoa Mahali na Wazazi wa Binti wakaipokea hapo hakuna shida,hiyo ni Ndoa tayari sema tu haina sherehe!!
Si sahihi! Yani hapo hata wakiachana wakaenda kudai talaka mahakamani, mahakama haiwezi kutoa talaka watahesabika kama vimada tu au wachumba.solution ni wao wafunge ndoa tu,mali watagawana hata kama hawajafunga ndoa
 
Hapana mkuu, hapo kidogo unakuwa unakosea mahala, kama mnaishi vizuri na mnaelewana basi mfunge ndoa, kwanza unampa heshima mkeo kuwa nae ni mke wa mtu, pili mkiwa ndani ya ndoa kuna haki ambazo mkeo atazipata (kwa mfano kama wewe ni mfanyakazi ukiwa na ndoa waweza kumkatia bima ya afya mkeo kama yeye sio muajiriwa), pia lijapo suala la mirathi iwapo imetokea wewe umetangulia mbele za haki inakiwa inafanya mkeo anakuwa analinda mali dhidi ya ndugu wenye uchu na mali zako, yaani mahakami kwa document ya cheti cha ndoa anakabidhiwa mali zote bila utata wowote. Kifupi ndoa ni nzuri itanguliwe na urafiki kati ya wenza then baada ya kuwepo maelewano ndipo ndoa ifungwe. Nyinyi mnaelewana na mna amani mkifunga ndoa haimaanishi amani itatoweka hapana bali itaongeza heshima fulani kwako na kwake.
 
Huyo ni mke wa ndo kwa mujibu wa shetia za nchi sema tu huna cheti cha ndoa
 
Ndiyo.Eidha uende Mbinguni au Jehanam.Na kuishi maisha ya dhambi ya uzinzi kwa kipindi chote ulichoishi ni dhahiri kwamba ukifa Jehanam inakuhusu.
Ulishawahi kufa hadi ukajua yote hayo ?

Au kuna mtu alikufa akafufuka akakusimulia ?
 
Huwa wanaona sisi Ni wakutangulia TU[emoji3525]
 
Uwe na hakika na wanao wataishi hivo. Hakuna mbingu ya wazinzi
 
Siku ukifa ndo utajua umuhimu wa ndoa (sikuombei mabaya)
 
Mwanamke akifariki kwanza hakunaga shida kubwa saana, ila akitangulia mwanaume hapo cha-cha ndipo palipo na mtihani ndiyo maana mwanaume huambiwa aweke mambo sawa, kuna mbaba mmoja mwanaye alikuwa mgonjwa badala yakufuatilia afya ya mwanaye yeye anaulizia mali alizonazo anataka kuzijua, ila Mungu ni mwema kijana kapona kabisa, naona Mungu alitaka kumuonyesha jinsi mzazi wake alivyo!
 
Kama umelipa mahari haina shida hamna sehemu niliona kwenye biblia mtu akifungiwa ndoa na mchungaji ama padri,nakubuka yakobo alijichukulia mkewe kwa malipo ya kuchunga sikuona mahali akifungishwa ndoa,
Kasome vizuri alifanyiwa sherehe nakukabidhiwa mbuzi kwenye gunia maana alichezewa faulo.
 
Mwanamke anakuwa mke baada ya kuolewa na mwanaume anakuwa mume baada ya kuoa. Jaribu kutofautisha kati ya kuishi na mke na kuishi na mwanamke.
 
Kama mtu unawasiwasi naye unaishi naye wa nini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…