Juzi tarehe 13. 11 Rais alitoa hotuba ya ufunguzi wa Bunge Dodoma na kuahidi kuimarisha na kushamirisha sekta binafsi nchini ili iweze kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi. Mimi ninakubaliana na hatua hizo kwa vile hakuna taifa duniani lililoendelea bila sekta binafsi.
Kimsingi ni kweli sekta binafsi ni injini na mhimili wa uchumi. Sekta binafsi hutengeneza ajira, hulipa kodi, husaidia kunawirisha sekta za afya, elimu na teknolojia nk. Kwa msingi huo ninashauri serikali iendelee kutengeneza mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji hususani watanzania.
1. Hii ni pamoja na kupitia upya sera, sheria, kanuni, taratibu na mifumo kandamizi ya kodi, tozo, na nyinginezo za kazi,uwekezaji nk
2. Kwa sasa serikali iongeze uwanja wa kufanya biashara na sekta binafsi kwa vile ndiyo mtumiaji mkubwa wa huduma zitolewazo na sekta hiyo.
3. Kuimarisha miundo mbinu na kuendelea kupunguza gharama za uzalishaji hapa nchini kwa kudhibiti rushwa, bei ya umeme, maji, leseni, kodi, riba nk
4. Mifumo ya malipo ya Serikali kwa mtandao au digitali iendelee kutumika imesaidia sana kupunguza urasimu na rushwa ni mizuri sana nk
Na mageuzi mengine yanahitajika kwa sasa ili kujenga uchumi wenye ushindani na kama alivyosema Rais kuifanya Tanzania kitovu cha biashara kikanda na kuvutia wawekezaji. Tutumie fursa tulizo nazo kuboresha uchumi wetu. Muda ni mchache Mambo ni mengi sana.