Ninakubaliana na Rais, hiki ni kipindi cha kuimarisha Sekta Binafsi

Ninakubaliana na Rais, hiki ni kipindi cha kuimarisha Sekta Binafsi

Yaani baada ya miaka mitano ya kuiua sekta binafsi sasa anawadanganya kuwa anakwenda kuinua sekta binafsi.

Muulizeni kwanza, ni kwanini aliiua sekta binafsi?
 
Una uhakika kwa haya uliyoandika?matatizo makubwa tuliokuwa nayo Waafrika chini ya Jangwa la Sahara ni mfumo wetu wa kufikiri.

Wazungu wanatuita sub human being, binaadamu tuliokuwa hatajaubwa tukakamilika

Waafrika weusi tunatanguliza HISIA zetu katika kuwaza,kuamua,kulea Watoto wetu Katika kujenga hoja,nk

Naona hayo ndio yaliokukuta Wewe, HISIA za kupenda chama zimekufanya uwe mjinga

Nani alazimisha baina ya Wapinzani na Chama tawala!?

Nani amevurugika kama sio Chama Tawala, ..hao waliokimbilia Upinzani si wamerudi CCM,yuko Lowasa na wenzake?

Uchaguzi jinzi ulivyoendeshwa ni ushahidi tosha kuwa Chama tawala kimevurugika,kimechanganyikiwa

Mfumo mbovu gani umeshavunjwa,?..CCM imetawala Tanzania tangu tupate uhuru lakini bado hawajui ni mfumo gani waiendeshe Tanzania

CCM haijui Kama wao ni ma socialist,ma kommunist,wa Capitalist, wamechanganyika na hapa ndipo walipo feli

Kikwete alikuja na mfumo mzuri, sekta binafisi zilikuwa zimeshaanza kutia Sura,..

Huyu jamaa Magu kaondoa ule mfumo amekuja na wake ambao hata Nyerere ulimshinda..

Pale unapopeleka tenda zote kwa vyombo vya serikali maana yake huo ni usochalist,maana yake ni KUUWA sekta binafisi

mfumo ambao Dunia nzima umeukataa Hata hao waliouazisha

CCM imekaa Madarakani muda mwingi kiasi ambacho wamejisahau

wanaanza KUTEKA, KUTESA, KUPOTEZA wale wote ambao wanaokuja na MAWAZO na FIKRA mpya

Ili Tanzania ifanikiwe kimaendeleo ya KIUCHUMI, KIMAADILI inahitaji MAWAZO na MFUMO mpya wa kutuongoza

CCM must quit, CCM must go,56 years is enough..

Free Mazrui and all Political prisoners
Umejibu vizuri sana.
 
Haha mugah di mathew umeandika nini😀😀

Fuata taratibu hakuna atakaekugusa

Kama unabiashara inaweza kuwa ngumu sababu ulizoea kutokufuata taratibu... ila usikate tamaa, cha kufanya tafuta wataalamu wakushauri ufanye nini wakati unarudi kwenye mstari ili uweze kusurvive
Mama D,umeshaona wapi mtu anafungua kiduka, kibiashara chake

Lakini kabla hata hiyo biashara haijafanya kazi tayari amesha pangiwa Kodi gani alipe..,

Mfumo wa kukusanya Kodi,TRA,ni mbovu, sio Mfumo rafiki kwa mfanya biashara mwenye biashara ndogo..

Sasa unamwambia huyu jamaa afate taratibu

Taratibu gani zifuatwe wakati serikali inakusanya kodi kwa mfanya biashara,bila hata kujua biashara inamuingizia faida Gani?!

CCM imechoka,..iondoke Tu

Free Mazrui and all Political Prisoners
 
Mimi ninaamini Muhula wa pili wa awamu hii utabadilisha sura ya utendaji kazi kuhusu sekta binafsi serikali itakuwa imejifunza kitu tutoe muda tuone. Tusianze na lawama na maneno mengi.
 
Mama D,umeshaona wapi mtu anafungua kiduka, kibiashara chake

Lakini kabla hata hiyo biashara haijafanya kazi tayari amesha pangiwa Kodi gani alipe..,

Mfumo wa kukusanya Kodi,TRA,ni mbovu, sio Mfumo rafiki kwa mfanya biashara mwenye biashara ndogo..

Sasa unamwambia huyu jamaa afate taratibu

Taratibu gani zifuatwe wakati serikali inakusanya kodi kwa mfanya biashara,bila hata kujua biashara inamuingizia faida Gani?!

CCM imechoka,..iondoke Tu

Free Mazrui and all Political Prisoners

Kaduka kadogo kodi inakuaje?

Sijakuelewa
 
Kaduka kadogo kodi inakuaje?

Sijakuelewa

Mmmh nilijua kuwa kichwa chako kizito kidogo,Wanachama wengi wa CCM wako hivyo

Nimekusudia kusema kuwa serikali inakosea pale inapokadiria Kodi Kwa mfanya biashara kabla duka au biashara halijanza kufanya KAZI..

Yaani ukienda tu ofisi za Tra na kuwambia kuwa unataka kufungua biashara fulani basi wao hapo hapo wanakwambia kwa biashara hiyo inabidi ulipe Kodi kiasi Fulani..

Mfumo huu nimeuona TZ Tu,ninavyojua mimi kodi inalipwa kutokana na mwenendo wa biashara husika
 
Pale alipowateka akina MO, kumtesa na kumkejeli MANJI, na Wengine wengi.

Pale aliposema hadharani kuwa MATAJIRI wataishi kama MASHETANI.

Mleta mada yeye na Raisi wake wameshasahau hayo?

Nchi za Kiafrika chini ya Jangwa la Sahara, hatuwezi kujitawala.

Wazungu wanasema hivyo kila Siku,wanatuita sub human being.
Wanaongelea sekta binafsi gani hiyo....
Ni nani aliyebaki ??
Kama hadi wale waliokuwa na vikampuni vidogo vya fumigation , kufagia , catering,clearing na biashara nyingine ndogo ndogo za kuanzia [start-ups] siku hizi kazi zao zinafanywa na makampuni ya Serikali .. maana hizo ndio biashara ambazo mitaji yake ni ya kawaida na watu wengi waliokuwa wanaanza biashara walikuwa wanamudu ....
 
Sasa hivi hapa dar hadi barabara zinafagiwa na makampuni ya serikali , hivi ni vibiashara vilikuwa vinafanywa na wamama wazee waliokuwa wanajiunga kwenye vikundi .....wanafagia ..wengi ni wastaafu au hawajawahi kuajiriwa , umri umeenda na hawana mtu wa kuwasaidia zaidi ya nguvu zao ..
Wengine pengine walivokuwa na nguvu na uruzi kidogo walikuwa wanauza bar , wanadanga au shughuli zisizo rasmi ambako leo hawawezi kufanya na wana watoto au wajukuuu wa kusomesha .....watu kama hawa unapochukua vikazi vyao mnataka waende wapi ??
 
Mmmh nilijua kuwa kichwa chako kizito kidogo,Wanachama wengi wa CCM wako hivyo

Nimekusudia kusema kuwa serikali inakosea pale inapokadiria Kodi Kwa mfanya biashara kabla duka au biashara halijanza kufanya KAZI..

Yaani ukienda tu ofisi za Tra na kuwambia kuwa unataka kufungua biashara fulani basi wao hapo hapo wanakwambia kwa biashara hiyo inabidi ulipe Kodi kiasi Fulani..

Mfumo huu nimeuona TZ Tu,ninavyojua mimi kodi inalipwa kutokana na mwenendo wa biashara husika

Kichwa chako wewe ndio kizito sana. Maelezo unayotoa nashindwa kuamini kama umeshawahi hata kuijua wachana na kufanya biashara kwakweli.

Ukiachana na biashara ndogondogo zetu wamachinga, TRA wako wazi kabisa kukuelekeza nini cha kufanya kama utatoa taarifa.

Fanya makadirio ya kodi wakilisha TRA, kama hujaanza biashara toa taarifa TRA na kama biashara ilikuepo lakini imesimama kwa sababu yoyote ile toa taarifa pia

Kama huelewi fika TRA watakuelekeza taratibu za kufuata, ila ukinyamaza itakugharimu
 
Daah tangu aingie kampuni binafsi ziko hoi.....kampuni yangu walikimbilia Namibia.......
 
Mama D,umeshaona wapi mtu anafungua kiduka, kibiashara chake

Lakini kabla hata hiyo biashara haijafanya kazi tayari amesha pangiwa Kodi gani alipe..,

Mfumo wa kukusanya Kodi,TRA,ni mbovu, sio Mfumo rafiki kwa mfanya biashara mwenye biashara ndogo..

Sasa unamwambia huyu jamaa afate taratibu

Taratibu gani zifuatwe wakati serikali inakusanya kodi kwa mfanya biashara,bila hata kujua biashara inamuingizia faida Gani?!

CCM imechoka,..iondoke Tu

Free Mazrui and all Political Prisoners
Hili la kukadiriwa kodi linajirudia sana TRA lazima walitolee ufafanuzi.

Kwa ufahamu wangu mataifa mengine wanavyofanya kwenye kukadiriwa kodi.

1 moja utakadiriwa kodi kama mfumo wa kukusanya kodi hasa VAT ni unaotumiwa na mamlaka ni ‘accurual vat accounting’ chini ya mfumo wa huo kinachoangaliwa ni siku ya kutoa au kupokea receipt ata kama umeuza kwa credit. Jamaa wakija tax point ya hiyo receipt ni siku uliyoitoa na watataka ulipe VAT ata kama ujapokea malipo. Ikitokea mteja ame default unao ushahidi unawadai.

Basically nadhani tatizo kubwa la malalamiko ya kodi ni watu kutotumia accountancy services na uelewa hafifu wa sheria wa mambo ya kodi kama umuhimu kutunza nyaraka za kihasibu kama receipt, communication za mauzo au manunuzi na suppliers kama unatumia email, banks statement, annual accounts etc.

Nchi nyingine unatakiwa utunze hizo records kwa miaka sita kwa sababu jamaa wakiamua kuja kukuchunguza kama wana wasiwasi na malipo yako wasipokuta hizo nyaraka jiandae kukadiriwa kodi mpaka miaka minne nyuma.

Issue hapa ni sheria, kutotumia wahasibu na elimu hafifu inayotolewa kwa walipa kodi kuliko tatizo kuwa TRA pekee.

Kuna mifumo mingine kama VAT cash accounting, kuna mfumo wa margin schemes, kuna mfumo wa wakulima etc; mifumo yote hiyo ina mtindo wake wa kukadiriwa inategemea we ni mlipaji mpya au una zaidi ya mwaka kwenye biashara. Na inategemea wewe ni mlipaji wa mfumo wa annual accounting au quarterly (that is kwenye nchi za wenzetu).

Sasa wewe jifanye mjanja ukwepe kodi nchi halafu wakutie mikononi au waongopee VAT return wakujie utatia akili we na huyo mhasibu alieshiriki.
 
Kichwa chako wewe ndio kizito sana. Maelezo unayotoa nashindwa kuamini kama umeshawahi hata kuijua wachana na kufanya biashara kwakweli....

Ukiachana na biashara ndogondogo zetu wamachinga, TRA wako wazi kabisa kukuelekeza nini cha kufanya kama utatoa taarifa.
Fanya makadirio ya kodi wakilisha TRA, kama hujaanza biashara toa taarifa TRA na kama biashara ilikuepo lakini imesimama kwa sababu yoyote ile toa taarifa pia

Kama huelewi fika TRA watakuelekeza taratibu za kufuata, ila ukinyamaza itakugharimu
Haya acha nianze kukufahamisha Kwa njia nyengine..

Mfumo wa kukusanya kodi ninachoona mimi ni mfumo kamdamizi,

Mfano, Wewe mama D Una biashara yako ya Vijora na Mimi nafanya biashara hiyo

Wewe unapata faida Laki tano Kwa siku, Mimi napata elfu hamsini kwa siku..

Ulipoenda TRA kuwambia kuwa unataka kufungua biashara ya Vijora walikukadiria kuwa ulipe Laki mbili kwa mwaka,na hivyo hivyo..

Kwa maana Hiyo,ndio maana nathubutu nasema kuwafumo wa kukusanya kodi si rafiki kwa mfanya biashara mwenye faida ndogo

TRA haikusanyi Kodi kulingana na faida anayopata mfanyabiashara,

TRA inakusanya Kodi kulingana na biashara gani anafanya mfanya biashara..

Nafikiri Sasa umefahamu,...

Najua watu wa kupiga makofi na kusifu hata kama Kuna kasoro kwenye system nyinyi mnasifu tu

CCM must go...

Free Mazrui and all Political Prisoners
 
Tatizo kubwa la Magufuli ni usanii, yeye ni mtu mwenye roho ya korosho hapendi kabisa kuona watu wanakuwa matajiri, amerudisha utaratibu mbovu wa zamani wa serikali kufanya biashara.

Ameanzisha Tasac ili kuua makampuni ya forodha pia anataka serikali ifanye biashara ya mafuta.

Tayari serikali hii imashaua makampuni mengi ya ukandarasi baada ya serikali kuamua kujenga kwa kutumia Suma JKT na TBA...!!!

Serikali pia inaua sekta ya usafiri wa anga baada ya kuamua kufufua shirika la ndege la Atcl japo linatengeneza hasara kiasi kwamba mahesabu yake hayaruhusiwi kukaguliwa na mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali CAG kwa amri ya rais kwa kile kinachoonekana kama kuficha siri ya hasara.
 
Ni muelekeo mzuri, tuanzie hapo:-
  • Suma Jkt isiendelee kupata miradi,
  • TBA isiendelee kupata miradi, zote hizi husababisha sekta binafsi kusinyaa au kudumaa coz fedha huzungukia ndani
 
Haya acha nianze kukufahamisha Kwa njia nyengine..

Mfumo wa kukusanya kodi ninachoona mimi ni mfumo kamdamizi,

Mfano, Wewe mama D Una biashara yako ya Vijora na Mimi nafanya biashara hiyo

Wewe unapata faida Laki tano Kwa siku, Mimi napata elfu hamsini kwa siku..

Ulipoenda TRA kuwambia kuwa unataka kufungua biashara ya Vijora walikukadiria kuwa ulipe Laki mbili kwa mwaka,na hivyo hivyo..

Kwa maana Hiyo,ndio maana nathubutu nasema kuwafumo wa kukusanya kodi si rafiki kwa mfanya biashara mwenye faida ndogo

TRA haikusanyi Kodi kulingana na faida anayopata mfanyabiashara,

TRA inakusanya Kodi kulingana na biashara gani anafanya mfanya biashara..

Nafikiri Sasa umefahamu,...

Najua watu wa kupiga makofi na kusifu hata kama Kuna kasoro kwenye system nyinyi mnasifu tu

CCM must go...

Free Mazrui and all Political Prisoners
Wewe ata biashara utakuwa huna ndani ya Tanzania.

TRA awaangaiki na mtu ambae taxable turnover yake aizidi 2 million hiyo ndio threshold kwa mwaka.

Ukizidisha threshold ya 2 million ndio unatakiwa ujiunge na mfumo rasmi wa kodi na TRA chini ya hapo kodi yako ni kitambulisho cha ujasiriamali unacholipia elfu 20.
 
Ukisoma ilani ya CCM halafu ukasikiliza Ile speech ya kufungua Bunge utaweza kujipanga kujua wapi uongeze nguvu.

Kwa upande wa mikopo midogomidogo SME Serikali imejipanga, wananchi tujipange, banks na taasisi za fedha wajipange pia

Maendeleo hayana vyama
Nakuona John, na a/c yako ya kike.
Hakika unafanya kaz nzuri sana.
 
Anachosema sio anachomaanisha. Haamini katika sekta binafsi, bali anaamini katika sekta ya umma, simply huko anaweza kwenda kwa kustukiza na kuwatambua ili kusaka kiki za kisiasa.

Kwa taarifa yako hakuna muwekazaji serious atawekeza chini ya utawala wake, maana sio mtu anayejali sheria. Ukiona taifa ambalo hata mchina anakwepa kuwekeza jiulize sana.

Hapa sekta binafsi itaanza kurejea tena ilipokuwa, baada ya yeye kutoka madarakani. Rejea kilichotokea kwa wafanyabishara wa Bureau de change.
Mkuu tindo lini utaondoks kwenye kifungo cha kifikra usiwe tegemezi?

Je, kuna kiongozi yeyote upinzani, kwa sasa, mwenye sifa za kuwa Rais wa nchi hii?

Ni yapi yaliahidiwa na CCM (kama yalivhoainishwa kwenye Ilani) Serikali yake haikutekeleza?

TUACHANE NA SIASA ZA MAJUKWAANI ZIMEPITWA NA WAKATI
 
Back
Top Bottom