Ninajua kila mtu anajua kinachoendelea kule Los Angeles ila sijui ni wangapi wanajua chanzo cha ule moto unaouangamiza mji wa uzuri wa Dunia

Ha ha ha..... Tutasikia stories nyingi sana za kubumba. Cheche inapaaa......inarukia jengo jingine....🀣🀣🀣🀣🀣 JF INA WATU UKIKAA HUMU UNACHEKA TU
Kweli mimwenyewe nilishangaa hiyo video unakaa ghafla unaona mnazi unaungua
 
Hili la kumpigia Kura si kweli. Ni kwamba kwa wale wote walioshinda tunzo katika tamasha hilo hakuna aliyemshukuru Mungu, hivyo basi mtangazaji akashangaa na kusema katika washindi wote hakuna hata mmoja aliyemshukuru Mungu kwa ushindi wake. Akaendelea kwa kusema inaonekana huu mji si wa watu wa Mungu. Hivyo bwana mshana uache mara moja kupotosha watu na kusambaza taarifa za uongo ili kufanikisha azima yako.
 
Mji wenyewe unaitwa lost angles!!!!
Unaitwa malikia wa
Walipanga kukufuru tu ili kumfurahisha baba yao shetani aliyewapa utajili na umaarufu,,chakushangaza shetani naye kawakimbia ujue shetani muongo Sana kipindi Niko mtoto unasikia kabisa iba mboga bhana hakuna anayekuona Sasa ibao uone Sasa unafumwa unakula mkongoto lenyewe lisha sepa,, shetani yupo jamani
 
Mtu anazusha uongo halafu anatafuta kundi la watu wamsapoti.

Na kwa vile waafrika wengi hasa watanzania wamejaa mihemko ya kiimani na kidini wanasapoti blindly.

Blind acceptance is the enemy of truth.
 
Mshana, Mungu unayemzungumzia hapa ndio huyu huyu, Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu? Ndio huyu huyu anayetufundisha samehe mara saba sabini? Ndio huyu huyu ambaye Injili inatufudisha Mungu ni Upendo? Yani wajinga fulani wapige kura halafu Mwenyezi Mungu akasirike alete moto? Ni Mungu huyu huyu aliyemtoa mwanae wa pekee afe msalabani ili wenye dhambi waokolewe na wauone uzima wa Milele?! Usije ukawa unamzungumizie shetani?!? Mungu Mwenye enzi ninayemjua mimi hawezi kuhangaika kumkomoa mwanaadamu aliyedhaifu, kwa kumchomea nyumba ili kuonyesha Ukuu wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…