Ninakubaliana na Rais, hiki ni kipindi cha kuimarisha Sekta Binafsi

Ninakubaliana na Rais, hiki ni kipindi cha kuimarisha Sekta Binafsi

Kaka, Waafrika chini ya Jangwa la Sahara wenzetu wanatuita Sub human beings, Binaadamu tulilokuwa hatujakamilika kuumbwa..

Nchi zetu zimejawa na rasilimali za kila Aina, lakini ni nchi maskini kupita nchi zote duniani

Waafrika weusi Hisia zimetawala maamuzi kuliko uhalisia wa Jambo husika

Mfano mzuri wa Mwafrika chini ya Jangwa la sahara ni Wewe,inawezekana umesoma unajua mambo ya Biashara

Lakini maamuzi yako yamejawa na hisia kuliko uhalisia wa haya tunayo comments kweye huu mjadala

Unapindisha pindisha.stori kutokana na hisia zako za kuipenda Chama chako na serikali yako

Costs, benefits, expenses, credit,debits,bla bla bla, hayo mambo hayahusiani na huu mjadala

Kama Wasomi Wenyewe ndio kama nyinyi basi, Tanzania as a country has got a long way to go
Si unaona sasa fuata JF motto ‘ficha ......

Kumbe unajadili vitu hujui kama topic yenyewe inayohusu mambo ya taxation ni accounts.

Wewe unadhani kwa nini waajiriwa wa TRA wanaokwenda kukadiria wafanyabishara kodi ni wahasibu. Unadhani kodi inakadiriwa tu kwa utashi wa mtu.

Matatizo watu wanajitafutia kwa kutotunza kumbukumbu zao na kuto kuandaa accounts zao on time.

Halafu sasa kwenye hii mada sina upande wala sifanyi siasa nataka nijifunze tatizo lilipo haswa maana malalamiko ya kodi yamekuwa mengi.
 
Kuinua sekta binafsi ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi kama kutakua na usimamizi makini wa sheria za nchi kwa maslahi ya nchi husika

Serikali inatakiwa kuongeza umakini na kuhakikisha ufuatwaji wa sheria na miongozo zinayosimamia sekta binafsi, na hapohapo inatakiwa kuhakikisha kwamba wananchi hawakosi huduma muhimu sababu ya urasimu wa sekta binafsi.

Kampuni binafsi zitakua na uhuru wake kwa kufuata taratibu zilizopewa na kuzikubali, kinyume cha hapo mkono wa serikali utakua nazo tuu hamna namna.

Hili la unazoita sheria kandamizi ni la kuangalia kwa jicho la tatu na kujiuliza kama hizo sheria kandamizi zimeanza baada investors kuanza operations au ni sheria zilizokuepo na akakubaliana nazo? Wengi wanalalamikia sheria ambazo zimekuepo miaka yote na wamekua kimya miaka yote pia ila sasa ndio imekuja shida.

Sheria za kodi kutofuatwa na adhabu katika matukio ya uhujumu uchumi zitaendelea kutekelezwa ili kuhakikisha kuna mazingira sahihi na rafiki kwa wawekezaji kwenye sekta binafsi, watendaji wao, walaji pamoja na serikali.

Follow the rules, is only way utakuwa safe.
Ni kweli kuna upungufu wa kumbukumbu na kutojua sheria za kodi zinapelekea wafanyabiashara kutozwa kodi na faini kwa kutotimiza wajibu wao na hii huwafanya kupata faini ambayo haiendani na kipato chao cha biashara hapo ndipo lilipo tatizo la wafanya biashara na pia upungufu wa sheria yenyewe kuzalisha faini na riba kubwa mno na ndiyo kilio kikubwa. Upande wa pili ni wafanya kazi wemyewe kubambikiza kodi na faini za uongo ili kushawishi rushwa kubwa mfano Kesi ya mfanyalazi wa TRA Mwanza-Mary Moyo mwezi uliopita aliyekamatwa na TAKUKURU kwa kumbambikia mfanya biashara kodi za uongo na kuomba mamilioni ya fedha. Hivyo kuna suala la elimu, sheria yenyewe,maadili kwa watumishi na mifumo.
 
Juzi tarehe 13. 11 Rais alitoa hotuba ya ufunguzi wa Bunge Dodoma na kuahidi kuimarisha na kushamirisha sekta binafsi nchini ili iweze kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi. Mimi ninakubaliana na hatua hizo kwa vile hakuna taifa duniani lililoendelea bila sekta binafsi.

Kimsingi ni kweli sekta binafsi ni injini na mhimili wa uchumi. Sekta binafsi hutengeneza ajira, hulipa kodi, husaidia kunawirisha sekta za afya, elimu na teknolojia nk. Kwa msingi huo ninashauri serikali iendelee kutengeneza mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji hususani watanzania.

1. Hii ni pamoja na kupitia upya sera, sheria, kanuni, taratibu na mifumo kandamizi ya kodi, tozo, na nyinginezo za kazi,uwekezaji nk

2. Kwa sasa serikali iongeze uwanja wa kufanya biashara na sekta binafsi kwa vile ndiyo mtumiaji mkubwa wa huduma zitolewazo na sekta hiyo.

3. Kuimarisha miundo mbinu na kuendelea kupunguza gharama za uzalishaji hapa nchini kwa kudhibiti rushwa, bei ya umeme, maji, leseni, kodi, riba nk

4. Mifumo ya malipo ya Serikali kwa mtandao au digitali iendelee kutumika imesaidia sana kupunguza urasimu na rushwa ni mizuri sana nk

Na mageuzi mengine yanahitajika kwa sasa ili kujenga uchumi wenye ushindani na kama alivyosema Rais kuifanya Tanzania kitovu cha biashara kikanda na kuvutia wawekezaji. Tutumie fursa tulizo nazo kuboresha uchumi wetu. Muda ni mchache Mambo ni mengi sana.
aliyeiua hawezi kuifufua. Kifupi pombe hapendi mafanikio ya watu wengine. Ndio maana yangu aingie madarakani ameshindwa kulipa madeni ya ndani na kusababisha baadhi ya wafanyabishara kufilisika
 
Juzi tarehe 13. 11 Rais alitoa hotuba ya ufunguzi wa Bunge Dodoma na kuahidi kuimarisha na kushamirisha sekta binafsi nchini ili iweze kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi. Mimi ninakubaliana na hatua hizo kwa vile hakuna taifa duniani lililoendelea bila sekta binafsi.

Kimsingi ni kweli sekta binafsi ni injini na mhimili wa uchumi. Sekta binafsi hutengeneza ajira, hulipa kodi, husaidia kunawirisha sekta za afya, elimu na teknolojia nk. Kwa msingi huo ninashauri serikali iendelee kutengeneza mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji hususani watanzania.

1. Hii ni pamoja na kupitia upya sera, sheria, kanuni, taratibu na mifumo kandamizi ya kodi, tozo, na nyinginezo za kazi,uwekezaji nk

2. Kwa sasa serikali iongeze uwanja wa kufanya biashara na sekta binafsi kwa vile ndiyo mtumiaji mkubwa wa huduma zitolewazo na sekta hiyo.

3. Kuimarisha miundo mbinu na kuendelea kupunguza gharama za uzalishaji hapa nchini kwa kudhibiti rushwa, bei ya umeme, maji, leseni, kodi, riba nk

4. Mifumo ya malipo ya Serikali kwa mtandao au digitali iendelee kutumika imesaidia sana kupunguza urasimu na rushwa ni mizuri sana nk

Na mageuzi mengine yanahitajika kwa sasa ili kujenga uchumi wenye ushindani na kama alivyosema Rais kuifanya Tanzania kitovu cha biashara kikanda na kuvutia wawekezaji. Tutumie fursa tulizo nazo kuboresha uchumi wetu. Muda ni mchache Mambo ni mengi sana.
Serikali yoyote makini dunia inakuwa na mfumo wa kuinua biashara yaani 'Business tool '
 
Ni kweli kuna upungufu wa kumbukumbu na kutojua sheria za kodi zinapelekea wafanyabiashara kutozwa kodi na faini kwa kutotimiza wajibu wao na hii huwafanya kupata faini ambayo haiendani na kipato chao cha biashara hapo ndipo lilipo tatizo la wafanya biashara na pia upungufu wa sheria yenyewe kuzalisha faini na riba kubwa mno na ndiyo kilio kikubwa. Upande wa pili ni wafanya kazi wemyewe kubambikiza kodi na faini za uongo ili kushawishi rushwa kubwa mfano Kesi ya mfanyalazi wa TRA Mwanza-Mary Moyo mwezi uliopita aliyekamatwa na TAKUKURU kwa kumbambikia mfanya biashara kodi za uongo na kuomba mamilioni ya fedha. Hivyo kuna suala la elimu, sheria yenyewe,maadili kwa watumishi na mifumo.

Suluhu la hili tatizo ni wenye makampuni/wawekezaji kujua sheria za na taratibu za kodi, na Watendaji wakuu wa makampuni kuzijua sheria na taratibu za kodi na kuzitekeleza kadri kadri ya taratibu za TRA. Wengi wetu tunafanya biashara lakini hatuna uelewa wa kodi. Na hata ikitokea TRA wanatuambia tulipe hizo kodi wanasema tuu lipa kiasi hiki ila hawatupatii maelezo/tasfiri/matokeo ya wanachotuambia.

Na kutekeleza hilo TRA wasiishie tuu kwenye kupokea reports, kukusanya kodi, na kutoa tax clearance. Wanatakiwa kukaa na kujitathmini kuhusu malalamiko ya wateja. Wafanye utafiti kujua gap lililopo kati yao na walipa kodi na kulifanyia kazi ili kujenga mazingira rafiki kati yao na pesa zinakotoka.

Sioni kwanini TRA ishindwe kupata suluhu katika kupunguza mateso na malalamiko ya wateja wanaowafanya wao kuwa walipo. Kumsaidia mlipa kodi kuelewa taratibu itawapa motisha watu wengi zaidi kuwekeza na kufanya kazi na TRA.

Idara ya huduma kwa mteja TRA mnafeli wapi?
Mkiweza kuvaa viatu vya walipa kodi mkawatendea haki watatimiza wajibu wao kiroho safi. Ila mkiwaacha waendelee kuumia kwa makosa madogomadogo wanayofanya kwa kutokuwa na uelewa wa kodi na kuwapa kodi kubwa na penalties mjue tuu mnachochea kuipunguzia nchi mapato
 
Nakupenda sitaacha kukufundisha ili ujue.

Ili sekta binafsi ikue ni lazima serikali ipunguze sana ushiriki wake katika biashara.

Pili, lazma Uhuru binafsi wa makampuni na wajasiriamali uongezeke maradufu.

Tatu,sheria kandamizi lazima zifutwe ili kutoa mwanya kwa ma kampuni kufanya biashara ,sheria kama za uhujumu uchumi, sheria za kodi nk. Nne,nilazima serikali ibadili mfumo wa kodi kwa wajasiriamali hasa wanapoanza.

NB: Kuinua sekta binafsi ni KUIPUNGUZIA SERIKALI MAJUKUM NA MAMLAKA, je jiwe yupo tayar kupunguza mamlaka yake?
Umeandika point za msingi kabsa, mfano angalia GPSA inavyokimbizana na wafanyabiashara wa stationery mjini mpaka wamefunga hiyo biashara ili gpsa iweze kufanya biashara peke yake na serikali.
 
Suluhu la hili tatizo ni wenye makampuni/wawekezaji kujua sheria za na taratibu za kodi, na Watendaji wakuu wa makampuni kuzijua sheria na taratibu za kodi na kuzitekeleza kadri kadri ya taratibu za TRA. Wengi wetu tunafanya biashara lakini hatuna uelewa wa kodi. Na hata ikitokea TRA wanatuambia tulipe hizo kodi wanasema tuu lipa kiasi hiki ila hawatupatii maelezo/tasfiri/matokeo ya wanachotuambia.

Na kutekeleza hilo TRA wasiishie tuu kwenye kupokea reports, kukusanya kodi, na kutoa tax clearance. Wanatakiwa kukaa na kujitathmini kuhusu malalamiko ya wateja. Wafanye utafiti kujua gap lililopo kati yao na walipa kodi na kulifanyia kazi ili kujenga mazingira rafiki kati yao na pesa zinakotoka.

Sioni kwanini TRA ishindwe kupata suluhu katika kupunguza mateso na malalamiko ya wateja wanaowafanya wao kuwa walipo. Kumsaidia mlipa kodi kuelewa taratibu itawapa motisha watu wengi zaidi kuwekeza na kufanya kazi na TRA.

Idara ya huduma kwa mteja TRA mnafeli wapi?
Mkiweza kuvaa viatu vya walipa kodi mkawatendea haki watatimiza wajibu wao kiroho safi. Ila mkiwaacha waendelee kuumia kwa makosa madogomadogo wanayofanya kwa kutokuwa na uelewa wa kodi na kuwapa kodi kubwa na penalties mjue tuu mnachochea kuipunguzia nchi mapato
Sidhani kama kodi za TRA hazilipiki bali tatizo biashara hakuna imefungwa kuanzia juu mpaka chini, unaporuhusu serikali ifanye biashara jua kuwa mamia kwa mamilioni watafunga biashara zao
 
Sidhani kama kodi za TRA hazilipiki bali tatizo biashara hakuna imefungwa kuanzia juu mpaka chini, unaporuhusu serikali ifanye biashara jua kuwa mamia kwa mamilioni watafunga biashara zao
That is not the issue.

Kitu ambacho nimejifunza kodi inayolalamikiwa for the most imekadiriwa ni VAT na hiyo aitakiwi kuwa tatizo kwa mfanyabiashara because it should be passed to the final consumer.

If you are business input VAT can be claimed back and you have the responsibility to claim output VAT on behalf of TRA.

Kwa maana hiyo kitendo cha kutoa risiti isiyo sahihi ni upumbavu uliopindukia because VAT is traceable.

Halikadhalika kitendo cha TRA kuwaadhibu walaji it’s just pathetic it’s not their duty to ask if a trader is registered if they are the final consumers or their duty to know who is a registered and unregistered traders complicated to explain but from what I heard from TRA ☝️ their explanation is just pathetic. To explain how pathetic requires a report.

Kuna tatizo TRA kwenye matakwa ya VAT payer in terms of records starting with what a receipt needs to cover and what records a business needs to keep in order to trace registered VAT payers, kuna watu wananunua kariakoo for exportation kuwaadhibu ni ushamba kwa uzembe wao.

Kuna maswali ya tax estimates kwa wafanya biashara when they are filing for their quarterly tax returns what system is used accrual or capital (as yet its not clear, to me). Hayo mambo yanahitaji washaushauri (accountants) kuliko TRA kuzunguka nchi nzima kutoa elimu.

Na linapokuja swala la profit accounts ndio kabisa utegemei mfanya biashara aweze fanya accounts bila ya accountant kwa sababu awezi jua all of his allowed expenses kama VAT tu inamshinda ku file. If that is the case most are at the mercy of TRA officials, that’s not ideal.

Unajua Trump halipi Tax ndogo huko kwao kwa bahati mmbaya it’s the Law, similarly malalamiko yetu ya makampuni kutolipa kodi kwa miaka sio kwamba kweli wanakwepa kodi ni sheria zetu za copy and paste ambazo pengine atuzuelewi vizuri ndio zinawaofanya watu wanaotumia firms kama PWC au Dolloite kufanya accounts zao kutumia loopholes za hizo sheria kukwepa kodi (hao watu ni tatizo ata kwa mabeberu)
that is the case everywhere in the world.

Kwetu sisi wafanyabiashara na accountants it appears have limited knowledge on the law to make matters worst kila finance act inaleta mabadiliko and people don’t keep up but TRA staffs: there is a problem of taxation in Tanzania.
 
Mwenyewe ndio kaiua sekta binafsi kwenye awamu yake ya kwanza, kila tenda anapeleka Suma JKT, leo anasema anataka kuifufua nitamuamini vipi?
JK aliweka vizuri secta binafsi yeye akabadilisha nakumnanga miaka mitano imepita anarudia matapishi if that the case amuombe radhi JK maana alimnanga
 
Sidhani kama kodi za TRA hazilipiki bali tatizo biashara hakuna imefungwa kuanzia juu mpaka chini, unaporuhusu serikali ifanye biashara jua kuwa mamia kwa mamilioni watafunga biashara zao
Serikali inafanya biashara gani zinazoharibu biashara zao?
 
Ukisoma ilani ya CCM halafu ukasikiliza Ile speech ya kufungua Bunge utaweza kujipanga kujua wapi uongeze nguvu.

Kwa upande wa mikopo midogomidogo SME Serikali imejipanga, wananchi tujipange, banks na taasisi za fedha wajipange pia

Maendeleo hayana vyama
kujipanga ni chaka fulan hivi
 
Anachosema sio anachomaanisha. Haamini katika sekta binafsi, bali anaamini katika sekta ya umma, simply huko anaweza kwenda kwa kustukiza na kuwatambua ili kusaka kiki za kisiasa.

Kwa taarifa yako hakuna muwekazaji serious atawekeza chini ya utawala wake, maana sio mtu anayejali sheria. Ukiona taifa ambalo hata mchina anakwepa kuwekeza jiulize sana.

Hapa sekta binafsi itaanza kurejea tena ilipokuwa, baada ya yeye kutoka madarakani. Rejea kilichotokea kwa wafanyabishara wa Bureau de change.
Kwa kutumia utaalamu na uzoefu wako wa uchumi, tupe mifano halisi ya jinsi sekta ya binafsi iliweza kukuza uchumi kabla ya utawala wa huyo unayembeza.

Ukishindwa kufanya hivyo bila shaka yoyote wewe tindo unaleta swaga tu za kijiweni humu JF kama mlivyojiaminisha "NiYeyeee" angeshinda Uchaguzi Mkuu. Badala yake mmelishwa matango pori kuamini viongozi watashitakiwa na nchi itawekewa vikwazo vya kiuchumi.

Uamini usiamini, iwapo utatumia kichwa chako vizuri, miaka 5 ya utawala wa sasa, kama wewe ni mjasiriamali, una kampuni au umeajiriwa, kuna fursa tele za kujikwamua kiuchumi.
 
Nakurahisishia kabisa, rais juzi kahamishia kitengo cha uwekezaji kwenye ofisi yake,maelezo yake ilikuwa kuwa utendaji wa hicho kitengo unakwamisha uwekezaji. Hilo moja, unasema kuna fursa tele za kujikwamua, nieleze zile pesa zilizoporwa kwenye Bureau de change kwa mtutu wa bunduki na Jwtz zikipelekwa wapi? Katika mazingira hayo unatarajia muwekazaji yoyote serious kutokea? Urudi na maelezo ya hizo pesa za Bureau nikupe chai ya moto.
 
Katika moja ya bandiko zake Salary Slip nimemshauri, nawe nakushauri, mtumie majukwaa ya mitandao ya jamii kueleza Itikadi na Sera za vyama vyenu vya siasa badala ya kuomba dua Serikali ya CCM iharibikiwe.

Km hilo la Bureau de Change, wewe unajua kuwa zilikuwa zinatumika kutakatisha fedha. Kwa sasa baadhi ya Benki za biashara, km NMB, kama ulikuwa hujui, zimefungua ATM ambazo mtu anaweza kutoa fedha ya kigeni.

Kwamba kuna fedha iliporwa kwenye Bureau de Change, nawe unataka tuamini hivyo wakati hakuna madai yoyote mahamakani! Porojo tu za kijiweni kama zile zile wakati wa kampeni za uchaguzi - ati ushindi kweupe.

Kama hambadiliki kifikra mtabaki kuongozwa na udaku. Pole zenu wafuasi wa upinzani humu JF kwa upumbavu na ulofa wenu kifikra.
 
Nilijua huna jibu zaidi ya kuleta blabla, mimi sio katibu wa itikadi wa chama chochote cha siasa, hivyo sio wajibu wangu kueneza sera za chama chochote cha siasa. Kama unataka kujua sera za chama chochote cha siasa hapa hakuna ofisi ya chama chochote, nakushauri uende kwenye ofisi za chama husika ukachukue vitabu na vijarida vya sera zao. Vinginevyo unionyeshe mada yoyote uliyowahi kuanzisha ili ueneze sera za ccm.

Kama bureau De change walikuwa wanatakatisha pesa chafu, ilipaswa wapelekwe mahakamani kila mmoja ashitakiwe kutokana na ukubwa wa kosa lake. Hilo la kuporwa pesa za Bureau de change lilifanyika mchana kweupe, sijui unakataa nini. Kama umeporwa na Jwtz, ni mahakama ipi utaenda hapa nchini kushitaki. Hakuna mtu yeyote anayeweza kuagiza Jwtz wakaendeshe operation yoyote nchi hii za rais, je ni mahakama gani nchi hii inathubutu kwenda kinyume na maagizo ya rais, tena rais mwenyewe huyu asiye heshimu sheria? Nasema hivi hakuna muwekazaji yoyote wa maana anaweza kuwekeza hapa nchini chini ya serikali hii.

Hilo la kuomba serikali ya ccm iharibikiwe, naona umechomeka haya maneno ili yaweze kubeba maelezo yako dhaifu. Hatuko tayari kuiunga mkojo serikali yoyote ya wakandamizaji na wakiukaji wa haki za binadamu, wauaji na wezi wa kura. Huko Afrika kusini walikuwa na serikali halali, lakini tuliingilia mambo yao ya ndani kwakuwa serikali hiyo ya wazungu ilikuwa inawafanyia uonevu watu weusi.
 
Back
Top Bottom