Hakuna anayeogopa fikra mpya,mawazo mapya utendaji mpya, maendeleo yanaletwa na mabadiliko kama vitakua na maslahi mapana ya taifa. Shida ni ubinafsi na kulazimisha uharamia uliokua umehalalishwa uendelee
CCM imebadilika tena mabadiliko chanya wakati Wapinzani sasa ndio wamevurugika, wako tayari kuiita nyeupe nyeusi.
Na hili ni dhahiri kabisa kwamba wapinzani waliokua wakijiita wapenda haki na wachukia rushwa walikua wakishirikiana mengi na wanaccm waliokua wala rushwa kwa maslahi binafsi. Sasa wale wanaccm wamekatiwa mirija wameungana na wapinzani kuipinga serikali ya rais John Pombe Magufuli.
Ule mfumo mbovu ulishavunjwa na ccm baada tuu ya NEC kumkata Lowasa na kupokelewa kwa shangwe kule CHADEMA.
CCM hai go popote, tena sasaivi imetengamaa kuishi miaka mingine 100 bila kutikiswa
CCM ni chama sio mtu, Lowasa na kundi lake walichafua nchi, amekuja John Pombe Magufuli imeiheshimisha nchi
Una uhakika kwa haya uliyoandika?matatizo makubwa tuliokuwa nayo Waafrika chini ya Jangwa la Sahara ni mfumo wetu wa kufikiri.
Wazungu wanatuita sub human being, binaadamu tuliokuwa hatajaubwa tukakamilika
Waafrika weusi tunatanguliza HISIA zetu katika kuwaza,kuamua,kulea Watoto wetu Katika kujenga hoja,nk
Naona hayo ndio yaliokukuta Wewe, HISIA za kupenda chama zimekufanya uwe mjinga
Nani alazimisha baina ya Wapinzani na Chama tawala!?
Nani amevurugika kama sio Chama Tawala, ..hao waliokimbilia Upinzani si wamerudi CCM,yuko Lowasa na wenzake?
Uchaguzi jinzi ulivyoendeshwa ni ushahidi tosha kuwa Chama tawala kimevurugika,kimechanganyikiwa
Mfumo mbovu gani umeshavunjwa,?..CCM imetawala Tanzania tangu tupate uhuru lakini bado hawajui ni mfumo gani waiendeshe Tanzania
CCM haijui Kama wao ni ma socialist,ma kommunist,wa Capitalist, wamechanganyika na hapa ndipo walipo feli
Kikwete alikuja na mfumo mzuri, sekta binafisi zilikuwa zimeshaanza kutia Sura,..
Huyu jamaa Magu kaondoa ule mfumo amekuja na wake ambao hata Nyerere ulimshinda..
Pale unapopeleka tenda zote kwa vyombo vya serikali maana yake huo ni usochalist,maana yake ni KUUWA sekta binafisi
mfumo ambao Dunia nzima umeukataa Hata hao waliouazisha
CCM imekaa Madarakani muda mwingi kiasi ambacho wamejisahau
wanaanza KUTEKA, KUTESA, KUPOTEZA wale wote ambao wanaokuja na MAWAZO na FIKRA mpya
Ili Tanzania ifanikiwe kimaendeleo ya KIUCHUMI, KIMAADILI inahitaji MAWAZO na MFUMO mpya wa kutuongoza
CCM must quit, CCM must go,56 years is enough..
Free Mazrui and all Political prisoners