mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,286
- 6,729
Nilijua huna jibu zaidi ya kuleta blabla, mimi sio katibu wa itikadi wa chama chochote cha siasa, hivyo sio wajibu wangu kueneza sera za chama chochote cha siasa. Kama unataka kujua sera za chama chochote cha siasa hapa hakuna ofisi ya chama chochote, nakushauri uende kwenye ofisi za chama husika ukachukue vitabu na vijarida vya sera zao. Vinginevyo unionyeshe mada yoyote uliyowahi kuanzisha ili ueneze sera za ccm.
Kama bureau De change walikuwa wanatakatisha pesa chafu, ilipaswa wapelekwe mahakamani kila mmoja ashitakiwe kutokana na ukubwa wa kosa lake. Hilo la kuporwa pesa za Bureau de change lilifanyika mchana kweupe, sijui unakataa nini. Kama umeporwa na Jwtz, ni mahakama ipi utaenda hapa nchini kushitaki. Hakuna mtu yeyote anayeweza kuagiza Jwtz wakaendeshe operation yoyote nchi hii za rais, je ni mahakama gani nchi hii inathubutu kwenda kinyume na maagizo ya rais, tena rais mwenyewe huyu asiye heshimu sheria? Nasema hivi hakuna muwekazaji yoyote wa maana anaweza kuwekeza hapa nchini chini ya serikali hii.
Hilo la kuomba serikali ya ccm iharibikiwe, naona umechomeka haya maneno ili yaweze kubeba maelezo yako dhaifu. Hatuko tayari kuiunga mkojo serikali yoyote ya wakandamizaji na wakiukaji wa haki za binadamu, wauaji na wezi wa kura. Huko Afrika kusini walikuwa na serikali halali, lakini tuliingilia mambo yao ya ndani kwakuwa serikali hiyo ya wazungu ilikuwa inawafanyia uonevu watu weusi.
Mmelalamika sana mitandaoni, kama viongozi wenu, na mtaendelea kulalamika na kulaumu sana, ndani na nje ya nchi, lakini ukweli unabaki kuwa nchi inatawalika, hata mkidai ni kwa mabavu (lakini ya nguvu ya umma).
Mimi na wewe tunachopaswa kufanya, japo unadai wewe sio katibu wa itikadi wa chama chochote cha siasa ni kujadili masuala ya kitaifa badala ya matukio ambayo kwayo hutatuliwa kwenye vyombo husika vya kikatiba. Kutokufanya hivyo ni lawama za kitoto, kwa mfano dai lako ati je ni mahakama gani nchi hii inathubutu kwenda kinyume na maagizo ya rais!!!